Binafsi nimeandaa sherehe isiyo na kifani nyumbani kwangu[emoji122]
Kwenye kamati ya msosi na vinywaji...
Tayari nimekwisha nunua mbuzi mzima, mchele Kg 40, maharage Kg 15, choroko Kg 7,nimeandaa 80k kwa ajili ya viungo na mapocho pocho ya hapa na pale, tayari nishaleta kreti 8 za Soda pamoja na kreti kumi za Maji Machungu, nimeandaa kuni za kutosha kutengenezea diko[emoji39]
Nategemea hizo siku watu tukifinye cha mtume kikiwa na maharage kwa juu, huku kikipambwa na mboga za majani, ongezea sotojo la choroko, bila kusahau chai ya rangi yenye kuwasha. Baada ya hapo, watoto watajimwaya mwaya kwa chupa zao za mirinda na fanta, huku sisi watu wazima tukimwagilia nyoyo zetu
Kamati ya muziki na vinywaji...
Kutakuwa na burudani swafi ya muziki kutoka kwa dj ambaye tayari nimekwisha muandaa
Nyimbo zitakazo taradadi siku hiyo ni pamoja na ° Nimeachwa sitaki tena maswali ° Shetani ya Mbosso ° Nyimbo mpya za Kizz Daniel ° Unabore ya Mojji Short Baba ° Nyimbo za sauti sol, huku nyakati za usiku tutasindikizwa na nyimbo za "Adaa" na "Lusa"
N.B: Siku hizo nitatumbuiza taarabu za akina Mbosso na Jay Melody
Kamati ya Wageni...
Sherehe hii itafana kwa jitihada zangu, mke wangu na wanangu, bila kuwasahau majirani zangu
Nitatoa nafasi kumi za upendeleo kwa wakina dada wa jf. Kiingilio chao kitakuwa ni app ya jf kwenye simu zao
Nyote mnakaribishwa ila msije, nyumba yangu haitowatosha nyote[emoji119]
Karibuni Buhongwa Mwanza. Jumapili iliyopita niliondoka Dar es salaam
Nasubiri mialiko...View attachment 2438594