Umasikini wa Watanzania chanzo chake ni kupenda kujenga nyumba ya kuishi kwanza badala ya kuanzisha biashara

Umasikini wa Watanzania chanzo chake ni kupenda kujenga nyumba ya kuishi kwanza badala ya kuanzisha biashara

Najua umri wako ni mdogo na unaongea hivi kwa kuwa hujui kuwa muda ni suala la kutilia sana maanani. Unavyochelewa utakuta uwezi kujenga kabisa kwa kuwa ujenzi unahitaji timing sana.

Mie nilianza kujenga nyumba ya kawaida sana at my early 30 nyumba ya milioni kama 30 hivi na baadae nikajenga nyingine ya kama milioni 40 eneo lilikuwa kubwa 860 square meters. Baada ya hapo nilipokaribia 40 ndio nikaanza kujenga dream house ambayo imenigharimu like 250 million ambayo ndio ninaishi kwa sasa. Baada ya kuona utamu wa kodi niliamua kujenga nyumba ndogo ndogo za kisasa (vyumba viwili na sebule) maeneo mbalimbali jijini ambayo kwangu ni biashara nzuri na rahisi nakusanya kodi kwenye nyumba nyingine najenga mpya mdogo mdogo.

Kwa kukushauri usifikirie sana kujenga nyumba kubwa sana bali jenga ambayo una uwezo nayo ila akikisha iwe nzuri sana kwa ramani madirisha makubwa na isiwe fupi na unapojenga mapema hamia na kama pesa ipo ndipo ufikirie kujenga nyumba kulingana na uwezo wako kipindi hicho. Kwenye ujenzi usijifananishe na mtu. Ujenzi una awamu zake. Waliojenga kipindi cha awamu ya nne simenti elfu 11 ni tofauti na wanaojenga sasa hivi simenti elfu 17 mpk 20. Kwa sasa utateseka zaidi so ni bora ujenge unachokiweza leo.

Nimeshauri kutokana na niliyopitia mie ambayo nahisi ni njia sahihi ukilinganisha na wenzangu wengi wenye kazi na biashara kama zangu ila walikosea tu timing
Nitakutafuta mkuu
 
Tatizo ni nini mpk ukijenga nyumba ya milioni 40 tuanike maturubai? Je ukijenga ya milioni 200 hawataanika maturubai. Shtuka ndugu yangu time is not on your side. Liwezekanalo leo lisingoje kesho, huu usemi una maana kubwa sana. Wazungu wanasema "make things high when sun shine" ikifika usiku imekula kwako
Kwa uchumi wangu wa sasa Itanilazimu kila nikipatacho kisifanyie jambo lolote isipokua kujenga..
Kwa ufupi nitajitesa sana, Kujenga nyumba isiwe sababu ya kuteseka,

Usitake kuniambia hata wewe ulijenga nyumba ya 30mil kwa kusimamisha kila kitu, ila ilifikia kipindi uchumi unaruhusu hivyo bila kukuathiti sana ndio ukajenga.

Sasa mimi hio level sijafikia, unatakiwa uelewe hapo, hakuna asiyetaka kua na kwake, Kujenga kwa sasa sio priority kwangu sababu Silazimiki ila kuweka uchumi wangu sawa kibiashara ndio priority na nalazimika,
Na kwa sababu gani nalazimika kwa hili...
Moja ya sababu ndio kama hioo ya kuandaa mazingira Nijenge kabla ya Muda niliojiwekea haujafika/pita, Naamisha kabla ya ule mda wa kujenga kwa lazima haujanifikia.
 
miaka arobaini unapanga kwa kodi ya 200k
ni ujinga na ufujaji wa hela, unatoa nyumba za 'maana' kwa iyo fedha
Angalia wahindi muhind anapanga nyumba kariakoo juu mfano analipa laki mbili kwa mwezi duka lake liko chini hapo hapo anapoishi hana gharama za usafiri wala chakula cha mchana mswahili hataki kulipa pango.laki mbili anaona bora akajenge nyumba yake kimara awe anakuja kwenye duka lake lililoko kariakoo la kuuza nguo gharama za kuweka mafuta kwenye gari yake kila siku ni elfu 20 kwa mwezi anatumia laki sita !! Kula yeye na mkewe chakula mchana wanatumia elfu kumi wote wawili kula hotelini kwa mwezi wanatumia laki tatu muhindi anakula kwake .Hapo nani mjinga Kati ya muhindi anayepanga na mswahili anayekaa kwake kwenye bungalow lake kimara? Piga hesabu kwa miaka 40 ,nani atakuwa lofa hapo Kati ya muhindi na mswahili
 
Wahindi wanaishi nyumba za kupanga na wanaongoxa kwa uwezo wa kukopesheka kwenye mabenki akienda kukopa hachukui hata masaa mawili mkopo unaingia kwenye akaunti yake!!! Wanatumia pesa zilizoko kwenye fixed deposit akaunti zao kama dhamana!!! Huku fixed deposit insendelea kuingiza faida ya riba wakati huo huo inatumia kama dhamana mkopo kule aliochukua imeendelea kuzalisha faida anapata pesa kotekote kwenye fixed na mkopo anaofanyia biashara

Sasa wewe mwenye hilo.jumba lako la kulala na ukiliweka dhamana halingizi hata Mia kipindi chote cha mkopo tofauti na muhindi aliyeona miliki ajenge nyumba heri pesa za hiyo nyumba aziweke kwenye fixed deposit akaunti awe anaitumia kukopea chap chap na pesa kuingia akaunti haraka afanyie biashara

Unajua maana ya Asset ? Asset ni mali inayoingiza pa to A property that generates income is called Asset.Nyumba ya kulala na kuamka sio Asset ni Liability!! Hata liwe la ghorofa

Hiyo nyumba us kulala na kuiita Asset sio sahihi
Nilichojifunza ni kwamba wewe bado hujayaanza maisha, bado unatafutatafuta au laah basi kile chama chako pendo kimepasua ufahamu wako.
 
Hata mtu mzima kabisa anakosea ktk baadhi ya matendo yake

lakini kukosea kwake hakumaanishi kua anachokifanya yupo sahihi

ukiwa kama mtoto unaetaka kufika mahali,yapasa ujue kuchuja mazuri na mabaya

chukua mazuri acha mabaya,songa mbele Wahindi wana mazuri mengi ila hilo la kupanga HAPANA.
 
Hakuna watu wanapenda kujenga nyumba za kuishi duniani kama Watanzania.

Ndoto kuu ya kwanza ya Mtanzania yeyote ngozi nyeusi ni kuwa na kwake hivyo akipenda vihela huvipeleka site kujenga nyumba ya kuishi hapa ndio siri ya umasikini wa Watanzania ngozi nyeusi kuanzia.

Wenzetu Wahindi hupanga hata miaka arobaini pesa zake akiweka na kukuza biashara yake. Wazo lake la kwanza huwa nikipata pesa natafuta nyumba ya bei rahisi ya kupanga halafu hela inayobaki naanzisha biashara. Wote mashahidi Wahindi matajiri hasa lakini maisha yote wanaishi nyumba za kupanga za National Housing. Sisi Waswahili tunashindana kujenga nyumba za kuishi za kulala na kuamka za mamilioni.

Waswahili hatushindani kwenye uwekezaji tunashindana kwenye nani kujenga nyumba kali kuliko mwingine! Hata waswahili wakiudhiana wakianza kutukanana isi mojawapo huwa kwani wewe una nini? Mimi Nina kwangu nimejenga nyumba za kuishi moja hapa mjini ingine kijijini

Nchi ziliizoendelea watu huwaza kuwekeza kwanza kama ndoto ya kwanza akipata pesa.

Hapa ndio siri ya umaskini wa waswahili ilipo.ndoto zenu za kwanza ni kwenye vitu visivyozalisha pesa hasa nyumba ya kulala na kuamka.
Kwahiyo wewe mbuzi, sisi tuache kuishi maisha yetu kama watu weusi "tuanze kukopi kila kitu, kila lifestyle ya Mhindi???
 
Kwa uchumi wangu wa sasa Itanilazimu kila nikipatacho kisifanyie jambo lolote isipokua kujenga..
Kwa ufupi nitajitesa sana, Kujenga nyumba isiwe sababu ya kuteseka,

Usitake kuniambia hata wewe ulijenga nyumba ya 30mil kwa kusimamisha kila kitu, ila ilifikia kipindi uchumi unaruhusu hivyo bila kukuathiti sana ndio ukajenga.

Sasa mimi hio level sijafikia, unatakiwa uelewe hapo, hakuna asiyetaka kua na kwake, Kujenga kwa sasa sio priority kwangu sababu Silazimiki ila kuweka uchumi wangu sawa kibiashara ndio priority na nalazimika,
Na kwa sababu gani nalazimika kwa hili...
Moja ya sababu ndio kama hioo ya kuandaa mazingira Nijenge kabla ya Muda niliojiwekea haujafika/pita, Naamisha kabla ya ule mda wa kujenga kwa lazima haujanifikia.
Nadhani tumeelewana mie nilianza kujenga baada ya kuwa na fedha ya kuniwezesha kujenga kipindi hicho. Cha muhimu panga mipango yako ikikaa vizuri jenga ukae kwako. Ukiwa na kwako hata kibiashara utasimamaSio leo pango la biashara kesho la nyumba utaumia zaidi. Na ukioa na kupata watoto ndio hatari zaidi maana wakianza kusoma gharama zake ni kubwa mno kama ulikuwa hujajiandaa kimakazi unaweza usijenge tena
 
Wapo waliowahi kumiliki pesa na biashara kubwa na walijenga nyumba za maana Leo hii hizo nyumba ndio kitu pekee wanachoweza kujivunia sababu pesa na biashara zilikufa wapo pia waliokua na biashara kubwa lakini hawakujenga leo imebaki tu historia kua walikua na pesa hawana cha maana kinachoweza kuthibitisha kua walikua na pesa
 
Hakuna watu wanapenda kujenga nyumba za kuishi duniani kama Watanzania.

Ndoto kuu ya kwanza ya Mtanzania yeyote ngozi nyeusi ni kuwa na kwake hivyo akipenda vihela huvipeleka site kujenga nyumba ya kuishi hapa ndio siri ya umasikini wa Watanzania ngozi nyeusi kuanzia.

Wenzetu Wahindi hupanga hata miaka arobaini pesa zake akiweka na kukuza biashara yake. Wazo lake la kwanza huwa nikipata pesa natafuta nyumba ya bei rahisi ya kupanga halafu hela inayobaki naanzisha biashara. Wote mashahidi Wahindi matajiri hasa lakini maisha yote wanaishi nyumba za kupanga za National Housing. Sisi Waswahili tunashindana kujenga nyumba za kuishi za kulala na kuamka za mamilioni.

Waswahili hatushindani kwenye uwekezaji tunashindana kwenye nani kujenga nyumba kali kuliko mwingine! Hata waswahili wakiudhiana wakianza kutukanana isi mojawapo huwa kwani wewe una nini? Mimi Nina kwangu nimejenga nyumba za kuishi moja hapa mjini ingine kijijini

Nchi ziliizoendelea watu huwaza kuwekeza kwanza kama ndoto ya kwanza akipata pesa.

Hapa ndio siri ya umaskini wa waswahili ilipo.ndoto zenu za kwanza ni kwenye vitu visivyozalisha pesa hasa nyumba ya kulala na kuamka.
Chanzo kimojawapo kuu cha Umaskini kwa watanzania wengi ni kuamini USHIRIKINA kivitendo; hata wasomi !

Kuamini ushirikina ni chanzo cha laani kama ilivyoandikwa katika vitabu vitakatifu " Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri, 11 wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu. 12 Kwa maana mtu atendaye hayo ni chukizo kwa Mungu;"; ...........................
 
Je, ukilipa kodi ya nyumba inazalisha? Kama unapanga na inakugharimu ni bora kujenga na kuwa na nyumba na kutolipa kodi. Kulipa kodi kwa mtu ni kumtajirisha. inabidi kila mja awe na kwake yawe makazi bora au ya wastani kwako ni kwako.
roho ya kichawi hio
 
Hakuna watu wanapenda kujenga nyumba za kuishi duniani kama Watanzania.

Ndoto kuu ya kwanza ya Mtanzania yeyote ngozi nyeusi ni kuwa na kwake hivyo akipenda vihela huvipeleka site kujenga nyumba ya kuishi hapa ndio siri ya umasikini wa Watanzania ngozi nyeusi kuanzia.

Wenzetu Wahindi hupanga hata miaka arobaini pesa zake akiweka na kukuza biashara yake. Wazo lake la kwanza huwa nikipata pesa natafuta nyumba ya bei rahisi ya kupanga halafu hela inayobaki naanzisha biashara. Wote mashahidi Wahindi matajiri hasa lakini maisha yote wanaishi nyumba za kupanga za National Housing. Sisi Waswahili tunashindana kujenga nyumba za kuishi za kulala na kuamka za mamilioni.

Waswahili hatushindani kwenye uwekezaji tunashindana kwenye nani kujenga nyumba kali kuliko mwingine! Hata waswahili wakiudhiana wakianza kutukanana isi mojawapo huwa kwani wewe una nini? Mimi Nina kwangu nimejenga nyumba za kuishi moja hapa mjini ingine kijijini

Nchi ziliizoendelea watu huwaza kuwekeza kwanza kama ndoto ya kwanza akipata pesa.

Hapa ndio siri ya umaskini wa waswahili ilipo.ndoto zenu za kwanza ni kwenye vitu visivyozalisha pesa hasa nyumba ya kulala na kuamka.
Huwa nawashangaa sana watu kama nyie mnaofananisha maisha ya wahindi na wabongo..
Nachelea kusema kwamba huna unalojua lolote kuhusu hao jamaa na wewe ni mmoja ya watanzania wasio na akili ya kufafanua mambo kwa uwanda mpana zaidi..
Pili unaonekana wewe ni maskini wa vyote..akili, pesa na afya vile vile.
Nenda kafanye homework chunguza bishara zao chunguza vyanzo vya biashara zao..kisha uje hapa ukiwa umekuwa kiakil na kifikra
 
Hayo majengo huko Uhindini na Uzunguni wamejengewa na watanzania??

Wenzetu huku wanatafuta maisha ndo maana wanapanga kama ilivyo tu kwa wabeba box na wengineo huko ugenini, lakini mwisho wa siku wanajengwa kwao.
 
Mkuu kwa upade mmoja uaweza kuwa upo sawa lakini kwa upandede mwingine mtazamo wako unapwaya!
Kwa mtumishi wa umma kuishi kweye yuma za kupaga aibu labda tu kama mhusika hajitamubui!
Pia kwa mazingira ya Tanzania unapoacha kutumia mkopo wako kujenga nyuma yako ya makazi na kuupandikiza kwenye iashara you need to think twice unaweza usirudishe hata ile ya kulipia panngo la nyumba unapokaa!
 
Back
Top Bottom