Kuzaliwa katika familia maskini si dhambi kwa kuwa wewe huna uwezo wa kubadili matokeo hayo, ila katika maisha haya uliyopewa na Mungu, ukifa maskini hiyo umejitakia. Umejitakia kwa kuwa wanadamu wote tumepewa masaa 24, na uwezo wa kufanya kazi tumepewa sawa, ni namna unavyotumia muda wako ndio inaleta utofauti kati ya maskini na tajiri.
Hivyo basi kama umezaliwa familia ya kimaskini, hakikisha wewe una sacrifice maisha yako ili kizazi cha baadae waweze kuendeleza pale utakapoishia. Wewe ndio uwe wa kwanza ku break hiyo chain ya umaskini. Utavunja vipi mnyororo huo wa umaskini ndio unakuja kwenye point za mtoa mada.
Pia kujifunza namna social class za walio juu yako namna wanavyoishi na hatimaye kuendeleza utajiri walio nao, ni muhimu sana. Hii hubadili mitazamo tuliyorithi kutoka kwenye jamii tunazoishi na husaidia kuwa na mbinu tofauti za kujitafutia maendeleo. Mfano mimi napenda kufuatilia na kujifunza namna jamii ya watu wa bara Asia(wahindi, waarabu, wachina). Watu hawa miaka 100 iliyopita walikuwa kama sisi tu lakini leo hii wanachangia kwa asilimia kubwa katika uchumi wa dunia.