Umbali kati ya Misri na Israel ni KM 613, lakini wana wa Israel walisafiri kwa miaka 40

Umbali kati ya Misri na Israel ni KM 613, lakini wana wa Israel walisafiri kwa miaka 40

Umbali kutoka misri hadi israel ni hatua chache tu,kwani hizo nchi zinapakana ,kwahiyo hamna umbali wowote.
Pia kipindi hicho eneo lote lilikuwa chini ya miliki ya wamisri,means story ya akina moses ni hekaya,it never happened
 
Majibu ni mengi
(1) kama wangekwenda moja kwa moja wangepoteza maisha hawakujua vita hata silaha hawakuzijua kumbuka israel ilikuwa na mataifa mengine ndani wasingekaribishwa pasipo kushinda vita
(2) Mungu aliwafundisha kumtegemea kwa kila jambo hawakujua kulima hata chakula kilitoka mbinguni
(3)kumbuka walikuwa zaidi ya watu laki moja sasa kuna waliokuwa wanazaa njiani hivyo wanaweka kambi,hivyo hivyo kwa mifugo yao
(4)hata njia iliwapasa kusubiri wingu na nguzo ya moto iwaongoze wakikorofishana na Mungu watakaa hapo mpaka wapatane nae.hawakujua njia ya kufika huko
Sawa ila c kwa miaka 40
 
biblia ni maandko ya kifalsafa,ukitumia akili za kibashite unaweza kusema ilikuwa safari kweli ya kwenda kwa miguu,kumbe lahasha.Ni sawa na kuzani Eva ndo mzambi sana kwa kula tunda la katkati pale Eden,thubutu tunda la kati kati ni fumbo la kifalsafa,ukianza kudadavua unaweza kuandika hata page kadhaa kuelezea akina bashite wakuelewe...
Wewe umeongea
 
Hii hadithi ya miaka 40 umeitoa wapi? Kama ni kwenye biblia basi hicho ni kitabu cha
Riwaya kama vile vya shigongo
Na kile kitabu kingine kilichoandika ni cha udakuu
 
Tunapaswa kufahamu kuwa wakati wanasafiri kuna mambo kadhaa yalikuwa yakitokea.
1. Hakuna aliyekuwa akijua nchi ya ahadi hasa ni wapi hivyo walikuwa na vituo vingi sana njiani.... ikumbukwe hawakupitishwa nchi ya Wafilisti ili wasije wakaogopa vita na kurudi Misri.
2. Wakati wanaondoka Misri waliondoka na watu wao wote... Hapa inajumuisha wazee, watoto na wagonjwa. Ukiwa na watu laki 6 halafu ukawa na wazee elfu 50 nadhani unaweza kukadiria mwendo wao ulivyokuwa.
3. Walikuwa wakihitaji kutafuta chakula cha kuwalisha watu laki 6 kila wakati.
4. Walikuwa wanalazimika kutuma watu kufanya upelelezi kwa siku kadhaa kabla hawajaingia kwenye mji. Kama nilivyosema aali hawakujua nchi ya ahadi hivyo ilikuwa wanapovamia sehemu wanakaa hapo muda mrefu kabla ya kupokea maelekezo mengine.
5. Kumbuka walikuwa wanapita jangwani kwenye changamoto kibao.
6. Baada ya kuasi na kuabudu ndama wa dhahabu walipewa adhabu ya kutanga tanga jangwani mpaka kizazi kile kilipotoweka wakiwemo Musa na Haruni.
7. Biblia haiexploit kila kitu....

8. Hivi unajua wamasai wamechukua miaka mingapi kutoka Masai Mara Kenya mpaka kufika Morogoro? Kuna umbali gani kutoka huko?

9. Hizo km 600 mnaongelea actual route waliyopita au mnaongelea route ya ndege?
 
Wakati mwingine ni ngumu sana kutafakari mambo ya kiroho au kuuliza mambo ya kiroho huku ukiwa ktk Akili hizi za kibashite, mambo ya kiroho hujadiliwa na watu wa kiroho
 
Hizo ni story tuu

Maana na pia ilitakiwa waondoke speed maana majesh ya farao yalio zama baharin yalikuwq yanawqfwata

Sasa sijui hata Yale majesh yaliwafukuzia kwa muda gan??

Umbali toka misri mpk bahat aliotenganisha mussa n kiasi gan??

Kaz kweli kweli
 
Ilikuwa lazima wazungushwe sana toka misri hadi israel kusudi wapate kupigana na makabila yote yaliyokuwepo maeneo yale.Namba 40 ni namba ya ukamilifu wa jambo lolote mbele ya Mungu na wanadamu.
Mfungo wa yesu kristo ni siku 40,gharika ilichukua 40 days kukauka,waisrael jangwani 40 years,za mwizi ni 40, mtu akifa siku ya 40 msiba huisha,mtoto hutolewa siku ya 40 toka kuzaliwa.40 ni namba ya kinabii ktk ulimwengu wa roho.Namba ngingine zenye nguvu ni 3,6,7,12 na 24.
 
Mungu aliwajaribu waisrael kwa vita,njaa na kiu.Israel ndiyo taifa la kwanza duniani lenye uwezo mkubwa kijeshi kutokana na kuanza kupigana vita muda mrefu.
Waisrael wanaambiwa na Mungu kuwa wanajaribiwa ili uthabiti wao uweze kujulikana.Tambua kuwa majeshi mengi imara duniani yamejawa na waisrael wengi ama kwa kujua au pasipo kujua.Uingereza na USA ni mojawapo ufaransa na ujerumani.
Hakika israel ibarikiwe.
 
Point ni kwamba biblia ni philosophical book Kama vitabu vingine vya dini zingine na nini mapungufu mengi kutokana na muda unavyoenda na watu wanavyozidi kupata maarifa eg wote huongelea mwisho wa dunia Yaani ki umbile kitu ambacho hakipo pia tunajua chini ya aridhi hakuna Shetteni wala mungu hakuhofia kuwa mnara wa baberi Utafika kwake na kuwabali watu lugha wasifanikiwe huo ni uongo ka stori ya Sungura kuwa na mkia mfupi sasa hivi watu wanaenda mwezini wanarudi Poa bila kubadilishwa lugha Tujue ukweli ulipo tuache utumwa wa ujinga tulionao wa kuinvest mbinguni na kusahau maisha ya dunia tunakua omba omba
 
Very interesting. Kuna njia fupi Sana toka Egypt mpaka Israel. Haps kwenye ramani inaonekana walizunguka Sana! Kuna wakati walikua wanarudia tena kule walikotokea kisha wanaendelea. Walikua vipofu au?
Tatizo la kukumbatia dini za kimapoieo na kuacha imani zenu za jadi kwa kuwa tu tuliambiwa ni za kishenzi, ni upagani. Haya ndo matokeo yake na ni mojawapo ya sababu za umaskini na ujinga wa waafrika. Kupoteza muda makanisani wakimuomba Mungu awaletee mvua mtera ijae ili umeme uwake, shenzi zetu kabisa, wakati waarabu ni jangwa na wana umeme, wenzetu weuoe wanatimiza wajibu wao na simkumuachia na kumsumbua Mungu kila siku. Watu kwa wiki wanapoteza siju 3 hadi 4 wakisali badala ya kuwajibika. Alafu mnazuia maandamano na kuwaacha watu wakijiongezea umaskini kwa kushindia makanisani. Sisi ni viumbe wa ajabu kweli kweli. Tunashindwa kuelewa kuwa biblia ni masimulizi ya kimapokeo tu na ulimwengu wa sasa kuna ambayo sio valid tena. Bado mtu anaamini kuwa Yesu alikuwa mwana wa Mungu wakati bikiara maaria alipewa ujauzito na askari wa Rumi, Joseph akaamua tu kumtunzia heshima na kumuepusha na adhabu ya kifo. Endeleeni kupoteza muda naenda shambani.
 
Nimefanya research kwenye maandishi mbalimbali na ukweli ni kuwa km 612 ni distance ya ndege ambayo inachukua saa. 0.68.
Ninaendelea na utafiti kisha nitaleta hapa uzi unaoonesha kuwa walitembea zaidi ya km 2000 na speed yao ilikuwa km 28 kwa siku.
wildjour.gif

Hii ndio ilikuwa actual route. Kutoka hapo walipoanzia safari Geshon mpaka mlima Sinai ni km kama 780 ambazo walitembea kwa siku 44 tu.
Nachambua maandiko kisha nitakuja na uzi.
 
Nadhani '40' ni msemo wa wa-Israel kuonyesha kua ugumu wa Jambo au muda wa kutosha nk! Kuna maelezo mengi sana kwenye Bibilia yanayozungumzia '40 ' hata Yesu alifunga siku arobaini Mchana na usiku, na katika kufunga huko alikataa kabisa ushawishi wa shetani ambae alitaka atumie Mamlaka yake ya Kimungu ili kuondolea mbali shida alizokua anapata kama binaadamu . Bado swali linakua Binaadamu aliwezaje kukaa siku 40 bila kula?
The rt
 
W t
 
Back
Top Bottom