Umasikini ule ulitutesa sana, Isijirudie tena...

Nmekumbuka mbali sana mbegu za mahindi zilikuwa zinaitwa Zimbabwe, kumbe zilikuwa zimetoka Zimbabwe, sijui kama bado zipo, nimeziona nineties, nilikuwa mdogo sana enz hizo..
Ni kweli kabisa zipo ni vile sasa Mkukima akishavuna anachagua yale ya Mbegu ana hifadhi kwa ajili mwaka unaofuata
 
Nae
Nakumbuka vizuri kipindi hiki Nyerere alituahidi miezi 18 ya njaa lakini badala yake ikawa ni ufukara wa kudumu, mbaya zaidi akamteuwa waziri mkuu kichaa ndio ikawa mshike mshike hasa.

Ila mimi mtaani kwetu tulipata bahati tulikuwa na brother ni mtundu wa kuiga signature gari la ugawaji likija foneni ya kuweka sign kwenye vitabu tulikuwa hatukai jamaa akiangalia tu zile saini za makarani wa siku hiyo mchezo umeisha anazipiga vilevile

Ila Zimbabwe inasikisha zaidi mwaka 1997 nilipita Zimbabwe transit nakumbuka nilitoa noti ya Zim dola 5 kununuwa hot dog na cicacola can lakini bado nilirudishiwa chenji ya kwacha kadhaa by that time Zimbabwe walikuwa wanatumia sarafu mbili kwa wakati mmoja ila Zim dola ilukuwa powerfull zaidi ilikuwa ikichuana na Rand ya Sourh Africa na Pula ya Botswana.

By the way jana Pasaka jana mji umepowa utadhani ni karume day, nadhani wenzetu wanaccm walikuwa sehemu yao maalum wanafurahia sikukuu.
 
Kama ndio hivyo kwa nini tusiwarusu wafanye kazi yao.
Mku mficha maradhi mwisho huumbuka kwa nini hujiulizi ukimya wa viongozi unasababishwa ni hili kwa dunia ya sasa hakuna kinafichika kwani iko wazi sana.
Asikudanganye mtu the world is controlled
 
Kama ndio hivyo kwa nini tusiwarusu wafanye kazi yao.
Mku mficha maradhi mwisho huumbuka kwa nini hujiulizi ukimya wa viongozi unasababishwa ni hili kwa dunia ya sasa hakuna kinafichika kwani iko wazi sana.
Angalia budget hadi Leo hela wanatoa nani?
Mimi na wewe tu ,tukiacha hela nyumbani lazima ufuatilie, hela uliyoiacha na matumizi ya kulishwa mchicha vinaendana?it's a natural law when you are dependant ,so ni ujinga tu kutunushia misuli ma sponsor wako ,it's the matter of time
 
Dah zilikuwa siku mbaya sanatorium, tumuombe Mungu zisirudi. Nakumbuka chenga za unga wa mahindi zinapikwa ubwabwa!
Tunataka kumtwisha Mungu jukumu lisilokuwa lake. Katuumba tofauti na wanyama kwa kutupa akili na utashi ili tuweze kuitawala dunia na vilivyomo. Tukishindwa kutatua matatizo yetu sisi wenyewe hilo ni tatizo letu na siyo lake!
 
Mku hayo maisha tuliyochaguliwa kuyaishi pasipo kuangalia madhara yake huko tuendako na kama mazingira yanavyoonyesha sasa hivi huko mikoani Mvua hazijashesha na mambo yalivyo sijui itakuwaje
 
natamani sana kungetengenezwa documentary/ makala ya watu walioishu enzi hizi wakielezea hali ilivyo huku ikiwa na video zilizochukuliwa enzi hizo huku wataalamu wa historia na wachumu wakisimulia chanzo cha ushu hiyo.

it is very intersting story.
 
na kuna mengi ya kutengenezea historical documentaries, kwa mfano chaguzi zetu za uraisi zungetengenezewa docymentary, inafurahisha sana kusikiliza juu ya akina mrema, slaa, mbowe na kina lowassa na kuundwa kwa UKAWA jinsi kulivyowahi kutikisa nchi kipindi cha chaguzi, hayo ndio.mambo ya kutengenezea docimentary
it is very interesting
 
natamani sana kungetengenezwa documentary/ makala ya watu walioishu enzi hizi wakielezea hali ilivyo huku ikiwa na video zilizochukuliwa enzi hizo huku wataalamu wa historia na wachumu wakisimulia chanzo cha ushu hiyo.

it is very intersting story.
Tulikuwa hatuna majani ya chai hizo Kamera za kupigia picha za Video zingetoka wapi ndugu yangu!?
 
Umesema ukweli na kunikumbusha mbali ila tofauti na sasa, wakati ule angalao pesa ilikuwepo sasa hata pesa hakuna mtaani hali itakuwa mbaya sana. Heri dikteta mwenye akili kuliko dikteta kilaza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…