Umasikini ule ulitutesa sana, Isijirudie tena...

Maisha yalikuwa mabaya sana lakini tuliambiwa hakuna namna ni lazima tuishi kama ilivyokuwa. Mwalimu alikataa kugeuka nyuma ili asije kugeuka jiwe. Mwinyi ndiye alikuja kuruhusu biashara huria na vitu toka Kenya kuingia Tanzania.

Nyerere hakuweza shindanana IMF pia pressure ya mabdaliko ya kidunia,awareness ya wananchi baada ya kuwapa elimu wakaanza kuuona mwanga,na kwa kuwa hakuwa Mwizi akaona ni heri apishe upepo abaki kama mlezi wa taifa, angekuwa mwizi na mpenda anasa angeng'ang'ania Madaraka kama madikteta wengine kina Mugabe, kilichomsaidia MWALIMU ni dini kusali kwa dhati na si kujaza mabenchi hivo akazishinda tamaa za nafsi ambazo uzaa kuiba kodi za wanyonge, kuwaua,kuwatesa,kuwafilishi,kuwafanya wawe masikini ili nafsi ifurahi kama wafanyavo madikteta.
 
Mkuu, ume no chekesha SAAANA,
Hakika PASAKA INOGILEEEEE
 

Kilio cha wengi Mungu ukisikia twaamini atatenda,siasa ni upepo si hesabu jibu lzm liwe moja.Kupitia upepo hata yye akutegemea pia kupitia upepo chochote chaweza tokea.
 
Mfikirie na aliyewatoa huko.
Ni IMF kupitia SAP, sera ambayo mwl nyerere alipata uzito sana kutekeleza ikabidi ampe Mwinyi nchi. Rais mwinyi alitekeleza sap kwa mikono miwili kupitia slogan yake ya 'rukhsa'. Hiyo ndiyo ikawa pona yetu kama taifa.
Kwa hiyo muwe mnaheshimu IMF, siyo kitu chepesi kama mnavyodhani hapo lumumba.
 
Kwahiyo IMF walikuza uchumi wa tz!!!
 
Yes ,uchumi unareflect maisha ya watu na kukuza pato LA MTU sio vitu.Awamu ya kwanza na ya tano wamefeli kwenye uchumi, na wote wanatoka Kanda ya ziwa,tujaribu Kanda zingine pia
Ikulu sio uwanja wa majaribio, awamu ya kwanza na ya tano zote ni awamu za mapinduzi, lazima kuwepo maumivu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…