Hata hao wahindi kwao wana nyumba wamejenga. Huwezi kuwa unaishi say Afrika Kusini ukafikiria kujenga huko. Utapanga na kufanya biashara au shughuli yoyote halali. Hii dhana ndio ipo kwa wahindi, hapa wahindi sio kwao. Kwa baadhi wenye fedha nyingi sana uwa wanajenga maeneo kama masaki, upanga n.k na wengi uwa wananunua apartment.
Halafu kujenga sio umasikini, kumiliki nyumba ni jambo bora sana katika maisha maana nyumba ni kitu ambacho kinakupa mengi sana ikiwepo kukupunguzia gharama za kodi, kukuondolea stress za kutokuwa na kwako na pia hata ukipata tatizo la kiuchumi unakuwa na pa kuanzia.
Nyumba ni kitu ambacho hata ukiondoka duniani ghafla familia yako inakuwa na sehemu ya kuanzia kuliko ukiwa huna nyumba.
Nyumba ni muhimu katika ukuaji wa miji na Taifa kwa ujumla. Unavyoona nje yale majengo ni kwamba watu wamewekeza ndio maana kunapendeza. Na sisi tujenge majengo kukuza nchi yetu. Tuachane na wahindi wale hapa sio kwao ndio maana hawajengi. Tena si wahindi tu hata wazungu hawajengi hapa kwa kuwa si kwao hapa watachuma tu ila kujenga wataenda jenga kwao