Umasikini wetu umesababishwa na wingi wa Rasilimali tulizonazo?

Umasikini wetu umesababishwa na wingi wa Rasilimali tulizonazo?

Pslmp

JF-Expert Member
Joined
Mar 18, 2021
Posts
1,622
Reaction score
2,458
Mimi najiuliza tu,

Nchi yangu Tanzania, inakila aina ya rasilimali ya utakachotaka, Inazo rasilimali za kila aina, ajabu hakuna chochote tunajivunia licha ya kuwepo Rasilimali nyiiingi kiasi kwamba nyingine hazijawahi kuguswa tangu dunia iumbwe..!

Najuiliza pia, Ni kwa nini Mungu alitupa Hizi Rasilimali nyingi kiasi hiki..! Kwa nini asingetupa nchi kama ya waisrael isiyokuwa na chochote? alitupa rasilimali hizi ili tunyanyasanee au! Au yeye hakuona kuwa kutakuwepo wachache tu, ambao hizi Rasilimali zitakuwa ni mali zao na vizazi vyao tu huku wengine wakiendelea kuishi kwa dhiki na mateso makubwa?

Natanani nchi yetu tusingepewa hizi Rasilimali, tungepewa nchi kama waliyopewa Israel isiyokuwa na chochote, labda hapo viongozi wetu wangekuwa wepesi wa wa kukubali kushauriwa hasa kwenye maswala ya uwekezaji,

Tuna ndege zisizokuwa na maana hata kidogo, ingawa mtazamo ni mzuri, na sasa tunataka kujenga bandari nzuuri na kuuubwa ili iziuwe zilizopo, na cha ajabu, zinazokufa ndio za kwetu 100% na mahali inapojengwa, ni jirani tu na bandari yetu iliyopo Posta jijini Dar es Salaam. Ni wakati wa kuanza kutumia zaidi ufahamu ambao Mungu ametupatia

Wakati mataifa mengi yakijivunia viongozi wao kuwaletea wananchi wake maendeleo makubwa, na kufanya mapinduzi makubwa ya kiuchumi, sisi tunajivunia kuwa na viongozi wenye kuwakomoa wale waliotangulia kushika madaraka kabla yao na matokeo yake tukapata ndege nyiiingi zisizo na faida kwetu, ingwa ni ukweli pia, kuna mengi mazuri yenye tija yaliyoanzishwa na serikali hiyo, tunayo ya kujivunia.

Mungu Ibariki Nchi yetu na viongozi wetu.
 
Israel bila Rasilimali wametokaje?

Huwenda ni kwa sababu ya kuwa na Rasilimali nyingi hatuumizi vivya kuhusu kesho, tupotupo tu kama taifa, Viongozi wetu wanajilimbikia mali na hakuna anayajaribu kuuliza ni kwa nini

Badala yake kila mtu anatamani awe kiongozi ili naye akaibe, na wananchi tunasifia tu, na saa nyingine tunabishana kusema, Eti acha naye afanye hivyo, mbona yule aliganya hivyo?

Hii ni kuonesha jinsi uwingi wa Rasilimali zetu zilivyotupumbaza kiakili, kwa kuwa tunaamini eti hazitaisha

Najiuliza, kama tungelikuwa na Rasilima aina moja tu au mbili, Tungelikuwa tunawaacha tu kweli hawa wezi wa Rasilimali zetu?

Kungelikuwa na mtu au kiongozi wa kujilimbikizia mali tukamwacha tu kweli?

yaani utakuta utajiri ambao viongozi wengi wa kiafrika wanamiliki, ungeweza kumilikiwa na zaidi ya watu m. 1+, lakini anao mtu mmoja na familia yake tu, huku raia wakiishi kwa Bora ya jana!

watu wanalaana!!
 
Swala la kuwa na rasilimali nyingi, ni kama limetuchelewesha kuendele kwa kweli

mf,

Mtoto wa tajiri na mtoto wa masikini wakiwa na elimu zao sawa,

wakiambiwa wakajitegemee na waondoke majumbani kwao bila chochote, ni nani atatoboza maisha kwa haraka?
 
Back
Top Bottom