Umejiandaa vipi na maisha ya uzeeni (Retirement)?

Umejiandaa vipi na maisha ya uzeeni (Retirement)?

Wana jamvi uzima na afya uwe kwenu nyote.

Hapa siongei na wavulana na vijana wa hovyo. Bali naongea na vijana na watu wazima wenye kujitambua haswa.

Ni ukweli pasina shaka kuwa maisha ya ujana yanapita upesi sana. Kama usipojiwekea malengo ya huko mbeleni utaishi maisha ya tabu sana.

Wala sio Siri wengi wa wazee tunao waona leo hii wanaishi maisha Duni, taabu na mateso walipitia nyakati kama zetu za utoto,ujana na utu uzima Hadi uzee.

Wengi wao wanaishi Kwa sonona na stress ya Hali juu mno ni vigumu kuwatofautisha na chizi.

Hivyo ukiona vile ni Vyema na haki nawewe ukajipanga Kwa ajiri ya kesho Yako.

Ningependa katika Uzi huu tupeane mbinu za kuwekeza Ili badae tuje tuishi maisha mazuri tukicheza na kuimbia wajukuu zetu kama baadhi ya wazee wanavyoishi Leo hii.

Ni furaha iliyo je uzeeke ukiwa na uhakika wa maisha mazuri na afya njema kabisa.View attachment 3118705
Wazo zuri, ila mimi kwa mtizamo wangu ni vizuri kuwekeza kwenye vitu visivyo hamishika hususani nyumba. Ukiwa na nyumba zako kadhaa utakuwa na uhakika wa kupata hela kila mwezi, japo itakuwa kidogo lakini ni heri.
Wana jamvi uzima na afya uwe kwenu nyote.

Hapa siongei na wavulana na vijana wa hovyo. Bali naongea na vijana na watu wazima wenye kujitambua haswa.

Ni ukweli pasina shaka kuwa maisha ya ujana yanapita upesi sana. Kama usipojiwekea malengo ya huko mbeleni utaishi maisha ya tabu sana.

Wala sio Siri wengi wa wazee tunao waona leo hii wanaishi maisha Duni, taabu na mateso walipitia nyakati kama zetu za utoto,ujana na utu uzima Hadi uzee.

Wengi wao wanaishi Kwa sonona na stress ya Hali juu mno ni vigumu kuwatofautisha na chizi.

Hivyo ukiona vile ni Vyema na haki nawewe ukajipanga Kwa ajiri ya kesho Yako.

Ningependa katika Uzi huu tupeane mbinu za kuwekeza Ili badae tuje tuishi maisha mazuri tukicheza na kuimbia wajukuu zetu kama baadhi ya wazee wanavyoishi Leo hii.

Ni furaha iliyo je uzeeke ukiwa na uhakika wa maisha mazuri na afya njema kabisa.
 
Ni wazo zuri kuja na hoja fikirishi ya namna hiyo;

Uzee unatisha

Uzee unaambatana na upweke pamoja na changamoto za kipato pamoja na maradhi.

Ni vyema kujiandaa na Uzee ukiwa bado una nguvu

Binafsi najitahidi kulinda afya Kwa kuepuka tabia hatarishi ambazo Kwa namna Moja ama nyingine zinaweza kuhatarisha afya Kwa kuleta magonjwa ya Uzeeni.

Pili nimeanza kujiwekeza, Kwa kufanya miradi itakayokuwa inaniingizia hela hata wakati wa Uzee.

Nisingependa kuwa Mzee msumbufu Kwa watoto wangu.

Niko mbioni kujikatia bima ya maisha, japo ni ghali lakini nitakata kwaajili yangu na Mke wangu
Hongera ndugu.
 
Ni jambo jema sana ambalo tunapaswa sana kuliwaza aisee mimi nimeanza kuwekeza kwa ajili ya uzee wangu
 
Watu wa kizazi chetu tunadhani dunia imeanza juzi uzee upo tena kama huna ajira serikalini hapo huna hela ya kustaafu yaani utalia na kusaga meno
 
Anza kujiandaa kwa kufanya shughuli ya kukuingizia kipato kabla ya miaka 5 au zaidi ya kustaafu. Mara nyingi watu wengi huanza kujishughulisha na biashara au shughuli yoyote ya kuingiza kipato punde wanapostaafu, hii hupelekea wengi kuanguka sababu ya kutokuwa na uzoefu.
 
Back
Top Bottom