KERO Umeme unakatika sana hadi inakera maeneo ya Matika, Wilaya ya Ludewa (Njombe)

KERO Umeme unakatika sana hadi inakera maeneo ya Matika, Wilaya ya Ludewa (Njombe)

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kero yangu ni kukatika-katika kwa umeme mara kwa mara katika eneo la MATIKA, Kata ya Lugarawa, Wilaya ya LUDEWA, Mkoa wa Njombe huku wahusika wakikaa kimya bila kufanyia ufumbuzi suala hili, tunaomba TANESCO Wilaya ya LUDEWA watueleze ni lini tatizo hili litakwisha maana imekuwa ni kero kubwa hasa nyakati za jioni.

Umeme huwa unakatika mara kwa mara hasa nyakati za jioni kuanzia Saa 12 mpaka Saa tano usiku na hakuna taarifa zozote za kufanyia ufumbuzi ni kero sana.

Ni mwezi mzima na tunashindwa kuangalia hata taarifa za habari usiku maana umeme unakatika kila muda, kwakifupi hatuna furaha na umeme wao ni kama tunapewa msaada.
 
Habari, Ndugu Mteja.

Kwanza, tunaomba radhi kwa kuchelewa kukupatia mrejesho kuhusu suala lako. Kwa kipindi hicho, akaunti yetu ilikuwa inakabiliwa na changamoto kwa muda, hali iliyosababisha kuchelewa kwetu kufuatilia na kujibu baadhi ya taarifa za wateja. Hata hivyo, kwa sasa akaunti yetu inafanya kazi katika hali ya kawaida.

Kwa kuwa muda umepita tangu ulipowasilisha taarifa yako, tunaomba utufahamishe ikiwa changamoto hiyo tayari imetatuliwa au bado unaendelea kukutana nayo, ili endapo bado ipo tuweze kukufanyia ufuatiliaji na kutoa msaada stahiki.

Asante! ^CM
 
Back
Top Bottom