Mtazamo wangu mtu akiniambia nimemharibia maisha:Kwa mtu ninayempenda sidhani kama nitamharibia maisha,kama kumharibia maisha anayozungumizia ni kumpotezea malengo kama vile masomo au mimba n.k,ambayo haikutarajiwa basi nitakuwa karibu naye na kumsaidia kadri ya uwezo wangu ila yeye ajue kwamba amechachangia kiasi gani nimemharibia maisha yake?na alikuwa hajui matokeo?kama sio mwelewa basi lawama zake hazisaidii maana yeye pia alichangia ktk kuharibu maisha yake.
Kwanini nione maisha hayana thamani?:Mimi kama Excellent naamini maisha yangu yana thamani sana na ninajua huyo mtu nilikutana naye tu na kabla yake nilikuwa na mfumo wangu binafsi wa maisha,kwahiyo hakuna kitakachobadilika maana najua maisha nikupambana ktk situation yoyote.
Kwanini kinyongo,chuki,fitina,wivu,hasira?:ni aliniharibia maisha,nadhani atakapokuwa mbali na mimi nitakuwa nimeutua mzigo wa mwiba na sitakuwa na chuki,fitna wala wivu au hasira.
Msiba wa mtu uliyemharibia maisha unaumiza sana,kama ulimharibia maisha mfano ulimbaka,H.I.V n.k lazima moyo uumie na daima hilo litakushitaki na hutapata amani wala utulivu wa moyo kwa kumharibia mtu ambaye ni innocent.
Mwenza wangu akiniambia atajiua maana maisha yake hayana thamani bila mimi:ukweli ni kwamba akinisaliti halafu aniletee hiyo kauli then tutaona ni jinsi gani maisha yake hayana thamani bila mimi.
Suluhisho kukabiliana na mtihani huo:Suluhisho ni kuwa makini katika uhusiano wa kimapenzi,kufanya ngono salama,kuwa waaminifu,kuaminiana,kuthaminiana na kuboresha mapenzi kila siku.Pale inapotokea mwingine kapata tatizo kwa ajili ya mwingine mchukuliane,kuelewana,kutafuta suluhisho pamoja na siyo kumkimbia mwenza wako wakati wa matatizo.[/QUOTE]
This is excellent piece of advise, niot only for married couples, but also for lovers.....