Umejiandaaje pale Familia yako itakapokutenga?

Unaweza kumfikiria kuhusu pesa zinaweza kukupa furaha lakini pesa siokitu katika kuitafuta furaha ya mtu kikubwa ni kuridhika na uhalisia uliopo na endapo ikatokea umezeeka Basi jitahidi utilize presha za kuwaza umezeeka Hali hauna pesa waza ni kwa namna gani utamalizia maisha yako ya uzee ukiwa na furaha na kuacha urithi wa busara na jumbe za kujenga katika jamii yako au familia yako usije ukatamani kujiangaisha kwa kutumia nguvu nyingi Wala akili nyingi ili kuishi ukiona huna kabisa uwezo wa kujihudumia sogea mahali panapoitwa kabisa au msikiti utaishi vizuri tu na utafurahia uzee wako kwa furahaa kiongozi . Au ukizeeka pia utakuwa unataman utajwe kwenye list ya wazee matajiri?
 
True lazima wakutenge uzeeni baada ya kulishwa sumu na mama yao ambae ni mkeo ,bila kujali umekuwa masikini Ili wao wafanikiwe.Kumbuka ipo vita baridi tena ya asili Kati ya mwanamke na mwanaume, mwanamke upambana Ili kumpiga vita mwanaume akiwashirikisha watoto wawe upande wake dhidi ya adui wake mwanaume. Mzee wa fasihi ataielezea hii zaidi.
 
Mtu pekee ambae hawezi kukutenga au kukuacha wakati wa dhiki na tabu ni wawili,Mama yako mzazi na Yesu Kristo pekee. Hao wengine usiweke tumaini lako.
Hasa kizazi hiki cha kuanzia mwaka 2000 ni kizazi kilichopo kwenye reformation sio cha kutegemea kabisa.
 
Nikweli nipo Dunia tofauti Sana Tena kwa asilimia 100 mzee kwa sababu zifuatazo

1) kimtazamo wa kutegemeana Mimi naamini maisha ya yakwangu Mimi Kama mwanaume lazima niyapange na kuyasimamia yatimie kwa nguvu zangu zote ikiwemo kuhakikisha familia yangu inapata mahitaji yake yote na kufanya uwekezaji kwaajili ya mahitaji ya uzee wangu Mimi na mke wangu ili hata ikija kutokea watoto hawapo na Mimi au nimetengana na mke wangu lazima furaha yangu na amani vibaki salama

2) Kama mwanaume lazima uipange akili yako kujua jukumu la furaha yako inakutegemea wewe mwenyewe ila furaha ya familia yako inakutegemea wewe Sasa ili usijekutengwa siku za usoni Basi jitambue nafasi yako na uiaminishe akili kuwa watakiwa kuwa neutral ili usije kuchanganyikiwa yatakapo tokea niaibu Sana mwanaume kulalamika umetengwa au kuachwa mwanaume anatikiswa kidogo tu ila hayumbishi na mawimbi
 
Katika maisha ya nyakati za sasa kutengwa ni very real. Nimeona wazee wengi wameachwa peke yao vijijini huku vijana wao wakiendelea na maisha mjini.

Kama kuna kitu wazazi wa leo na wazazi watarajiwa tunatakiwa kujiandaa nacho ni hili la kujiandalia maisha ya kujitegemea hadi siku za mwisho za uhai wetu. Kutegemea watoto ni kujiweka kwenye mtego ambao unaweza kunasa na usitoke
 
Hili linajulikana na wanaoyengwa huwa ni wanaume wala usizunguke Sana.
 
Na hii tabia ya wazee kutegemea laana haitawasaidia,binafsi napendelea kutunza pesa kwenye account ya bank kuliko kuweka mali zinazoonekana kwa sababu watoto watukutu wanaweza kukufanyia unyama.
 


Huko mbeleni Sisi ndio tutaipata hasa Wale wasio na makazi
 


😊😊😊
 
T U J I F U N Z E K U J I T E G E M E A
 
Kuna sehemu ubongo wangu umefunguka aisee....

Nishastukaaaaaaa

Yaani kwa somo hili,tunatembea na sumu za panya ndani ya familia tulizoziumba wenyewe
 
Wewe haunaga jipya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…