Umejifunza au ulijifunza jambo gani kipindi unapopitia au ulipopitia nyakati ngumu maishani mwako?

Umejifunza au ulijifunza jambo gani kipindi unapopitia au ulipopitia nyakati ngumu maishani mwako?

Unapopitia nyakati ngumu kiuchumi unatakiwa usilete unyonge nyumbani......sio unashinda tu nyumbani.....

Unatakiwa kwa muda huo ukiwa unasikilizia mambo yako........fanya kazi yoyote iliyo mbele yako ili uweze kutatua mambo madogo madogo hapo home..........

Mwanamke ni kiumbe dhaifu na muoga.....ukimuambia kuwa huna kazi akili yake inaogopa na anawaza mbali sana.....
Sikuwa naishi naye nyumba 1, akiishi mbali nami na wala sikuwa namtegemea kwa kila kitu. Kwa mfano nilikua najilisha mwenyewe na wakati huo huo nikampa pesa kama 1.1m aongezee mtaji ila kwa kuwa sikuwa na kazi maalum alikua hana imani kabisa.
 
Sikuwa naishi naye nyumba 1, akiishi mbali nami na wala sikuwa namtegemea kwa kila kitu. Kwa mfano nilikua najilisha mwenyewe na wakati huo huo nikampa pesa kama 1.1m aongezee mtaji ila kwa kuwa sikuwa na kazi maalum alikua hana imani kabisa.
Kwa mwanamke kutokuwa na kazi maalumu maana yake huna kazi
 
Hakika nimepata faraja, ila wanawake sijui ni viumbe wa aina gani?.

Nimeamka sina kitu zaidi ya 5000 mfukoni nikamwambia mwanamke kuwa sina kitu ila 5000 kaniomba hiyo 5000 akanunue mboga ya siku nyingine (siku hiyo ilikuwepo), kwa madai kuwa yeye ana hela atanipatia.

Imefika muda wa kuondoa chombo nikaweke mafuta niingie kutafuta riziki, namuomba pesa anasema "Hivi ni kweli huna pesa?, mimi nilijua unatania."

Yaani nilikasirika, kagundua akaniambia eti akauze ile mboga ili anirudishie pesa yangu, (si aibu hizi jamani?)

Nilimuangalia tu nikakaa kimya, kazurula karudi bila kitu anajichekecha chekesha tu, mimi nina hasira zangu hapo aiseee. 😥😥😥
Sasa elfu 5 ndo umdai mwanamke??? Nyie kweli mnatafuta maishaaa
 
Nilitumia nguvu, akili, pesa kujenga maisha ya ndoto yangu familia ya ndoto yangu..

Nilipo pita Nyakati ngumu kila kitu nilichokuwa nacho kilipotea kuanzia mali, mke na watoto.
Inauma sana..
Sasa nipo peke yangu nimerudi kukaa gheto walah kutoka nyumba zima self.!
Kwangu maisha hayana maana naishi ishi tu.
Pole sana mkuu ilikuaje?
 
I feel you bruv, itakua uliingia kwenye mikopo ukashindwa kulipa ukafilisiwa i guess.
Nilitumia nguvu, akili, pesa kujenga maisha ya ndoto yangu familia ya ndoto yangu..

Nilipo pita Nyakati ngumu kila kitu nilichokuwa nacho kilipotea kuanzia mali, mke na watoto.
Inauma sana..
Sasa nipo peke yangu nimerudi kukaa gheto walah kutoka nyumba zima self.!
Kwangu maisha hayana maana naishi ishi
 
Mimi nilijifunza kuwa hata simu kuita ni kwa sababu nina kaauheni kwenye maisha.

Kuna wakati sikuona simu ya ndugu,rafiki wala mzazi kwa sababu pengine simu zao zilikutana na kinywa changu kilichojaa manung'uniko na kuombaomba.

Nikajifunza kwamba siku zote kwenye maisha yangu nitajitanguliza mimi kwanza kwa kuwa mimi ndiye niliejifariji mwenyewe wakati huo.
 
Nilichotaka niandike kimeandikwa na kurudiwa na watu wengi.

Summary:
1. Nyakati ngumu huja na kupitia

2. Kumuamini binAdamu YEYOTE ni kosa lisilorekebishika

3. Mungu anapaswa kuheshimika, akitoka Mungu anayefuata ni pesa

4. Upendo ni uongo, ukipitia wakati mgumu kifedha hakuna wa kukupenda.
 
Habari za muda huu wapendwa.

Maisha ni safari ndefu sana yenye milima na mabonde.

Kuna nyakati unapitia Raha mpaka unajiona hapa duniani upo peke yako.

Kuna nyakati unapitia msoto mkali mpaka unajuta kuzaliwa, lakini kila nyakati tunazopitia kwenye maisha zinabeba ujumbe na mafunzo ambayo unaweza kunufaika kwayo siku za mbeleni.

Si vibaya kama uta share baadhi matukio ya nyakati hizo zilizokufanya ujifunze mambo mengine ya msingi.

NB;
Mimi binafsi nilipofukuzwa na kazi na kuishi maisha ya dhiki ndio nilijifunza kuwa thamani ya mwanamume kwenye jamii, ndoa au hata familia ipo kwenye kutoa.
msaada wa kweli, faraja ya kweli, ushindi wa kweli, watoka kwa Mungu, usitegemee wanadamu.
 
Back
Top Bottom