Umasikini wa Tanzania ni matokeo ya mfumo mbovu wa Elimu yetu, kujaza wenye Degree mtaani ni ujinga mkubwa sana

Umasikini wa Tanzania ni matokeo ya mfumo mbovu wa Elimu yetu, kujaza wenye Degree mtaani ni ujinga mkubwa sana

RNA

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2013
Posts
1,647
Reaction score
2,803
Nchi yetu ni Maskini sana na wananchi wake ni maskini sana ,kiasi kwamba bado kuna wanakufaa kwa kukosa Matibabu ,Njaa na kukosa malazi.

Najiuliza sana Hawa Wasomi waliopo serikalini na kwenye Uongozi wanatudia kweli?

Sababu kubwa ikiwa ni Siasa ndani ya mfumo Elimu .Nchi yetu ina Mali asili nyingi sana ambazo tungeweza tumia kwa kutengeneza Mali na vifaa tukaweza uza nje.

Kwa kifupi Tunahitaji Mafundi Bomba, Ujenzi, Makarani, Umeme, Ushonaji ,Uvuvi, Komyuta na nk.

Kwa maana Nyingine Tunahitaji Kuwa na Vyuo vingi vya Ufundi kuliko kutengeneza Wasomi wengi wa Digrii ambao Ujuzi wao na uelewe ni sawa na Fundi wa darasa la 7 au kidato cha 4.

Kibaya Zaidi hawa wasomi wa Digrii ndio miaka yote wanaaminika na kuwekwa kwenye Nyazifa za Uongozi kana Kwamba kwa kuwa na hizo Digrii kunalisaidia Taifa kumbe hawana kitu.

Wengi wao watataka wawe na Mali nyingi ziendane na elimu Zao.

Lakini hata Uelewa wao ni mdogo sana kulinganish na elimu zao hivyo wanalipoteza Taifa tu.

Mwisho Kabisa ni Bora tukajenga vyuo vingi vya Ufundi na Viwanda Tukaachana na Hawa watu wanaoitwa Wasomi waliojazana kwenye Siasa sijui Prof ,Doctor ,Wanasheria Wasomi na Nk ambao hawana mchango sana zaidi digrii zao .
 
Tcu wanafungua mfumo muda sio mrefu, kajiunge upate digrii nyingine ili uje ugundue.
Hata usomeje kama hauna hela hugundui.
 
Mnanikera sana mnaodharau wenzenu kisa mfumo umewagomea. Huwezi kufanikiwa kwa kumchukia mwenye nacho. Wewe unamchukia mwenye digrii lakini Hilo halikufanyi mawe kuwa na digrii zaidi yakuumia Kama jamaa yako mbunge msukuma.
 
Walamba asali hawatakuelewa.

Huwa najiuliza..nchi inasema ina utoshelezi wa waalimu wakutosha..na mtaani wamejaa na kila mwaka vyuo vinaleta mtaani walimu maelfu kwa maelfu.

Kunahaja gani ya kuendelea kuzalisha walimu wengi hivyo..kwanini wasilimit namba iwe ndogo au wasitishe uzalishaji wa walimu.
 
Mkuu, tunahitaji taifa lenye wasomi,fundi rangi awe na PhD
 
Hao walisomea 'Digrii' bila kuendelea kwani kuna Mtu/Serikali iliyewatuma?
 
Hela ya corona imeongeza na kuboresha madarasa zaidi ili wasomi waongozeke .
 
Bila kuwa na wasomi wenye digrii Nani atawafundisha hao wa vyuo vya kati?
Vipi kuhusu walimu wakiwa na kiwango kidogo cha elimu?.
 
Back
Top Bottom