Umejifunza au ulijifunza jambo gani kipindi unapopitia au ulipopitia nyakati ngumu maishani mwako?

Sikuwa naishi naye nyumba 1, akiishi mbali nami na wala sikuwa namtegemea kwa kila kitu. Kwa mfano nilikua najilisha mwenyewe na wakati huo huo nikampa pesa kama 1.1m aongezee mtaji ila kwa kuwa sikuwa na kazi maalum alikua hana imani kabisa.
 
Sikuwa naishi naye nyumba 1, akiishi mbali nami na wala sikuwa namtegemea kwa kila kitu. Kwa mfano nilikua najilisha mwenyewe na wakati huo huo nikampa pesa kama 1.1m aongezee mtaji ila kwa kuwa sikuwa na kazi maalum alikua hana imani kabisa.
Kwa mwanamke kutokuwa na kazi maalumu maana yake huna kazi
 
Sasa elfu 5 ndo umdai mwanamke??? Nyie kweli mnatafuta maishaaa
 
Pole sana mkuu ilikuaje?
 
I feel you bruv, itakua uliingia kwenye mikopo ukashindwa kulipa ukafilisiwa i guess.
 
Mimi nilijifunza kuwa hata simu kuita ni kwa sababu nina kaauheni kwenye maisha.

Kuna wakati sikuona simu ya ndugu,rafiki wala mzazi kwa sababu pengine simu zao zilikutana na kinywa changu kilichojaa manung'uniko na kuombaomba.

Nikajifunza kwamba siku zote kwenye maisha yangu nitajitanguliza mimi kwanza kwa kuwa mimi ndiye niliejifariji mwenyewe wakati huo.
 
Nilichotaka niandike kimeandikwa na kurudiwa na watu wengi.

Summary:
1. Nyakati ngumu huja na kupitia

2. Kumuamini binAdamu YEYOTE ni kosa lisilorekebishika

3. Mungu anapaswa kuheshimika, akitoka Mungu anayefuata ni pesa

4. Upendo ni uongo, ukipitia wakati mgumu kifedha hakuna wa kukupenda.
 
msaada wa kweli, faraja ya kweli, ushindi wa kweli, watoka kwa Mungu, usitegemee wanadamu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…