Umejiandaa vipi na sikukuu za X Mass na Mwaka Mpya 2022 - 2023?

Umejiandaa vipi na sikukuu za X Mass na Mwaka Mpya 2022 - 2023?

Melki Wamatukio

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2022
Posts
6,156
Reaction score
10,974
Binafsi nimeandaa sherehe isiyo na kifani nyumbani kwangu[emoji122]

Kwenye kamati ya msosi na vinywaji...
Tayari nimekwisha nunua mbuzi mzima, mchele Kg 40, maharage Kg 15, choroko Kg 7,nimeandaa 80k kwa ajili ya viungo na mapocho pocho ya hapa na pale, tayari nishaleta kreti 8 za Soda pamoja na kreti kumi za Maji Machungu, nimeandaa kuni za kutosha kutengenezea diko[emoji39]

Nategemea hizo siku watu tukifinye cha mtume kikiwa na maharage kwa juu, huku kikipambwa na mboga za majani, ongezea sotojo la choroko, bila kusahau chai ya rangi yenye kuwasha. Baada ya hapo, watoto watajimwaya mwaya kwa chupa zao za mirinda na fanta, huku sisi watu wazima tukimwagilia nyoyo zetu

Kamati ya muziki na vinywaji...
Kutakuwa na burudani swafi ya muziki kutoka kwa dj ambaye tayari nimekwisha muandaa

Nyimbo zitakazo taradadi siku hiyo ni pamoja na ° Nimeachwa sitaki tena maswali ° Shetani ya Mbosso ° Nyimbo mpya za Kizz Daniel ° Unabore ya Mojji Short Baba ° Nyimbo za sauti sol, huku nyakati za usiku tutasindikizwa na nyimbo za "Adaa" na "Lusa"

N.B: Siku hizo nitatumbuiza taarabu za akina Mbosso na Jay Melody

Kamati ya Wageni...
Sherehe hii itafana kwa jitihada zangu, mke wangu na wanangu, bila kuwasahau majirani zangu

Nitatoa nafasi kumi za upendeleo kwa wakina dada wa jf. Kiingilio chao kitakuwa ni app ya jf kwenye simu zao

Nyote mnakaribishwa ila msije, nyumba yangu haitowatosha nyote[emoji119]

Karibuni Buhongwa Mwanza. Jumapili iliyopita niliondoka Dar es salaam

Nasubiri mialiko...
anjappar-catering.jpg
 
Ntakuwa ghetto, ntakaanga zangu viazi na mayai manne afu ntafta mirinda,

wanaume wenzangu mtanisamehe, ni hiyo siku tu ya sikukukuu itakuwa mwanzo na mwisho[emoji23]
 
Nasubiria mialiko ya majirani
Karibu Bibie, hata ukitaka VIP haitokuwa na shida, VIP itafanyikia Chumbani kwangu, kitanda kitakuwa na maua maua. Mke wangu atakuwa sebureni akiumwagilia moyo
 
Ntakuwa ghetto, ntakaanga zangu viazi na mayai manne afu ntafta mirinda,

wanaume wenzangu mtanisamehe, ni hiyo siku tu ya sikukukuu itakuwa mwanzo na mwisho[emoji23]
Dah, pole sana. Ungekuwa maeneo ya Mwanza ungekaribia mkuu
 
Dah nimekosa kitu cha mtume ningekuwa Mwanza ningekaribia
 
IMG_0164.jpg

siwezi kwenda iringa na mbwa wangu xmass ikifika wanaweza jua nimewaletea mbuzi wa kizungu
 
Back
Top Bottom