Umejiandaa vipi na maisha ya uzeeni (Retirement)?

Wazo zuri, ila mimi kwa mtizamo wangu ni vizuri kuwekeza kwenye vitu visivyo hamishika hususani nyumba. Ukiwa na nyumba zako kadhaa utakuwa na uhakika wa kupata hela kila mwezi, japo itakuwa kidogo lakini ni heri.
 
Hongera ndugu.
 
Ni jambo jema sana ambalo tunapaswa sana kuliwaza aisee mimi nimeanza kuwekeza kwa ajili ya uzee wangu
 
Maisha ni Leo ya kesho yatajisumbukia
 
Watu wa kizazi chetu tunadhani dunia imeanza juzi uzee upo tena kama huna ajira serikalini hapo huna hela ya kustaafu yaani utalia na kusaga meno
 
Anza kujiandaa kwa kufanya shughuli ya kukuingizia kipato kabla ya miaka 5 au zaidi ya kustaafu. Mara nyingi watu wengi huanza kujishughulisha na biashara au shughuli yoyote ya kuingiza kipato punde wanapostaafu, hii hupelekea wengi kuanguka sababu ya kutokuwa na uzoefu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…