Umbali kati ya Misri na Israel ni KM 613, lakini wana wa Israel walisafiri kwa miaka 40

Walipitishwa njia ya mbali yenye mzunguko mkubwa

lakini pia walikuwa wanaweka matuo na kukaa mahala kwa muda.
 
Tatizo hii safar watu wanaichukulia kiroho sana ndo mana baadh hufikri kuwa ni hadith ya kufikirika..kuna wakat walikuwa wanakaa siku kadhaa bila safar..mfano wakat Mussa anapewa taratibu za kijamii na sheria mbal mbal ilihtajika mda wa kuziwasilisha kwa kusanyiko lote takriban watu million mbil au tatu hv..na ilichukua miezi kadhaa...mtu mkubwa akifarki walikuwa wanaomboleza siku takriban 40... Safar ilikuwa ya taratbu sana kutokana na kusanyiko kuwa na kila aina ya watu hasa watoto wadogo, wajawazito, wanyonyeshao na mifugo....ukiachana na hayo miaka 40 ilikuwa adhabu ya Mungu kwao...!! Na ndo mana kuna wakat uvumilivu ulikuwa unawashinda..jua kali, shida ya maji na njia zisizoeleweka..somtme walikuwa wanalianzisha la vurugu...kusolve changamoto kama hv kulisababisha hapa na pale kusitisha safr...ni kama leo Yesu alisema atarud mda si mrefu but response mbovu ya watu inamfanya achelewe huku mamilion ya watu wakiendelea kuzikwa ardhin
 
ahaa haah ahaa! Mkuu lyinga umenichekesha sana. We unadhani walikuwa wanafanya nini miaka yote hiyo njiani. Eti kama kulikuwa na mama mjamzito, then akajifungua alikuwa na uwezekano wa kupata mjukuu akiwa safarini .emegine!
[emoji2] [emoji2] miaka 40 ya kale usikute hata wiki ya sasa haifiki
 
Misri ya Leo sio Misri ya enzi za Musa, pia haimaanishi kuwa walikuwa wakisafiri kwa miaka yote hiyo, Kuna process kuweza kuachiliwa kutoka mtumwa hadi kwa huru


Ndugu hongera kwa kufikiria jambo hilo,

Safari ya wana wa israel toka misri kwenda nchi ya ahadi lazima ujue ilikuwa imepagwa na Mungu pia ilijaa majaribu mengi sana kumbuka hata musa alivyopanda mlima sinai ilimchukua zaidi ya mwaka kushuka mapaka akawakuta wana wa israel wanaabudu sanamu ya ndama wa dhahabu.

Mungu aliwapa adhabu nyingi pia safari yao hawakuachana nyuma kulikuwa na watu wengi wagonjwa,wazee,walemavu watoto nk.

Angalia sana pale mkji wa kadeshi walirudi marambili.

Hesabu 33
1 Hizi ndizo safari za wana wa Israeli, hapo walipotoka nchi ya Misri kwa jeshi zao chini ya mkono wa Musa na Haruni.

2 Musa akaandika jinsi walivyotoka katika safari zao, kwa amri ya Bwana; na hizi ndizo safari zao kama kutoka kwao kulivyokuwa.

3 Wakasafiri kutoka Ramesesi mwezi wa kwanza, siku ya kumi na tano ya mwezi wa kwanza; siku ya pili baada ya Pasaka, wana wa Israeli wakatoka kwa mkono wa nguvu mbele ya macho ya Wamisri wote,

4 hapo Wamisri walipokuwa wanazika wazaliwa wa kwanza wao wote, Bwana aliokuwa amewapiga kati yao; Bwana akafanya hukumu juu ya miungu yao nayo.

5 Wana wa Israeli wakasafiri kutoka Ramesesi, wakapanga katika Sukothi.

6 Kisha wakasafiri kutoka Sukothi, wakapanga Ethamu, palipo katika mwisho wa nyika.

7 Wakasafiri kutoka Ethamu, na kurudi nyuma hata Pi-hahirothi palipokabili Baal-sefoni; wakapanga mbele ya Migdoli.

8 Wakasafiri kutoka hapo mbele ya Hahirothi, wakapita katikati ya bahari na kuingia jangwani; kisha wakaenda safari ya siku tatu katika nyika ya Ethamu, wakapanga Mara.

9 Wakasafiri kutoka Mara, wakafikilia Elimu; huko Elimu palikuwa na chemchemi za maji kumi na mbili, na mitende sabini; nao wakapanga hapo.

10 Wakasafiri kutoka Elimu wakapanga karibu na Bahari ya Shamu.

11 Wakasafiri kutoka Bahari ya Shamu, wakapanga katika nyika ya Sini.

12 Wakasafiri kutoka nyika ya Sini, wakapanga Dofka.

13 Wakasafiri kutoka Dofka, wakapanga Alushi.

14 Wakasafiri kutoka Alushi, wakapanga Refidimu, ambapo hapakuwa na maji ya watu kunywa.

15 Wakasafiri kutoka Refidimu, wakapanga katika nyika ya Sinai.

16 Wakasafiri kutoka nyika ya Sinai, wakapanga Kibroth-hataava.

17 Wakasafiri kutoka Kibroth-hataava, wakapanga Haserothi.

18 Wakasafiri kutoka Haserothi, wakapanga Rithma.

19 Wakasafiri kutoka Rithma, wakapanga Rimon-peresi.

20 Wakasafiri kutoka Rimon-peresi, wakapanga Libna.

21 Wakasafiri kutoka Libna, wakapanga Risa.

22 Wakasafiri kutoka Risa, wakapanga Keheletha.

23 Wakasafiri kutoka Keheletha, wakapanga katika mlima wa Sheferi

24 Wakasafiri kutoka huo mlima wa Sheferi, wakapanga Harada.

25 Wakasafiri kutoka Harada, wakapanga Makelothi.

26 Wakasafiri kutoka Makelothi, wakapanga Tahathi.

27 Wakasafiri kutoka Tahathi wakapanga Tera.

28 Wakasafiri kutoka Tera, wakapanga Mithka.

29 Wakasafiri kutoka Mithka, wakapanga Hashmona.

30 Wakasafiri kutoka Hashmona, wakapanga Moserothi.

31 Wakasafiri kutoka Moserothi, wakapanga Bene-yakani.

32 Wakasafiri kutoka Bene-yakani, wakapanga Hor-hagidgadi.

33 Wakasafiri kutoka Hor-hagidgadi, wakapanga Yotbatha.

34 Wakasafiri kutoka Yotbatha, wakapanga Abrona.

35 Wakasafiri kutoka Abrona, wakapanga Esion-geberi.

36 Wakasafiri kutoka Esion-geberi, wakapanga katika nyika ya Sini (ni Kadeshi).

37 Wakasafiri kutoka Kadeshi wakapanga katika mlima wa Hori, katika mpaka wa nchi ya Edomu,

38 Haruni akakwea mlima wa Hori, kwa amri ya Bwana, akafa hapo, katika mwaka wa arobaini baada ya wana wa Israeli kutoka katika nchi ya Misri, mwezi wa tano, siku ya kwanza ya mwezi.

39 Naye Haruni alikuwa mtu wa umri wa miaka mia na ishirini na mitatu hapo alipokufa katika mlima wa Hori.

40 Ndipo Mkanaani, mfalme wa Aradi, aliyekaa pande za Negebu katika nchi ya Kanaani akasikia habari za kuja kwao wana wa Israeli.

41 Nao wakasafiri kutoka mlima wa Hori, wakapanga Salmona.

42 Wakasafiri kutoka Salmona, wakapanga Punoni.

43 Wakasafiri kutoka Punoni, wakapanga Obothi.

44 Wakasafiri kutoka Obothi, wakapanga Iye-abarimu, katika mpaka wa Moabu.

45 Wakasafiri kutoka Iye-abarimu, wakapanga Dibon-gadi.

46 Wakasafiri kutoka Dibon-gadi, wakapanga Almon-diblathaimu.

47 Wakasafiri kutoka Almon-diblathaimu, wakapanga katika milima ya Abarimu, kukabili Nebo.

48 Wakasafiri kutoka hiyo milima ya Abarimu, wakapanga katika nchi tambarare za Moabu, karibu na mto wa Yordani, hapo Yeriko.

49 Wakapanga karibu na Yordani, tangu Beth-yeshimothi hata kufikilia Abel-shitimu katika nchi tambarare za Moabu.

50 Kisha Bwana akanena na Musa hapo katika nchi tambarare za Moabu, karibu na Yordani, hapo Yeriko, na kumwambia,

51 Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Mtakapovuka mto wa Yordani na kuingia nchi ya Kanaani,

52 ndipo mtakapowafukuza wenyeji wote wa hiyo nchi mbele yenu, nanyi mtayaharibu mawe yao yote yenye kuchorwa sanamu, na kuziharibu sanamu zao zote za kusubu, kuvunja-vunja mahali pao pote palipoinuka;

53 nanyi mtaishika hiyo nchi kuimiliki na kuketi humo; kwa kuwa mimi nimewapa ninyi hiyo nchi ili mwimiliki.

54 Nanyi mtairithi nchi kwa kufanya kura, kama jamaa zenu zilivyo; hao walio wengi mtawapa urithi zaidi, na hao waliopunguka utawapa kama kupunguka kwao; mahali po pote kura itakapomwangukia mtu ye yote, mahali hapo ni pake; mtarithi kama kabila za baba zenu zilivyo.

55 Lakini kama hamtaki kuwafukuza wenyeji wa nchi watoke mbele yenu; ndipo hao ambao mtakaowasaza watakuwa kama sindano machoni mwenu, na kama miiba ubavuni mwenu, nao watawasumbua katika hiyo nchi ambayo mwakaa.

56 Kisha itakuwa, kama nilivyoazimia kuwatenda wao, ndivyo nitakavyowatenda ninyi.

KARIBU
 
Ikumbukwe hawa waisraeli walikuwa utumwani miaka laki nne hivyo walikuwa hawajui lolote kuhusu Mungu na matakwa yake. Walikuwa wapagani full. Na wakati wanaondoka walikuwa wanasema wanaenda kumwabudu Mungu wao jangwani maanake wanaenda kufundishwa taratibu za Mungu. Bahati mbaya nao wanavichwa ngumu hivo iligarimu muda zaidi na zaidi.
 
duuuhh hapa umenimaliza kabisa...sina swali ""
 
hizo huwa ni hadithi tu kama za akina bulicheka.
Wewe vita gani ya mapanga inauwa watu 500,000 kwa siku.wakati kule hiroshima ilipigwa atomic hawajafika hata laki 2
hahaa.nimecheka...hapo bado hujapiga hesabu za population ya watu waliokuwa wanapatikana katika miji hiyo"" waweza kuta hata ml.2 walikuwa hawafiki""
 
Acha upumbavu wa kuingiza mambo hayo kwenye suala kama hili..
 
haha haaaa
 
 
hahaaa...
 
[QUOTE="Ziroseventytwo,

Wachungaji naomba msaada wa ufunuo hapa hapa.... [/QUOTE]
Biblia yenyewe inajibu sehemu ya swali ama swali zima. Kutoka 13:1- 18

17 Ilikuwa hapo Farao alipokwisha kuwaacha watu hao waende zao, Mungu hakuwaongoza kwa njia ya nchi ya Wafilisti, ijapokuwa ilikuwa ni ya karibu; maana Mungu alisema, Wasije wakaghairi watu hawa hapo watakapokutana na vita, na kurudi Misri;
18 lakini Mungu akawazungusha hao watu kwa njia ya bara kando ya Bahari ya Shamu; wana wa Israeli wakakwea kutoka nchi ya Misri hali wamevaa silaha.
 
hahaaa...daaahh Jamaa unatoa fact ..tatizo hawawezi kukuelewa ukishakuwa brain wash niutumwa kwisha kazi""
 
Aiseee bado kuna mtu atapinga na hoja kama hii"""
 
kweli ujinga hatutaki aisee...kuongopeana kama Watoto wadogo ndio nini
 
Kwa mujibu wa uislamu mtume mussa baada ya kukamilisha siku 40 na kwenda kuchukua kitabu alivyorudi aliwakuta wana wa Israel wakiabudia ngombe

Mungu akawapa adhabu ya kutanga tanga jangwani na kusafiri kwa muda wa miaka 40
uwongo "" huyo mungu atakuwa hajielewi ...kwasababu inaonyesha lengo lake kuu la kuwatoa waisrael chini ya utawala wa misri nikwasbabu walikuwa wanaonewa wanafanywa kama watumwa ..haiyumkiniki Mungu huyo huyo aliyeamua kuwakomboa watu kwa lengo lakuwatoa katika mateso na kwenda kujitawala"" eti aamue kuwageuka watu hao hao aliotaka kuwakomboa na kuanza kuwatesa kiasi hicho...sasa hapo sibora wangebaki kule kule misri tu"" natunaamini kuwa mungu nimjuzi. yote ..kwann asingetumia ujuzi wake wa yote kujua mambo yatakayokuja kuwa Hawa watu hata akikomboa hawatokuja kumsikiliza "" maana kama angeamua kutumia ujuzi wake huo asingehangaika kuwakomboa watu ambao baadae wamekuja kuonyesha kuwa hawana muda wakumuamini "" huoni kuwa ingeasidia mnoo kutuutumia muda wake vibaya..nakuwza kufnya mambo mengine yenye tija zaidi haswaa kwa wale ambao waliokuwa wanamuamini ktik wakati huo.......

lazima tukubali kuwa hivi vitabu vya dini vinauowongo mwingi sana....wametunywesha sana chai
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…