Victor Mlaki
JF-Expert Member
- May 1, 2016
- 5,628
- 6,411
Uwepo wa mtu yeyote Duniani ni uwepo wa zawadi awe anajua au hajui. Uumbaji umeweka zawadi ndani ya kila kitu kwa ajili ya kila kitu. Zawadi uliyokuja nayo siyo kwa ajili yako ila ni kwa ajili ya Jamii. Mti wa muembe zawadi unayoitoa ni maembe ila wenyewe hauli maembe.
Zawadi uliyokuja nayo ni kwa ajili ya wanaokuzunguka siyo lazima unufaike wewe ila elewa unayo zawadi kwa ajili yetu na sisi tunayo zawadi kwa ajili yako. Kwa ujumla Dunia imejawa na zawadi mbalimbali. Hatuna zawadi ya aina moja, upekee wetu ni ishara ya utofauti wa zawadi zetu.
Hatuna zawadi ileile ndiyo maana halipo haja ya kufuata mtiririko tulioukuta na badala yake tunapaswa kuleta mabadiliko. Dunia ya leo imejawa na makundi mbalimbali ya watu waliojitungia Sheria mbalimbali Ili kuleta mtiririko fulani na kuzima upekee ambao kwa hakika ndiyo msingi wa zawadi zetu.
Mchungwa huzaa mchungwa hata kama ukipandwa katikati ya mipapai, mfano huu nimeutoa nikimaanisha kuwa, upekee wa kila mtu ndiyo ladha halisi na zawadi ya Dunia licha ya ukweli kuwa leo wanadamu tumefunikwa na wingu zito la utumwa usiokoma.
Ni vigumu sana muembe kuzaa mchungwa, hapa namaanisha zawadi uliyokuja nayo inapowekewa utaratibu unaozima upekee wako ni zaidi ya majanga. Siyo kosa kuwa wa pekee katika mfumo wa asili wa kiumbaji ila leo ni hatari sana kuwa wapekee katikati ya Jamii iliyojitungia utaratibu wake unaotaka watu wawe namna fulani.
Jamii leo ni kama inataka watu wawe na mtazamo fulani, wa aina fulani waliyoipanga wao kwa maslahi fulani jambo ambalo kwa hakika linaifanya Dunia kuwa mahali pagumu sana kwa sababu ni kama kuzuia maji yasifuate mkondo wake. Utofauti wetu katika mambo mbalimbali ni njia muhimu ya kuzalisha zawadi zetu.
Tafakari juu ya hili: "ndani ya matunda ya mimea mingi Duniani ndimo zinapopatikana mbegu za mimea hiyo". Maneno haya ni sawa na kusema zawadi ya mtu ni sawa na tunda la mtu, tunda lina mbegu. Unapotoa zawadi aliyokupa Mungu kwa wengine ni sawa na kupanda mbegu. Hapa ndipo ilipo siri ya utoaji ambayo lugha ya asili ya kiumbaji hufundisha.
Watu wenye moyo wa upendo wanapotoa zawadi kwa wengine katika lugha ya asili huwa wanapanda mbegu zao ambazo kwa wakati wake huota na hapo ndipo tunapowaona kama wanafanikiwa sana pamoja na kutoa sana kuliko wale wanaoona kutoa ni sawa na kupoteza.
Dunia imefunikwa na mbadilishano wa zawadi, kila kitu kinahitaji kutoa. Hakuna njia nyingine rahisi ya kupata uyatakayo kama njia ya kutoa zawadi yako kwa Jamii kwa sababu ndilo kusudi haswaa la wewe Kuwepo katika Dunia hii.
Suala la msingi ni kutoa zawadi yako, suala la anaipenda nani au anaichukia nani siyo la muhimu. Mchungwa unapozaa mchungwa haujiulizi nani atayapenda au nani atachukia unazaa matunda kwa wakati wake. Ni binadamu tu ndiye aliyejiweka kifungoni kwenye gereza kubwa la mtazamo na hisia.