Umekutana na kero gani benki ambayo ilikukwaza na kukupotezea muda? Wataje hapa wajirekebishe

Umekutana na kero gani benki ambayo ilikukwaza na kukupotezea muda? Wataje hapa wajirekebishe

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2021
Posts
590
Reaction score
1,648
Wakuu,

Kuna baadhi ya benki ukienda kupata huduma unaenda umetabasamu ukitoka unatamani upasuke kwa hasira.

Baadhi ya kero ya kero ni wadumu kufanya mambo mambo taratibu sana, mtu mmoja anatumia hata nusu saa halafu kikubwa kinachofanyika hakuna.

Ama unakuta benki ina madirisha mengi lakini yanayotoa huduma ni mawili tu au moja, bado hujaongeza kufanya mambo taratibu na wahudumu kutoka toka kwenye vyumba vyao, DTB mjitafakari😡.

Benki gani inakuchefua kwa huduma zao mbovu, nini kilifanyika/hakikufanyaka ipasavyo kikakupotezea muda na kukuharia siku?
 
Huduma za kibenki zimehamia mikononi kuna watu bado mnapanga foleni benki?

Labda wenzetu mna mahela mengi, sisi wa vijihela tunamaliza mikononi mwetu kwa simu, simple.
Kuna nyakati ambazo unalazimika kwenda benki, inawezekana isiwe kutoa au kuweka pesa, ukahitaji huduma nyingine
 
Walinambia nikafate kitambulisho cha nida na sio namba tena kwa ukali kama mwalimu wa physics nikamuuliza ni kipi nimekukwaza mama asilimia kubwa vitambulisho hatuna tuna namba fanya kazi kwa kusaidia jamii hata kesho mteja asijutie kuja sio kuja kuleta makasiriko ya nyumbani kwa wateja naomba nionyeshe huo utaratibu wa benk ambao unataka kitambulisho cha nida tu? nikatoka nakaribia kutoka nje kabisa mlinzi kaniita nikarudi kaniomba radhi nikahudumiwa.
 
Huduma za kibenki zimehamia mikononi & mitaani kuna watu bado mnapanga foleni benki?

Labda wenzetu mna mahela mengi, sisi wa vijihela tunamaliza mikononi mwetu kwa simu, simple.
Kuna baadhi ya ishu ATM sio msaada hata kama hauna hela nyingi
 
Sipendagi kero za hivyo. Kuna wakati crdb niliwakimbia sababu ya kujidai dai nikahamia equity. Napo nilijuta mara hamna mtandao unataka ulipie kitu usiku mtandao hamna. Nikaenda kutoa hela zangu nikarudi crdb. Siku hizi kila wiki equity wananipigia account yangu imelala.
 
Ukweli mm Sina kero kwa mabenk isipokuwa moja tu kwa nn unapochukua mkopo hasa kwa wafanyakazi Kuna Ile bima ya mkopo zaman kidogo bima hii ilikuwa inalipwa kidogo kidogo mpaka unamaliza mkopo lakin siku hizi wanakata kwa mara moja ukweli Jambo hili lingerudishwa Kama zaman maana lilikuwa linatoa nafuu kubwa Kwa maana mkopaji. Sa hv ukienda unataka hata 20m basi karibu 2m unaweza kuziacha bank. Nashauri bima ya mkopo ilipwe kwa awamu mpaka iishe kwa mfumo wa sasa sio rafiki kwa mkopaji kabisa .
 
Back
Top Bottom