Umasikini wa Watanzania chanzo chake ni kupenda kujenga nyumba ya kuishi kwanza badala ya kuanzisha biashara

Hapana mie napenda tu ujenzi. Niliona biashara easy kwangu ni kujenga na kupangisha watu (real estate) haina stress kama biashara nyingine na pia unaifanya huku unaendelea na kazi zake za kuajiriwa. All in all mtu ukiwa na makazi yako inakuondolea sana usumbufu ingawa katika stage fulani ya maisha lazima upange ila mambo yakikaa sawa jenga. Wapangaji wangu wengi nawashauri hivi
Asante, nimejifunza kitu kutoka kwake. Nitafanyia kazi insha Allah
 
Je ukilipa kodi ya nyumba inazalisha? Kama unapanga na inakugharimu ni bora kujenga na kuwa na nyumba na kutolipa kodi. Kulipa kodi kwa mtu ni kumtajirisha. inabidi kila mja awe na kwake yawe makazi bora au ya wastani kwako ni kwako
Mkuu Tatizo sio tuu kujenga tatizo unajenga nini...
Nikijenga Sasahivi Nitajenga upuuzi tuu.

Hicho kitu SITAKI, nimeandika kwa herufi kubwa kama msisitiozo,
Kuliko kujenga kijumba hakieleweki Miaka hii bora niishie kupanga,

Ila siwezi jenga nyumba kama aliyojenga babu miaka ya 60s, Narudia bora niishie kupanga kuliko kuchafua ardhi.

Masuala unajenga nyumba yako, Unaiongelea mbele ya wenzako baada ya kuita nyumba unaita Kibanda(na kweli unamaanisha) mimi siwezi.

Nikitaka hicho kibanda eti ilimradi nijiegamize kwangu hata leo naweza na wengi humu naamini wanaweza...
Ila maisha ya leo kuishi kinyonge kuanzia ndani mpk nje hapana.
 
Kodi ya nyumba ni kati ya vitu vinavyotafuna mtaji wa biashara kuliko maelezo..umepanga nyumba ya wastani ya laki nne kila mwezi. Kutoa kiasi hiki kama kodi ya nyumba toka kwenye pato la biashara ni pesa nyingi sana. Usipokuwa makini unaweza ukayumba hata kibiashara. Kumbuka bado biashara ina gharama zake za uendeshaji ikiwemo kodi ya ofisi, mishahara, etc.

Usipo kuwa makini utajikuta milioni inachomoka kila mwezi kwaajili ya kodi pekee.....haina afya kibiashara.

Kingine ni swala la kukopesheka na taasisi za fedha. Biashara haiwezi kusimama bila mikopo, na hakuna mkopo bila dhamana. Siku hizi hawapokei tena eneo lisiloendelezwa kama dhamana ya mkopo. Wanahitaji nyumba. Huna nyumba utatumia muda mwingi sana kusimama kibiashara.

Vijana jengeni....nyumba ni asset.
 
Kupanga ni kuchagua. Kila mtu acheze mechi zake awezavyo.
Njia za mafanikio ziko nyingi sana, kila mmoja atumie hekima na busara zake kuchagua njia anayoona itamfikisha pale anapotaka kufika.

Mtu uko na familia imepanga chumba na sebule, watoto wanalala sebileni na wewe unajitapa umepanga!

Fikiria umepanga nyumba ya maana kwa ajili ya familia ambayo utatakiwa kulipa 500k hapo bado utilities. Wakati huo kwenye biashara TRA wanakufuatilia kama mwizi.

Kila mtu ashinde mechi zake!
 
Hakuna watu wanapenda kujenga nyumba za kuishi duniani kama watanzania

Ndoto kuu ya kwanza ya mtanzania yeyote ngozi nyeusi ni kuwa na kwake hivyo akipenda vihela huvipeleka site kujenga nyumba ya kuishi hapa ndio siri ya umasikini wa watanzania ngozi nyeusi kuanzia

Wenzetu wahindi hupanga hata miaka arobaini pesa zake akiweka na kukuza biashara yake .wazo lake la kwanza huwa nikipata pesa natafuta nyumba ya bei rahisi ya kupanga halafu hela inayobaki naanzisha biashara. Wote mashahidi wahindi matajiri hasa lakini maisha yote wanaishi nyumba za kupanga za National housing sisi waswahili tunashindana kujenga nyumba za kuishi za kulala na kuamka za mamilioni

Waswahili hatushindani kwenye uwekezaji tunashindana kwenye nani kujenga nyumba kali kuliko mwingine !!! Hata waswahili wakiudhiana wakianza kutukanana isi mojawapo huwa kwani wewe una nini? Mimi Nina kwangu nimejenga nyumba za kuishi moja hapa mjini ingine kijijini

Nchi ziliizoendelea watu huwaza kuwekeza kwanza kama ndoto ya kwanza akipata pesa
Hapa ndio siri ya umaskini wa waswahili ilipo.ndoto zenu za kwanza ni kwenye vitu visivyozalisha pesa hasa nyumba ya kulala na kuamka
Utamu wa pipi ni mate yako.
Kupanga ni kuchagua.
Kila mtu ashinde mechi zake.
 
Ukweli mchungu, ila wachache watakuelewa.Umenikumbusha nilikaa na mangi mmoja sehemu akawa anelezea jinsi watu tunavyoshindwa kufanikisha ndoto zetu kwa kushindwa kuwekeza badala yake tunazika pesa na kuzikalia...
 
Mkuu Tatizo sio tuu kujenga tatizo unajenga nini...
Nikijenga Sasahivi Nitajenga upuuzi tuu.

Hicho kitu SITAKI, nimeandika kwa herufi kubwa kama msisitiozo,
Kuliko kujenga kijumba hakieleweki Miaka hii bora niishie kupanga,

Ila siwezi jenga nyumba kama aliyojenga babu miaka ya 60s, Narudia bora niishie kupanga kuliko kuchafua ardhi.

Masuala unajenga nyumba yako, Unaiongelea mbele ya wenzako baada ya kuita nyumba unaita Kibanda(na kweli unamaanisha) huo upuuzi siwezi.

Nikitaka hicho kibanda eti ilimradi nijiegamize kwangu hata leo naweza na wengi humu naamini wanaweza...
Ila maisha ya leo kuishi kinyonge kuanzia ndani mpk nje hapana.
Najua umri wako ni mdogo na unaongea hivi kwa kuwa hujui kuwa muda ni suala la kutilia sana maanani. Unavyochelewa utakuta uwezi kujenga kabisa kwa kuwa ujenzi unahitaji timing sana.

Mie nilianza kujenga nyumba ya kawaida sana at my early 30 nyumba ya milioni kama 30 hivi na baadae nikajenga nyingine ya kama milioni 40 eneo lilikuwa kubwa 860 square meters. Baada ya hapo nilipokaribia 40 ndio nikaanza kujenga dream house ambayo imenigharimu like 250 million ambayo ndio ninaishi kwa sasa. Baada ya kuona utamu wa kodi niliamua kujenga nyumba ndogo ndogo za kisasa (vyumba viwili na sebule) maeneo mbalimbali jijini ambayo kwangu ni biashara nzuri na rahisi nakusanya kodi kwenye nyumba nyingine najenga mpya mdogo mdogo.

Kwa kukushauri usifikirie sana kujenga nyumba kubwa sana bali jenga ambayo una uwezo nayo ila akikisha iwe nzuri sana kwa ramani madirisha makubwa na isiwe fupi na unapojenga mapema hamia na kama pesa ipo ndipo ufikirie kujenga nyumba kulingana na uwezo wako kipindi hicho. Kwenye ujenzi usijifananishe na mtu. Ujenzi una awamu zake. Waliojenga kipindi cha awamu ya nne simenti elfu 11 ni tofauti na wanaojenga sasa hivi simenti elfu 17 mpk 20. Kwa sasa utateseka zaidi so ni bora ujenge unachokiweza leo.

Nimeshauri kutokana na niliyopitia mie ambayo nahisi ni njia sahihi ukilinganisha na wenzangu wengi wenye kazi na biashara kama zangu ila walikosea tu timing
 
Hakuna watu wanapenda kujenga nyumba za kuishi duniani kama watanzania

Ndoto kuu ya kwanza ya mtanzania yeyote ngozi nyeusi ni kuwa na kwake hivyo akipenda vihela huvipeleka site kujenga nyumba ya kuishi hapa ndio siri ya umasikini wa watanzania ngozi nyeusi kuanzia

Wenzetu wahindi hupanga hata miaka arobaini pesa zake akiweka na kukuza biashara yake .wazo lake la kwanza huwa nikipata pesa natafuta nyumba ya bei rahisi ya kupanga halafu hela inayobaki naanzisha biashara. Wote mashahidi wahindi matajiri hasa lakini maisha yote wanaishi nyumba za kupanga za National housing sisi waswahili tunashindana kujenga nyumba za kuishi za kulala na kuamka za mamilioni

Waswahili hatushindani kwenye uwekezaji tunashindana kwenye nani kujenga nyumba kali kuliko mwingine !!! Hata waswahili wakiudhiana wakianza kutukanana isi mojawapo huwa kwani wewe una nini? Mimi Nina kwangu nimejenga nyumba za kuishi moja hapa mjini ingine kijijini

Nchi ziliizoendelea watu huwaza kuwekeza kwanza kama ndoto ya kwanza akipata pesa
Hapa ndio siri ya umaskini wa waswahili ilipo.ndoto zenu za kwanza ni kwenye vitu visivyozalisha pesa hasa nyumba ya kulala na kuamka
Umeongea Non sense tupu mkuu.

Hapo zamani kabla ya Uhuru,, majumba mengi ya mjini kkoo ,,upanga,,posta,,hata oyesterbay nk yalikuwa ni ya wahindi,,na wageni wengine.
Zikiwemo hata hizo nyumba za NHC za sasa.

Baada ya uhuru serikali ilizitaifisha na kuzimiliki,,baadhi au nyumba zote za wageni .
-Majengo ..
--Shule..
--Majumba ..
-- hata mahospitali.
Sasa hakuna muhindi yeyote anayeiamini serikali ya kiafrica tena ktk suala la ardhi au kujenga nyumba ,,zaidi ya kujenga kwao India.

Muhindi anaishi NHC sababu
--Kodi ni rahisi,,
--karibu na biashara zake.
--karibu na misiikiti yao.
-- karibu na jamaa zao.

Yupo radhi akuhamishe mtu mweusi tena kwa kukununuwa kwa pesa ndefu ili uhame NHC aingie yeye kwenye flat..

Kujenga nyumba ndy ndoto ya kwanza ya kila binadamu mwenye utimamu wa akili..
 
Najua umri wako ni mdogo na unaongea hivi kwa kuwa hujui kuwa muda ni suala la kutilia sana maanani. Unavyochelewa utakuta uwezi kujenga kabisa kwa kuwa ujenzi unahitaji timing sana.

Mie nilianza kujenga nyumba ya kawaida sana at my early 30 nyumba ya milioni kama 30 hivi na baadae nikajenga nyingine ya kama milioni 40 eneo lilikuwa kubwa 860 square meters. Baada ya hapo nilipokaribia 40 ndio nikaanza kujenga dream house ambayo imenigharimu like 250 million ambayo ndio ninaishi kwa sasa. Baada ya kuona utamu wa kodi niliamua kujenga nyumba ndogo ndogo za kisasa (vyumba viwili na sebule) maeneo mbalimbali jijini ambayo kwangu ni biashara nzuri na rahisi nakusanya kodi kwenye nyumba nyingine najenga mpya mdogo mdogo.

Kwa kukushauri usifikirie sana kujenga nyumba kubwa sana bali jenga ambayo una uwezo nayo ila akikisha iwe nzuri sana kwa ramani madirisha makubwa na isiwe fupi na unapojenga mapema hamia na kama pesa ipo ndipo ufikirie kujenga nyumba kulingana na uwezo wako kipindi hicho. Kwenye ujenzi usijifananishe na mtu. Ujenzi una awamu zake. Waliojenga kipindi cha awamu ya nne simenti elfu 11 ni tofauti na wanaojenga sasa hivi simenti elfu 17 mpk 20. Kwa sasa utateseka zaidi so ni bora ujenge unachokiweza leo.

Nimeshauri kutokana na niliyopitia mie ambayo nahisi ni njia sahihi ukilinganisha na wenzangu wengi wenye kazi na biashara kama zangu ila walikosea tu timing
Mkuu Nimekuelewa sana, ila ukweli sasahivi Nikisema nijenge nyumba ya 40mil, kwisha habari yangu, narudia tena kwisha habari yangu..
Namaliza tuu hio nyumba watu wanaanika maturubai, habari zitakazo bakia ni
"Oooooh Marehemu alikua mtu mzuri....." "Ameacha nyumba..." na blah blah nyingi..

BTW kuna hints nimezichukua, asante kwa hilo.
 
Tatizo ni nini mpk ukijenga nyumba ya milioni 40 tuanike maturubai? Je ukijenga ya milioni 200 hawataanika maturubai. Shtuka ndugu yangu time is not on your side. Liwezekanalo leo lisingoje kesho, huu usemi una maana kubwa sana. Wazungu wanasema "make things high when sun shine" ikifika usiku imekula kwako
 
Kingine ni swala la kukopesheka na taasisi za fedha. Biashara haiwezi kusimama bila mikopo, na hakuna mkopo bila dhamana. Siku hizi hawapokei tena eneo lisiloendelezwa kama dhamana ya mkopo. Wanahitaji nyumba. Huna nyumba utatumia muda mwingi sana kusimama kibiashara.

Vijana jengeni....nyumba ni asset.
Wahindi wanaishi nyumba za kupanga na wanaongoxa kwa uwezo wa kukopesheka kwenye mabenki akienda kukopa hachukui hata masaa mawili mkopo unaingia kwenye akaunti yake!!! Wanatumia pesa zilizoko kwenye fixed deposit akaunti zao kama dhamana!!! Huku fixed deposit inaendelea kuingiza faida ya riba wakati huo huo inatumika kama dhamana ya mkopo kule aliochukua imeendelea kuzalisha faida anapata pesa kotekote kwenye fixed na mkopo anaofanyia biashara

Sasa wewe mwenye hilo.jumba lako la kulala na ukiliweka dhamana halingizi hata Mia kipindi chote cha mkopo tofauti na muhindi aliyeona miliki ajenge nyumba heri pesa za hiyo nyumba aziweke kwenye fixed deposit akaunti awe anaitumia kukopea chap chap na pesa kuingia akaunti haraka afanyie biashara

Unajua maana ya Asset ? Asset ni mali inayoingiza pa to A property that generates income is called Asset.Nyumba ya kulala na kuamka sio Asset ni Liability!! Hata liwe la ghorofa

Hiyo nyumba us kulala na kuamka kuiita Asset sio sahihi
 
Kujenga ni muhimu sana hasa kwa hizi familia zetu za kiafrika kwa sababu kusaidiana hakuepukiki.
Mathalani kwa mji kama Mwanza ambao ni kuna huduma kama hospitali kubwa, shangazi yako akipewa rufaa kwenda Bugando cha kwanza anachowaza ni kuwa nina mwanangu Mwanza n.k

Kuna ndugu wengi ambao wameshanikuru kwa sababu niliwasaidia angalau sehemu ya kulala wakati wanashida ya kupata matibabu katika hospitali zetu hizi, kwangu hiyo ni baraka.

Lakini pia kwa sisi wafanyakazi ukisema mshahara wote uwekeze wakati muda wa kusimamia huna, utashangaa watu wanafaidika tuu na uwekezaji wako , wakati wewe unahangaika kupanga na mwisho wa siku hamna cha maana unachopata.
 
Kama kujenga ni umasikini, je, wenye nyumba ni masikini?

Je, ambao hawajajenga ni matajiri?

Maelezo yako hayana logical sequence.

Mfano,

Kujenga ni umasikini

Kupanga ni utajiri

Wenye nyumba ni masikini? Hapana

Wapangaji ni masikini? Hapana

Basi, kuwa tajiri haimaanishi kwamba una nyumba au huna na au unepanga.

Kwa hiyo kuwa na nyumba siyo sababu ya utajiri wala umasikini.

Wapo matajiri wasio na nyumba. Hawa wengi wapo mjini.

Wapo masikini pia wana nyumba. Wengi wa vijijini.

Mtoa mada tafuta tafsiri sahihi ya umasikini.
 
Umeongea Non sense tupu mkuu.

Hapo zamani kabla ya Uhuru,, majumba mengi ya mjini kkoo ,,upanga,,posta,,hata oyesterbay nk yalikuwa ni ya wahindi,,na wageni wengine.
Zikiwemo hata hizo nyumba za NHC za sasa.

Baada ya uhuru serikali ilizitaifisha na kuzimiliki,,baadhi au nyumba zote za wageni .
-Majengo ..
--Shule..
--Majumba ..
-- hata mahospitali.
Sasa hakuna muhindi yeyote anayeiamini serikali ya kiafrica tena ktk suala la ardhi au kujenga nyumba ,,zaidi ya kujenga kwao India.

Muhindi anaishi NHC sababu
--Kodi ni rahisi,,
--karibu na biashara zake.
--karibu na misiikiti yao.
-- karibu na jamaa zao.

Yupo radhi akuhamishe mtu mweusi tena kwa kukununuwa kwa pesa ndefu ili uhame NHC aingie yeye kwenye flat..

Kujenga nyumba ndy ndoto ya kwanza ya kila binadamu mwenye utimamu wa akili..
Umemaliza mkuu, umeongea kama mtu mzima mwenye akili zako timamu haswa.
 
Back
Top Bottom