Umasikini wa mtu unaanzia kichwani pake. Kama utani nilivyopoteza mtaji wangu wote kizembe

Ndio mkuu kikubwa nikuziba myanya ya pesa zinapo potelea
 
Ndio mkuu kikubwa nikuziba myanya ya pesa zinapo potelea
Yaani maswala ya pesa Mkuu ni changamoto sijui kwa wengine lakini naamini hata waliofanikiwa sana ukifuatilia utagundua changamoto kama hizi walikutana nazo,

Mimi kipindi cha nyuma iliwahinitokea sikuwa na pesa lakini nilikuwa na plan nzuri sana, nilikuja pata pesa tena ya mkopo 7m aseee plan zote ziliyeyuka hewani zikaja zingine, Nimekuja kupata akili tayari nimepoteza Zaidi ya 70%.
Nikachukua risk kwa tahadhari nikawekeza kwenye moja ya plan zangu za awali japo kwa kusua sua na mtaji huku nikitegemea mshahara kulipa marejesho aseeee biashara na yenyewe ikawa haileti hesabu ni hasara tu (yaani msimamizi akawa mjanja mjanja)

Nikaachana nae nikatafuta mwingine, kidogo ikawa afadhali nikaona mwanga biashara ikakua nikamaliza deni.
Nikachukua tena mkopo tena mkubwa kidogo zaidi ya awali, nikaongeza mtaji kwenye bzness, nikaanzisha zingine mbili,

Bahati mbaya zile biashara mpya zote zilikufa na mtaji, nikajifunza kitu sikufanya tathmin ya kutosha pia usimamizi mbovu.
Kupitia biashara ya kwanza nikapata tena kianzio nikaanzisha ujasiriamali na bizness ndogo ndogo nyingine.

Bado naendelea kulipa deni, Nili apa nikimaliza sichukui tena pesa ya mkopo bila kuwa na tathmin ya kutosha.

Pesa ya mkupuo si yakutegemea sana, kwanini matajiri ni wachache kuliko maskini ni kwa sababu ya nidham ya pesa, Wote tunapata pesa ila inategemea unainvest wapi pia uwezo wa kuifanya igenerate hata kama ikiyumba unakuwa na uelewa wa kuifanya ikue tena sasa pesa ya pamoja(mkupuo) ukiipoteza kuirudisha ni mtihani mwingine.
 
Uzoefu murua ndugu, shukrani sana.
 
Hahaahahahah dah aisee sijui nikutafute nikupe story yangu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
uliona wapi pesa ya kamari ikafanya la maana...
pesa n pesa tu mzee hakunaga pesa ya kamari, ya mshahara wala ya sadaka. na ndio maana ukiwa na sh 1000 hata iwe ya kamari au ya sadaka au ya kuiba au ya kupewa ukienda dukan utapata vocha ya 1000 haijalish hyo pesa umeipataje.....kinachomata n thaman na sio chanzo cha pesa
 
Hayo maelezo umeyaelekeza kwa mtu hasiye sahihi. Mimi pia nina uelewa kama huo kwamba pesa ni pesa
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] kweli mkuu. Unakuta mtu kafanya kazi miaka 40 anapewa mafao million zaidi ya 100 baada ya miaka 2 unakuta kazitumbua zote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…