Kwa uchumi wangu wa sasa Itanilazimu kila nikipatacho kisifanyie jambo lolote isipokua kujenga..
Kwa ufupi nitajitesa sana, Kujenga nyumba isiwe sababu ya kuteseka,
Usitake kuniambia hata wewe ulijenga nyumba ya 30mil kwa kusimamisha kila kitu, ila ilifikia kipindi uchumi unaruhusu hivyo bila kukuathiti sana ndio ukajenga.
Sasa mimi hio level sijafikia, unatakiwa uelewe hapo, hakuna asiyetaka kua na kwake, Kujenga kwa sasa sio priority kwangu sababu Silazimiki ila kuweka uchumi wangu sawa kibiashara ndio priority na nalazimika,
Na kwa sababu gani nalazimika kwa hili...
Moja ya sababu ndio kama hioo ya kuandaa mazingira Nijenge kabla ya Muda niliojiwekea haujafika/pita, Naamisha kabla ya ule mda wa kujenga kwa lazima haujanifikia.