Mkuu nipo tofauti na ww kimtazamo kwa hoja zifuatazo.
Kwanza kuna mahitaji muhimu makuu matatu ya mwanadamu:
1.Chakula
2.Mavazi
3.Malazi
Ukiacha mahitaji mawili tajwa hapo juu hilo hitaji la tatu MALAZI ni hitaji muhimu sana kwa mwanadamu yoyote. na tunapoongelea MALAZI hatuongelei KITANDA tunaongelea sehemu ambayo mwanadamu anaweza kujihifadhi katika hali zote na apo tunaongelea NYUMBA.
Usipokua na nyumba ww bado ni MASKINI NA MKIMBIZI USIYE NA MAKAZI MAALUMU NA BADO hujakava mahitaji yako muhimu.
Huna pako na mwenye nyumba anaweza kukufukuza muda wowote anaotaka na kukuaibisha kwa sababu ww ni MKIMBIZI NA HUNA PAKO. Ukiugua, kazi ukafukuzwa, biashara zikayumba ukawa huna hela mfukoni mwenye nyumba atakufukuza kama mbwa koko na kukunyang'anya vyombo vyako mali zako na kubaki maskini zaidi na zaid. Utatanganga tanga bila stahaa na watoto na mke wako.
Kwnye context ya uchumi kuna ASSETS NA LIABILITIES. nakubali kweli nyumba ya kuishi ni Liability lakini kuna kitu Tunakisahau nacho ni WELFARE.
WELFARE ni hadhi ya maisha ambacho ni kitu muhimu sana kwenye maisha.
Kama umepanga ww hadhi yako ya maisha still ipo poor.
Mf: Kuna sehemu nilipanga mwenye nyumba hataki wageni waje kwangu eti choo kinajaa. Daah niliumia sana na nikahama ndo maana napambana usiku na mchana nimalizie site yangu nihamie. Sipendi fedheha za nama hii.
Kua kwako kuna raha sana acha tuu..
WATANZANIA TUJENGE NYUMBA BORA KWA MAENDELEO YETU, NYUMBA NI MAISHA JAMANI. HATA MAISHA YAKITETELEKA NYUMBA ITAKUSITIRI SANA. UNAKULA ZAKO MCHICHA UNALALA. LAKIN KOSA KODI UTAJUA NINACHOKIONGEA HAPA KAMA CHA MAANA AU CHA KIPUUZI.