Miaka 40 ya Waisrael kutoka Misri kwenda Kanaani waiona mingi mno kiasi cha kuwa na mashaka. Ukimwasi MUNGU na kuigiza kama vile unamtumikia na yeye amekuchagua lazima akurudi kama baba amrudivyo mwanawe anayempenda. Nitakupa mfano rahisi wa kibinadamu unaoujua au waweza kuutafuta na kuupata. Miaka Tanganyika iliyojitawala (pamoja na muda wa muungano) ni miaka 53 sasa. Huu ni muda mrefu kuliko safari ya wana wa Israel na vikwazo vyake. Pima kiwango cha maendeleo na mafanikio yetu. Kufikia mwaka 1971 tulifanya makubwa mno ambayo tumeibomoa na sasa tunaanza upya. Tuliweza kutengeneza nguo zetu,viberiti vyetu,viatu vyetu. Tukaviharibu.Tunashangaa hakuna ajira. Tunatamani kuvifufua wengine wanaona bora Mwingereza arid I( kama Waisrael walivyokumbuka nyama Misri)
Ni kanuni ya MUNGU Taifa lisipomtii litazunguka tu. Walipoisha kizazi cha kuasi kwa kuabudu Ndama na kujitukuza fahamu zikafunguliwa. Joshua akakiongoza kizazi kipya kuingia kanaani.
Afu hili tatizo nilidhani ni mimi tu naliona ! Yaani unaweza safiri toka Mtwara hadi Mwanza usione serious production activity afu viongozi wetu wanafunga tai tu ! Sijui wamepigwa na pepo . Yaani hamna hata kiwanda kimoja njiani duh!