Umeniharibia maisha! ...what?

Hahahah nimegundua sie wengine tunajomasikinisha wenyewe kwa kujitia twajua kususa loh! Mie nlimsusia mpaka vya kwangu! Laiti ningemjua Matty mapema hakuna rangi angeachaiona mbaba yule.

Ukisusa mpenzi inakula kwako, maana mitoto yenyewe ya siku hizi hasa wangu mchaga huyu naona wakizaliwa tu wanavutiwa kwao. Mzazi unajitia kususa kama pesa ninazo nitatunza mwanangu mwenyewe unajipinda mtoto akikua huyooooooooooooo kwa babake, unabaki unajuta na kuona bora mngetunza wote. Kuna vitu vya kususa bana, mie pesa yangu kibindoni atunze mwenyewe mtoto wake na akijiletaleta na mimi nakula pia nani kasema pesa inatoshaga zikija nazifyandula vilivyo.
 
Reactions: Mbu
Leo leo Gaga,Maty,MJ na nyamayao kuna mtu atanyofolewa huko aliko kama naziona hasira zinavoishia kwenye keyboard.

Hhahaha lol, we chauro acha uchokozi lol
 
Sijasema urudiane nae....ila nimesema unaogopa ukikaa nae karibu mtarudiana.....trying to say you not over him...
Ila naishia hapa...right?

nope...endelea! kurudiana nae itakuwa ni ndoto za alinacha, kwa muda alionisumbua kama angekuwa amebakisha ka sehemu ka upendo moyoni mwangu ungekuta hata nimeshasema nikae japo nimckilize uongo anaotaka kuniambia, hana nafac kabissa kwenye lyfe langu, it was swir....
 

Case rested darling.....me knows u, remember?
 
Kazi ipo...

mpenzi si ndugu yako. Jiweke tayari kwa lolote i.e kuishi hadi kifo kuwatenganisha au kutemana ikibidi na kulazimu.
 
Ukiwachia mambo ya ukatili yaliyotajwa kama kubaka au kuambukizana magonjwa, matukio mengine yote katika mahusiano hayawezwi kusemwa kuwa "Umeniharibia maisha".
Tatizo ni kuwa wengine wanapopenda, hujisahau na kuwa "wategemezi" sana kwa wanayempenda kiasi siko wakiwachwa saa yao ya kuishi huwa imeishia hapo. Mfano.mmeishi pamoja miaka 10 na kuendelea, siku moja mwenzako anakwambia tumeishia hapa na wewe unasema umeharibiwa maisha. Tukumbuke mapenzi huzaliwa, hukua na hufa...siku yakifa yamekufa na usidai umeharibiwa maisha.
Je ikiwa kwa mfano huohuo hapo juu, baada ya miak 10 na zaidi Mwenyezi Mungu anaamua kumchukua mwenzako, jee nani utalalamikia amekuharibia maisha, yule "aliyeamua kufa na kukuwacha katika mataa" au utamlaumu Mungu aliyempenda zaidi?

Ushauri: Katika mapenzi tujaribu "kuogelea na nguo zetu mkononi", tuwapende tunaowapenda lakini tubakishe asilimia fulani ya mapenzi kwa ajili yetu, nikiwa na maana tujitayarishe kwa lolote bila ya kujiwacha na kuja kutafuta mchawi baadaye.
 
Wapendwa,

Binafsi naamini katika kuwa na kiasi. Ukitaka kuishi maisha ya furaha ni bora ukawa na kiasi. Hata katika kupenda, hatuna budi kupenda kwa kiasi na kuweka angalizo moyoni.."nitafanya nini mwenzangu asiponipenda ninavyompenda mimi"?. Jibu la angalizo hilo halipasuwi kuwa kujiua; kwa maana si suluhisho sahihi la tatizo. Kila mcha Mungu hatachukua uamuzi wa kujiua, maana twajua Mungu mara zote ana fikra nzuri kwa wamchao.

TUMCHE MUNGU; NA HAKUNA MWANADAMU AWAYE CHINI YA JUA AWEZAYE KUHARIBU MAISHA YA MWENZAKE.

Tumsifu Yesu Kristu.
 
mjadala mzuri sana mbu...!hongera sana na tunashukuru sana!mawazo binafsi: kwenye hili swala uloleta hapa wahanga wa kubwa wa kukata tamaa na kunakopelekea kujiua ni WAKINAMAMA!...na sio kweli kwamba wanaume hawaharibiwi maisha.kinachowatofautisha wanaume na wakinamama ni ''a degree of emotions''....tafiti zimeonyesha asilimia kubwa ya wakinamama wako too emotional,kiasi cha kujichukulia maamuzi ya ghafla mojawapo ni hilo la kujiua.ukweli hii biashara ya malovee ni ngumu sana.ushauri binafsi:your thread must and it has to be a ''wakeup call to all the women'' na wajue wazi kabisa hakuna sababu ya kuwa emotional au kuumia sana kwenye hii tasnia ya mapenzi kwakuwa tu kila mtu alizaliwa peke yake na hakuna aliyezaliwa kwa ajili ya mwingine..HAKUNA KABISA!mahusiano kama mahusiano hujengwa na hisia na state of mind.kuna vitu vingi sana vizuri na vya maana vya kuangalia kuliko hao wapenzi.....!kwamba mtu unajiua kisa umeumizwa na mtu unaempenda SIO KWELI...!au kudanganywa na vimisemo kama I WAS BORN TO MAKE YOU HAPPY...AU SIJUI I CAN'T LIVE WITHOUT YOU...hapana hapana!sio kweli.huwezi ukafikiria kujiua wakati wewe unajua kabisa unawajibika kwa wazazi wako kwa kukufikisha ulipo au kama ndo familia zetu za kiafrika wazazi na familia wanajinyima ili wewe ufike walau university...halafu mwaka wa nne wa shahada ya sheria unajitupa ghorofani pale HALL FIVE kisa mwanaume..!hapana hapana!wakina dada muwe na huruma japo kidogo kwa wazazi na familia zenu japo kidogo!...ahsante sana mbu!
 
Du maisha yalivo matamu nijiue kisa, maisha lazima yaendelee after broken heart, ni kweli unakuwa dissapointed na huyo jamaa lakini ina budi utafute njia ya kujikwamua urudie maisha ya zamani, jiulize kabla yake ulikuwaje utapata moyo wa kuendelea
 
Haya mapenzi mkuu yanavochipuka, ni vigumu kujicontrol kabisa
 


Haya wadada mnaochipukia mapenzini maushauri haya yenye ujumbe mzuri sana mkijumlisha mifano tuliyotoa dada zenu Mungu awape nini? hatutaki kusikia tena mtu analalamika katendwa hapa au kaharibiwa maisha. Jitahidini kutumia akili na si mioyo yasije wakuta yaliyowahi tukuta sie. Jitahidini pia elimu hii muwape na ndugu jamaa na marafiki ambao kwa namna moja au nyingine hawawezi ingia humu na kusoma.

Mwisho shukrani kwa Mbu kwa kuanzisha hii thread mimi nimeprint kabisa thread nzima naenda weka kwenye file binti akiongezeka kidogo tu nampa somo nikimaliza nampa na file zima akajisomeage. Kazi ibaki kwake ajiharibie maisha au ayaboreshe.
 

hasa cheki huyu hapo chini

 
vikikwama jipe hili
"I will survive" by Gloria Gaynor
 
Mie mpaka leo nashutumiwa kwa kumharibia mtu maisha yake..
 
Reactions: Mbu
 
Thanks mkuu for the compliment
 
hapa jamani wengine tulikumbwa na upofu, msiuombee huu upofu jamani, lakini tulijifunza kutokana na makosa, sasa hivi yaani roho nyeupe tayari kwa kupokea lolote litakalotokea.
Pole sana nahisi sasa hivi upofu umekutoka unaona hadi nukta, haya mambo usipoyapatia unaweza tembea mikono kichwani kila siku
 

mkuu ujue hili ni mtu na mtu tu....Ukiona mtu amejiua au anataka kujiua si utani anajua mwenyewe tu how pains he/she is facing.....Usiusemee moyo alisemaga lady jaydee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…