Umaskini na ufukara ni hatari kuliko ushoga na usagaji. Tuanze na vita ya umaskini na ufukara kisha tukatae ushoga

Umaskini na ufukara ni hatari kuliko ushoga na usagaji. Tuanze na vita ya umaskini na ufukara kisha tukatae ushoga

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Binafsi naona umaskini na ufukara mkubwa ndani ya Tanzania ndio viwe adui nambari moja kabla hatujahamishia magoli kwenye issue ya ushoga na usagaji.

Leo hii mtu analala kwenye nyumba ya nyasi na udongo pamoja na kuku ndani lakini watu hawaoni ajabu kwasababu umaskini na ufukara umerasimishwa katika nchi hii.

Leo hii kuna wanafunzi wa msingi wanakwenda shule na yeboyebo mbovu na wengine miguu ya bata kabisa.

Binafsi naumia sana kuuona ufukara namna hiyo. Leo hii kuna nyumba zinafungwa kwa milango ya mabua lakini watu hawapigi kelele.

Hata mashoga wengine ni impact ya ufukara tu. Ushoga mbaya ila umaskini na ufukara ni mbaya zaidi.

mgogo 1.jpg
 
Tatizo la waafrika ni kudakia mambo tu!!ila ni "kama hujui uendako huwezi kupotea" hili suala la ushoga walivyolivalia njuga utadhani ndio tatizo kubwa kwetu kuliko hata huu umasikini tulionao!!!jamaa wana jutafunia nchi lakini huoni kelele ila eti ushoga!!
 
Mkuu jichunguze sana. Huwezi kulalamikia kulala kwenye nyumba ya nyasi wakati kila mtanzania chimbuko lake ni huko. Pia sidhani kama post yako umetumia akilo kulinganisha ushoga na usagaji na umasikini wa kulala kwenye nyumba ya nyasi na kufungia mabua mlangoni wakati hiyo ndo asili yetu. Kwani lini Watanzania wote wamewahi kumiliki magorofa then wakapoteza vyote na kulala kwenye nyasi?

Ivi ulishawahi kufikilia nn maana ya kupoteza utu? Ivi ukijua kuwa either mtoto wako, mshua wako, kaka, mdogo wako, or ndugu yako yeyote anapigwa nyuma unaweza kulichukuliaje? Ebu tulizeni akili kwanza kabla ya kupost vitu kama hivi. Vinginevyo watu watakuchukulia kuwa na wew ndo wale wale.....
 
Mkuu jichunguze sana. Huwezi kulalamikia kulala kwenye nyumba ya nyasi wakati kila mtanzania chimbuko lake ni huko. Pia sidhani kama post yako umetumia akilo kulinganisha ushoga na usagaji na umasikini wa kulala kwenye nyumba ya nyasi na kufungia mabua mlangoni wakati hiyo ndo asili yetu. Kwani lini Watanzania wote wamewahi kumiliki magorofa then wakapoteza vyote na kulala kwenye nyasi...??. Ivi ulishawahi kufikilia nn maana ya kupoteza utu..??. Ivi ukijua kuwa either mtoto wako, mshua wako, kaka, mdogo wako, or ndugu yako yeyote anapigwa nyuma unaweza kulichukuliaje....??. Ebu tulizeni akili kwanza kabla ya kupost vitu kama hivi. Vinginevyo watu watakuchukulia kuwa na wew ndo wale wale.....
Hawa jamaa unawaona hapa wakipeana malike ni wanyanyasaji na wengi wao sio watu wa hapa Tanzania. Hakuna mtu anyejielewa anaweza kuanza kujidhihaki. Hakuna.

Ni mtandao mahususi wa kigaidi na ulio na azma ya kuchafua Mtanzania, Mwaafrika na Hususani mtu Mweusi.
Wakemewe popote humu jamvini
 
Uwe na hela halafu litoto lako lisenge
Hapo ndio maji utaita manjota
Binafsi naona umaskini na ufukara mkubwa ndani ya Tanzania ndio viwe adui nambari moja kabla hatujahamishia magoli kwenye issue ya ushoga na usagaji.
Leo hii mtu analala kwenye nyumba ya nyasi na udongo pamoja na kuku ndani lakini watu hawaoni ajabu kwasababu umaskini na ufukara umerasimishwa katika nchi hii.
Leo hii kuna wanafunzi wa msingi wanakwenda shule na yeboyebo mbovu na wengine miguu ya bata kabisa.
Binafsi naumia sana kuuona ufukara namna hiyo.
Leo hii kuna nyumba zinafungwa kwa milango ya mabua lakini watu hawapigi kelele.
Hata mashoga wengine ni impact ya ufukara tu.
Ushoga mbaya ila umaskini na ufukara ni mbaya zaidi.View attachment 2574244
 
Heri kuwa maskini ukiwa umelinda utu wako. Heri mtoto wako atembee peku km1 kwenda shule akirûdi akachanje kuni porini, jioni ale viazi na mtindi alake, kuliko kupanda school bus, akiwa shoga. TUANZE NA VITA YA USHOGA, umaskini baadaye
 
Ushoga na usagaji unaiangamiza dunia , binadamu anatoweka kwa kuwa hakuna kuzaana; halafu unaulinganisha na umaskini!
May be uko sawa kwa kuwa binadamu wakiisha hakutakuwepo maskini.
 
Kama taifa haya ndiyo masuala yenye tija kujadili, hayo ya ushoga na usagaji ni aibu na fedheha kujadili
Huwa naona aibu Sana uongelea ushoga sijui naanzaje Yani!!!Huwa nashangaa nakosa jibu!! Mwanaume unamtamanije mwanaume!??unaanzaje!?
 
Kama taifa haya ndiyo masuala yenye tija kujadili, hayo ya ushoga na usagaji ni aibu na fedheha kujadili
90%ya watanzania hawana uwezo wa kujadili hoja zenye manufaa kwao!!.
Pitia hata humu jamii forum uone mada zipi zana wachangiaji wengi!!
 
Back
Top Bottom