Umeme wa Zero tarrif Bado upo, wavuja Jasho changamkieni fursa

Tulipiga simu, kuuliza wakasema kwa hapa dsm hii huduma wameitoa, labda vijijini
Ukisikia uchawi ndo huo sasa, watu wa kipato Cha chini wapo Nchi nzima,

Usikate tamaa, jaribu tena wakati tukiendelea kuomba Maharage ya chande YACHACHE!!!
 
Uko sahihi kwa 72 au 73 pia...
Ilikuwa 75 Units

Ni kweli kabisa mwanzoni mwa Huduma hii ilikuwa ni Units 75, hii ilikuwa kabla ya makato ya Kodi ya majengo au kodi ya Ardhi ambayo kipindi inaanza ilikuwa 1000 hivyo umeme ukapungua unit na ukawa Unit 73 baada ya makato yao....

Kivumbi kimekuja Mwaka huu hahaha mwezi wa Nane Baada ya kupandisha Kodi ya Majengo ambayo kwa sasa ni Tsh 1500 na sio 1000 tena Units zimekuwa 69.1...

Na kias cha kulipia Kila mwezi kulingana na mkataba Na Tanesco ni Kiasi cha Tsh 9950 hautakiwa uzidishe kwa sababu ukizidisha Kiasi hichi Mfululizo kwa miezi miwili utatolewa kwenye Huduma....

UZUSHI;-
Kwamba lazima uzitumie ziishe zote Hapa si kweli hata kidogo...
Unaweza ukatumia umeme na ikafika mwisho wa mwezi umebakiza unit 30 unaruhusiwa kuongeza na zitajumlishwa kwenye unit zako mpya na kadhalika mwezi ujao na wenyew hivyo hivyo hakuna atakaye kunyang'anya unit....
 
Tulipiga simu, kuuliza wakasema kwa hapa dsm hii huduma wameitoa, labda vijijini
Mkuu huduma Ipo ni connection Tu πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€ Hizi huduma huwa zina manufaa sana huwez zipata Simpo simpo kama unavofikiria
 
Hapo kwenye connection wakati ni HAKI ndo KICHWA Huwa kinapata moto!!

Ingekuwa ndani ya uwezo wangu, wakikiona Cha moto.
Hahaha Mkuu nchi yetu ilishaharibika Sana kuirekebisha ni Ngumu sana kwa sababu ukipeleka maswala ya Haki ndo lazma ujibiwe kwamba Dar Haiwezekani ilaukienda mwenyewe pale TANESCO na kisuuzio cha Roho ukaongea VIZURI (ELEWA MAANA YA NENO VIZURI) Na wahusika Siku hiyo hiyo unapata Namba za kubadili Mita yako
 
Ndomana tunaendelea na maombi, Maharage ya Chande pia YACHACHE!!
 
Ipo ila kwa mijini inahitaji ukunjue mkono. Vijijini wanaunganishwa moja kwa moja kwenye matumizi madogo
Mkuu kwasasa hata huko kijijin ambapo wapo REA walishaacha kuunganisha matumizi madogo mojakwamoja mpaka ujiongeze,ninakibanda kijijin nimeunganisha umeme toka Novemba mwaka jana nimevuta subira hadi mwakahuu mwezi wa6 sijaunganishwa hayo matumizi madogo ikabidi nijiongeze ndani yamasaa manne napokea msg POKEA KEY CHANGE kundi lakwanza___ kundi lapili ___
 
Usitoe RUSHWA siku ingine,

HAKI hainunuliwi!!
 
Kaka, hii mada ya mda but am interested. Hivi malipo ni 9950 au 9150? Mwanzo nilikua najua ni 9500, then kuna mtu akaja niambia ni 9150, so kwa muda sana sasa nalipa 9150, ukiplus na haya makato unit zinazidi tu kushuka! Now napata 62 mostly! Kimtazamo ni bora hii 1500 wangeiongezea juu yake, ili mtu upate zilezile unit 75, ingesaidia sana!
 
Unaweza kununua hata baada ya umeme kuisha, kununua ziada mara moja ama mbili haikuondoi katika utaratibu huo, ukizidisha mara tatu ndio hukuondo, japo kwa walio mijini hata mara mbili unaondolewa
 
Mkuu upo kijijini au town?
 
Town, sema huduma iliungwa kitambo sana.
Dah awamu hii acha niandae fungu. Last tume nilicomment humu ilikua ni 2023, niliangukia pua kwa kufata taratibu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…