Umasikini ni matokeo ya fikra na sio matokeo ya mazingira

Umasikini ni matokeo ya fikra na sio matokeo ya mazingira

bongo dili

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2015
Posts
12,350
Reaction score
25,180
Umasikini upo wa aina nyingi unalengwa hapa ni ule wa kipato.

Umasikini ni matokeo ya akili kushindwa kubaini fursa zinazokuzunguka ili uzigeuze mtaji.

Popote penye watu Pana pesa,watu ndio soko lenyewe.

umasikini ni hali ya mtu kushindwa kuchukua pesa Toka kwa watu.Bakhresa anachukua pesa Toka kwa watu kwa kubadilishana na kile wanachohitaji.

Mtaji ni 4H
1. Head
2. Health
3. Hand
4. Heart

Umasikini ni laana, kuzaliwa masikini hakumfanyi mtu kuwa masikini, kutokuwa elimu sio kisingizio cha kuwa masikini.

Utajiri unaozungumzwa hapa sio ule wa ukwasi Bali wa mtu binafsi kumudu kupata mahitaji yake na ziada.
 
Mazingira hayamfanyi Mtu kuwa masikini,thus weupe wanakuja na akili na bag wakiwa masikini wanaondoka na utajiri kurudi kwao.
Pesa na mtaji wanavikutia huku
Sio kweli huwezi kuwa huna mtaji ukapa hela mala nyingi kila mwenye hili udhaminiwe uwe na kitu,ila hii kauli ya kusema heti masikini ni laani ni kutojua nini maana ya neno laana na neno masikini hiwe iwavyo masikini lazima wawepo tu hata huko mnakopaamini masikini wapo
 
Umasikini upo wa aina nyingi unalengwa hapa ni ule wa kipato.
Umasikini ni matokeo ya akili kushindwa kubaini fursa zinazokuzunguka ili uzigeuze mtaji...
Umaskini huu umeuangalia mizizi yake lakini au unaongea juu juu tu?. Ulishawahi kuona tajiri amekuwa maskini? Je ni mambo gani hutokea n kupelekea hili kuwepo?. Huu ni umaskini wa tokeo la nn?
 
Sio kweli huwezi kuwa huna mtaji ukapa hela mala nyingi kila mwenye hili udhaminiwe uwe na kitu,ila hii kauli ya kusema heti masikini ni laani ni kutojua nini maana ya neno laana na neno masikini hiwe iwavyo masikini lazima wawepo tu hata huko mnakopaamini masikini wapo
Hela ni matokeo ya wazo kuligeuza kuwa pesa.mfano
.Kumiliki taarifa za soko,malighafi,usafiri,nk then unawauzia wasio na taarifa hizo unapata pesa yaani commission
.kutumia nguvu zako kuzalisha then unauza unapata pesa.
Nguvu kwenye kilimo,uvuvi,ufugaji,nk
.unaweza ukatumia uaminifu eg kujidhamini Mali kauli upate kazi,tenda,au bidhaa za kuuza,au kifaa Cha kufanyia kazi eg pikipiki,gari,nk

Mtaji sio pesa japo pesa ni sehemu ya mtaji.pesa ni nguvu wezeshi ya kufanya jambo.
 
Umaskini huu umeuangalia mizizi yake lakini au unaongea juu juu tu?. Ulishawahi kuona tajiri amekuwa maskini? Je ni mambo gani hutokea n kupelekea hili kuwepo?. Huu ni umaskini wa tokeo la nn?
Umasikini ni matokeo ya akili kufungwa yaani kutoruhusu au kutafuta taarifa mpya zitakazokusaidia kuyachakata mazingira yako uone fursa.
ni rahisi kwa mtoto wa tajiri kuwa masikini case study zipo nyingi.
 
Back
Top Bottom