Umasikini wa Watanzania chanzo chake ni kupenda kujenga nyumba ya kuishi kwanza badala ya kuanzisha biashara

Nitakutafuta mkuu
 
Kwa uchumi wangu wa sasa Itanilazimu kila nikipatacho kisifanyie jambo lolote isipokua kujenga..
Kwa ufupi nitajitesa sana, Kujenga nyumba isiwe sababu ya kuteseka,

Usitake kuniambia hata wewe ulijenga nyumba ya 30mil kwa kusimamisha kila kitu, ila ilifikia kipindi uchumi unaruhusu hivyo bila kukuathiti sana ndio ukajenga.

Sasa mimi hio level sijafikia, unatakiwa uelewe hapo, hakuna asiyetaka kua na kwake, Kujenga kwa sasa sio priority kwangu sababu Silazimiki ila kuweka uchumi wangu sawa kibiashara ndio priority na nalazimika,
Na kwa sababu gani nalazimika kwa hili...
Moja ya sababu ndio kama hioo ya kuandaa mazingira Nijenge kabla ya Muda niliojiwekea haujafika/pita, Naamisha kabla ya ule mda wa kujenga kwa lazima haujanifikia.
 
miaka arobaini unapanga kwa kodi ya 200k
ni ujinga na ufujaji wa hela, unatoa nyumba za 'maana' kwa iyo fedha
Angalia wahindi muhind anapanga nyumba kariakoo juu mfano analipa laki mbili kwa mwezi duka lake liko chini hapo hapo anapoishi hana gharama za usafiri wala chakula cha mchana mswahili hataki kulipa pango.laki mbili anaona bora akajenge nyumba yake kimara awe anakuja kwenye duka lake lililoko kariakoo la kuuza nguo gharama za kuweka mafuta kwenye gari yake kila siku ni elfu 20 kwa mwezi anatumia laki sita !! Kula yeye na mkewe chakula mchana wanatumia elfu kumi wote wawili kula hotelini kwa mwezi wanatumia laki tatu muhindi anakula kwake .Hapo nani mjinga Kati ya muhindi anayepanga na mswahili anayekaa kwake kwenye bungalow lake kimara? Piga hesabu kwa miaka 40 ,nani atakuwa lofa hapo Kati ya muhindi na mswahili
 
Nilichojifunza ni kwamba wewe bado hujayaanza maisha, bado unatafutatafuta au laah basi kile chama chako pendo kimepasua ufahamu wako.
 
Hata mtu mzima kabisa anakosea ktk baadhi ya matendo yake

lakini kukosea kwake hakumaanishi kua anachokifanya yupo sahihi

ukiwa kama mtoto unaetaka kufika mahali,yapasa ujue kuchuja mazuri na mabaya

chukua mazuri acha mabaya,songa mbele Wahindi wana mazuri mengi ila hilo la kupanga HAPANA.
 
Kwahiyo wewe mbuzi, sisi tuache kuishi maisha yetu kama watu weusi "tuanze kukopi kila kitu, kila lifestyle ya Mhindi???
 
Nadhani tumeelewana mie nilianza kujenga baada ya kuwa na fedha ya kuniwezesha kujenga kipindi hicho. Cha muhimu panga mipango yako ikikaa vizuri jenga ukae kwako. Ukiwa na kwako hata kibiashara utasimamaSio leo pango la biashara kesho la nyumba utaumia zaidi. Na ukioa na kupata watoto ndio hatari zaidi maana wakianza kusoma gharama zake ni kubwa mno kama ulikuwa hujajiandaa kimakazi unaweza usijenge tena
 
Wapo waliowahi kumiliki pesa na biashara kubwa na walijenga nyumba za maana Leo hii hizo nyumba ndio kitu pekee wanachoweza kujivunia sababu pesa na biashara zilikufa wapo pia waliokua na biashara kubwa lakini hawakujenga leo imebaki tu historia kua walikua na pesa hawana cha maana kinachoweza kuthibitisha kua walikua na pesa
 
Chanzo kimojawapo kuu cha Umaskini kwa watanzania wengi ni kuamini USHIRIKINA kivitendo; hata wasomi !

Kuamini ushirikina ni chanzo cha laani kama ilivyoandikwa katika vitabu vitakatifu " Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri, 11 wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu. 12 Kwa maana mtu atendaye hayo ni chukizo kwa Mungu;"; ...........................
 
Je, ukilipa kodi ya nyumba inazalisha? Kama unapanga na inakugharimu ni bora kujenga na kuwa na nyumba na kutolipa kodi. Kulipa kodi kwa mtu ni kumtajirisha. inabidi kila mja awe na kwake yawe makazi bora au ya wastani kwako ni kwako.
roho ya kichawi hio
 
Huwa nawashangaa sana watu kama nyie mnaofananisha maisha ya wahindi na wabongo..
Nachelea kusema kwamba huna unalojua lolote kuhusu hao jamaa na wewe ni mmoja ya watanzania wasio na akili ya kufafanua mambo kwa uwanda mpana zaidi..
Pili unaonekana wewe ni maskini wa vyote..akili, pesa na afya vile vile.
Nenda kafanye homework chunguza bishara zao chunguza vyanzo vya biashara zao..kisha uje hapa ukiwa umekuwa kiakil na kifikra
 
Hayo majengo huko Uhindini na Uzunguni wamejengewa na watanzania??

Wenzetu huku wanatafuta maisha ndo maana wanapanga kama ilivyo tu kwa wabeba box na wengineo huko ugenini, lakini mwisho wa siku wanajengwa kwao.
 
Mkuu kwa upade mmoja uaweza kuwa upo sawa lakini kwa upandede mwingine mtazamo wako unapwaya!
Kwa mtumishi wa umma kuishi kweye yuma za kupaga aibu labda tu kama mhusika hajitamubui!
Pia kwa mazingira ya Tanzania unapoacha kutumia mkopo wako kujenga nyuma yako ya makazi na kuupandikiza kwenye iashara you need to think twice unaweza usirudishe hata ile ya kulipia panngo la nyumba unapokaa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…