Umati wajitokeza kutia nia kwenye Ubunge na Udiwani kupitia CHADEMA, nafasi zimejaa kabisa

Umati wajitokeza kutia nia kwenye Ubunge na Udiwani kupitia CHADEMA, nafasi zimejaa kabisa

Lazaro Nyalandu anafanya kazi nzuri sana, juzi nilikuwa Kindai karibia mkoa wote wa Singida ni Chadema tu, muda huu ninaoandika... No hate No fear

View attachment 1415752
Mkuu 'imhotep',

Samahani sana mkuu wangu, kwa sababu inachanganya sana namna hii.

Huyu ni Nyalandu, anafanya mkutano wa hadhara? Lini, na wapi?

Haya maswali ukiyajibu kwa ukweli, nitaelewa, lakini ndio akili yangu itaongezeka kuchanganyikiwa juu ya hili.
Hilo ni moja.

Pili.
Hivi huko CHADEMA yupo Nyalandu peke yake, Tanzania nzima; na wala siyo mbunge basi!

Hawa wengine wote wapo wapi?

Tunawajua wanaoshinda mahakamani na magerezani kiasi kwamba hawana nafasi kama aliyonayo Nyalandu. Hawa wengine wooote wako wapi?

Tusipeane sababu na visingizio za ushabiki wa chama. Tuelezeni tu kiuhakika kwa nini awe Nyalandu pekee ndiye aonekane kuwa imara. Akina Wenje wapo wapi? Na wengi wengine waliowahi kuwa viongozi ndani ya chama. Mbona hawaskiki.

Au wanasubiri uteuzi ndio waanze kazi ya kukijenga chama?

Ndio maana nikamwandikia rafiki yangu Erythro hapo juu, kwamba wakati wa mchujo, msikose kutafuta msaada wa mawazo ya watu. Mnao ma'opportunists' wengi sana ndani ya CHADEMA
 
Weka ushahidi hapa
Mkuu 'misasa'

Siku hizi umekuwa jasiri kweli na michango yako hii; umepandishwa cheo?

Baada ya kusema hayo ngoja nikupe ushauri mzuri tu, tena bila ya hiana yoyote, kwa sababu naelewa wewe ni mtu 'reasonable'; labda uwe umeharibiwa na kupandishwa cheo, lakini historia yako humu ndani ya JF sio mbaya.

Ushauri ni huu: Jitahidi kusoma habari toka vyanzo mbalimbali, hasa vya nje. Usitegemee hivi vya ndani ya nchi pekee ambavyo sasa hivi vinaimba habari moja tu!

Uliyoandika hapa kuhusu hiyo unayoiita 'package' inaonyesha dhahiri kwamba wewe dunia yako inaishia hapoahapa Kariakoo tu basi!

Yaani hata hapa kwa jirani zetu Kenya huna habari nao kuhusu vitu kama hivyo?

Sikuzodoi, nakupa tu ukweli wenyewe ulivyo, kwa sababu najua wewe ni mTanzania safi anayekosa taarifa mhimu kumwezesha kuchambua mambo kwa utashi na sio kwa ushabiki.
 
Erythrocyte,
Tatizo ni kwamba mnapenda kuanika mambo mapema mapema matokeo yake mwisho wa siku mnaingiziwa mamluki. Kwa taarifa kama hizi zinawaumiza vichwa kwa upande ule wa pili, nao hawatoweza kulala bila kupanga mikakati ya kuharibu.
 
Msikosee tu mkabeba tena zile taka ngumu toka ccm za dakika ya majeruhi. Hiyo ni hatua namba moja, lakini hatua kubwa kabisa ni kudai tume huru ya uchaguzi, maana bila hiyo ni kupoteza muda na fedha.
Mwenuekiti wa chadema sio mtu wa kuaminika au hajitambui. Utashangaa linakuja jitu na timu yake toka ccm na kupewa nafasi "muhimu" na wafuasi wake kupewa nafasi za upendeleo dhidi ya makada wenyeji waliowahi nafasi hizo.
 
Kalamu1,
Mkuu

Kutoka kupigia debe tufanye lockdown/curfew,sasa mmekuja na wimbo mpya mnahitaji stimulus package.

Stimulus package siwezi kukataa lakini ni mapema mno kujua tathmini za athari wa Corona katika biashara au viwanda.

Serikali sikivu ikifikia huko italetwa hiyo stimulus package mjichotee mapesa, si ndio mnavyotaka?

Mwisho mkuu Kalamu1 furaha yako rais akiwa lissu au Mbowe nahisi utaruka na kugalagala, sijawahi kuona unachangia mazuri ya serikali ya awamu ya tano,ina maana hii serikali inafanya mabaya tu?
 
Erythrocyte, Mkuu watia nia wa CHADEMA kwa mujibu wa taatifa yako waliyo wengi mwisho ni watatu lakini kwa CCM kwa uchache kwa jimbo au kata moja huwa si chini ya watia nia kumi. Hapo inakiwaje kwa wingi wa watia nia ndiyo ushindi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Erythrocyte,
Ukipanga ujue kuna anayepanga juu ya uliyopanga. Be careful with the so called "unknowns" might be the mojority of your nominees!
 
Mwenuekiti wa chadema sio mtu wa kuaminika au hajitambui. Utashangaa linakuja jitu na timu yake toka ccm na kupewa nafasi "muhimu" na wafuasi wake kupewa nafasi za upendeleo dhidi ya makada wenyeji waliowahi nafasi hizo.

Safari hii hana bahati.
 
Back
Top Bottom