Umati wajitokeza kutia nia kwenye Ubunge na Udiwani kupitia CHADEMA, nafasi zimejaa kabisa

Umati wajitokeza kutia nia kwenye Ubunge na Udiwani kupitia CHADEMA, nafasi zimejaa kabisa

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Hii ni Taarifa kutoka kwa John Mrema ambaye ni mkurugenzi wa Itifaki wa Chadema, Ikumbukwe kwamba Chadema iliweka utaratibu kwa wanachama wake wote wanaotaka kugombea nafasi hizi kujitokeza mapema kutia nia kwenye chama chao ili usaili ( Vetting ) juu yao uanze mapema, lengo likiwa ni kutoa nafasi kwa viongozi kuwafahamu kiundani Wagombea hawa kabla ya kuwapa nafasi za kugombea.

Nafasi zote za ubunge na udiwani kwenye majimbo na kata zote nchi nzima, hakuna mtia nia ambaye yuko peke yake, yako majimbo ambayo kuna watia nia ya ubunge kuanzia watatu hadi watano!

Kwa aina ya siasa za Tanzania za sasa Umati huu wa watia nia wa Chadema una maana gani?

# TUENDELEE KUNAWA MIKONO ILI KUJIKINGA NA VIRUSI VYA CORONA .
 
Msikosee tu mkabeba tena zile taka ngumu toka ccm za dakika ya majeruhi. Hiyo ni hatua namba moja, lakini hatua kubwa kabisa ni kudai tume huru ya uchaguzi, maana bila hiyo ni kupoteza muda na fedha.
 
Kitu kama Stimulus Package ili kuzisaidia Biashara na Viwanda vinavyoathiriwa na pandemic hii ya corona

Au Catarist haielewi hiiiii bhagosha
Niambie viwanda au biashara ngapi vimeathiriwa na hii so called pandemic?

Mbona mnapenda kukuza mambo? Maana huko USA kwenye cases nyingi sijasikia wakitangaza stimulus package. Nahisi utakuwa mpigaji unatafuta pesa za bure kwa kisingizio cha Corona, kumbuka JK alitoa stimulus package kipindi chake, zilinufaisha mini?
 
Lazaro Nyalandu anafanya kazi nzuri sana, juzi nilikuwa Kindai karibia mkoa wote wa Singida ni Chadema tu, muda huu ninaoandika... No hate No fear

DPAw_34XUAYIq3u-1.jpg
 
Back
Top Bottom