Umeniharibia maisha! ...what?

Umeniharibia maisha! ...what?

Na yule aliyeletewa magonjwa kwenye ndoa (mfano ukimwi)...,???
Au yule anayeambiwa na mwenzake kuwa kila anachofanya akiwezekani badala ya kumpa moyo
Mkuu all in all mafanikio yetu au kutokufanikiwa kwetu kunategemea the Company we Keep na ni nani tunashirikiana nae..,

Mkuu, hata hilo la UKIMWI linaweza kuwa la kujitakia.
Likitokea ndani ya ndoa kwa kweli linakuwa UMEHARIBIWA MAISHA.
Ndio maana nikasema kabla ya ndoa UNAJIHARIBIA MAISHA MWENYEWE.

Nadhani umeelewa nasisitiza nini . . .
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Kikubwa ni jinsi ya kuepuka kudondokea kwenye mikono ya wanyang'anyi ili kuepuka kuona kwamba 'umeharibiwa' maisha:
a) Jitahidi kumjua mtu kwa undani zaidi kabla mapenzi hayajafika mbali - ni kweli hisia za mvuto zinaweza kuwa kubwa (kwa kisingizio cha love at first sight) na hii ndo imetengeneza waathirika wengi (kwa mtazamo wangu)
b) Kujaribu kuyajua mahitaji - wengi hapa wanakuwa na shida za kimwili ( tamaa, umaskini) au elimu n.k : Point ni kwamba; kutoruhusu mahitaji yatuzidi akili na uwezo wa kuamua kama jambo ni sahihi au sio sahihi kwa wakati huo
c)
d)
e)

....baadaye

Kwa kifupi hayo ndo maoni yangu

Kaka mpendwa nakubaliana na weye kabisa,
lakini hebu turudi nyuma tukiwa tunadadavua haya kwa,
kuangalia na context nzima ya maisha tuliyonayo kwa sasa,

Nowadays maisha yamebadilika sana, sijui ndo umagharibi wenyewe huu au vipi,
lakini maisha yanatupeleka kweli sisi viumbe,
ukiangalia unakuta sisi viumbe tuna haraka kweli katika kila jambo tunalolifanya,
either tukifikiri tumechelewa, au tunaogopa kuona jicho la jamii linatuonaje,
ndio maana utakuta binti mdogo tu lakini tayari ukifuatilia wakuta ashapita na mijibaba kumi si kidogo,
au kijana wa kiume, lakini tayari ameshatengezeza chain ndefu!

Na issue hii ya uharaka wetu sio katika mapenzi tu,
hata katika mazingira na majukumu mengine yanayotuhusu sisi viumbe......
Inafikia hatua unakuta inakuwa kama sifa kijana kutembea na mabinti wa aina tofauti...
au hata binti kutembea na waume za watu au wanaume tofauti na jamii ikaona ni sawa bila kuonyesha mshangao....
nadhani huku ndipo tulipofikia!!

Sasa issue ya kusema kupata muda wa kusomana tabia kabla hujajiingiza kwenye mahusiano,
kiukweli kuna wakati mimi inanichanganya sana, ukijaribu kuangalia jinsi mchakamchaka wa maisha ulivyo sasa,
na hayo mambo ya kimagharibi yalivyotutawala wallahi unabaki umechanganyikiwa tu.......
 
Mwj1...kwenye mapenzi kuna kitu utashi, ushawishi, mvuto, masikilizano na makubaliano.
Lazima, narudia tena,....Lazima kabla ya kufikia makubaliano yoyote kwenye maisha ya mapenzi na ndoa,
kila mmoja awajibike kuwa mkweli kwenye kutambua, kuchanganua na kufikia maamuzi ya nini kina heri na nini kina athari.

Mnapoamua watu wazima kuoana na kuanza maisha yenu ya pamoja, kuna mambo inabidi kujitolea muhanga ili kufanikisha malengo ya maisha. Compromises zipo...flexibility ni moja ya njia za kuweza mudu pale misuko suko itapojitokeza kwenye maisha.

Makubaliano ya mtaishi vipi, wapi,
lipi mtalipa priority, wakati gani nk yote ni katika kutafuta kuondosha ule u ndindindindi "mie nimesema thats it!" ....mtu yupo so rigid >>>Autocratic<<< Hitler yupo nyuma kwa hizo amri na 'kupelekeshwa!'...

Genesis (ufunuo 2:24) unasema
"This explains why a man leaves his father and mother and is joined to his wife, and the two are united into one."... Maisha yanapokuwa balanced sidhani kama kuna haja ya kuwa na hofu mwenza wako atakuharibia foundation na malengo ya maisha yako kama ulivyowekewa na familia na pia wewe mwenyewe ulivyokuwa umeyakusudia.

Ndio maana kwenye mwanzo wa Topik niliandika na nina quote;
WHAT DO YOU WANT IN LIFE? [/quote]
[SUP]Naamini kwenye hatua za awali kabisa za mapenzi, mkiwekana sawa katika hili, huko mbele ya safari ni kusahihisha
deviations zitazojitokeza au kuzibia viraka pale nytufa zitapoanza kujitokeza.

Ni muhimu kila mmoja kujitambua nini anataka maishani na kuwa muwazi kwa mwenza wake kuelezea malengo yake.
Ajuabu ya haya maisha yetu sie dunia ya tatu, wengi wetu tunasukumwa sukumwa tu, mtu unamuuliza nini malengo ya maisha yake , hana jibu! kisha siku ya siku anakwambia umemharibia maisha...ukimuuliza kivipi hana jibu!
[/SUP]

Mkuu, hata hilo la UKIMWI linaweza kuwa la kujitakia.
Likitokea ndani ya ndoa kwa kweli linakuwa UMEHARIBIWA MAISHA.
Ndio maana nikasema kabla ya ndoa UNAJIHARIBIA MAISHA MWENYEWE.

Nadhani umeelewa nasisitiza nini . . .
Ndoa its just papers watu mnaweza mkawa mnakaa pamoja mkitegemea kwamba future yenu mtakuwa pamoja.., kwahiyo ukitumia upendo wa mwenzako kwako kama silaha ya kuweza kumlaghai au kumpa matumaini ambayo hayapo.., au baadae baada ya kumpa mzigo ukakataa responsibilities... you are liable....

Si hivyo tu hata kwa mtu yoyote ambaye alikuwa kwenye mstari ulionyooka ila kwa company yako mbovu ukampelekea kupotoka utakua umechangia kuanguka kwake..., (therefore watu wote tuna-credit ya kujenga au kubomoa maisha ya wenzetu) si kwa mapenzi tu mfano mtu akija kwako kwa ushauri wa kibiashara ukamtapeli ukampelekea kukata tamaa ya maisha pia utakuwa umesababisha kuanguka kwake..., kwahiyo mkuu actions au ommissions zetu zinaweza zikasababisha heri au balaa kwa wenzetu
 
Mbu nimekusoma sawia kaka...zipo sacrifice ninakubali na ni wazi nitakuwa sawa kufanya hivyo kwa kuwa ni maamuzi yangu katika kuboresha ninachoamini ni kwa faida yangu/yetu.....kama ni mapenzi nitafanya ninachogomba mie ni ile hali ya nimefanya kwa hiyari afu m,ambo yakienda mrama nimnyooshee kidole eti amenioharibia maisha yangu kwa kuwa nilitoka nje ya malengo yanu ya maisha?!! Nilitoka kwa utashi wangu uliopatikana through makubaliano na maelewano yetu. nim Nilitoa maelezo hayo kwa kuangalia ile mtu eti anakuachisha kazi, kwa sababu iso na msingi kisa kaamua tu kwa kuwa yye ni 'Kichwa' cha nyumba basi anatakiwa asikilizwe, niache kazi kwa kumfurahisha yeye bna nafsi yake.pasipo makubaliano!! Akijanitema kusema kweli sitawezajisamehe kwa upuuzi huo!! yaani toil yooote ya wazazi kunisomesha, mie kusoma halafu bila makubaliano niache!! mwe hapo mtanisamehe kwa kweli!
 
ha ha ha, nyamayao bana...uliishi miezi tisa tumboni mwa mama yako, ukaishi miaka nenda rudi mpaka ulipokutana na huyo prince charming,...iweje uone maisha hayakuwa na thamani tena? huu UGONJWA MAPENZI NI BALAA...

Hebu leo miaka kadhaa ishapita jaribu kurudisha hisia zako siku ile ulipojiona maisha hayana thamani tena, kwanini ulifikiria hivyo?

Mbu my dear haya mambo yanategemea na umri bana lol, hebu na mimi nifunguke kidogo nisijifanye mgumu siwezi umizwa kumbe msururu wa matukio umri nao vinachangia,

Yaani kama asemavyo nyamayao mi naona hata yeye anaafadhali yaani mimi nasema kabisa kama sikufa kipindi kile basi walahi Yesu atanikuta hai hata kama ni kikongwe cha aina gani, ingawa sikumtishia mtu kujiua lakini nilikua natamani nife kabisa niiache hii dunia.

Ila sasa nikikumbuka huwa najicheka kabisa mwenyewe na kujiuliza sa nini kilikuwa kinanisumbua? mbona maisha sasa ni mazuri kuliko kipindi kile? ila ndio hivyo tena kuna umri kujitambua ni ngumu sana asee. Sasa hivi huwa namshangaa eti we ma fulani nionjeshe basi nimekukumbuka mi mzazi mwenzio, yaani namshangaaga sana asee, ni kipi nilichobadilika sasa? Sana sana kwa hasira lakini za moyoni namwambia embu acha hizo naomba hela ya pampas za mtoto alizonazo zinambana na kutaja kiasi kilichoshiba ili nikapunguzie hasira hata kwa kunywea bia tu. Na yeye kwa ujinga wake anatoa wakati litoto lina miaka kumi huku akidhani ananivuta akiwa na matumaini ipo siku huyu mama atanionjesha lol.

So kuna umri mtu mapenzi yakikuumiza unatamani kufa kabisa na hili wengi wetu tumepitia ila kwa sababu sasa hivi umri umeenda tunajifanya hatujawahi umizwa mwe!
 
hahahaah Maty, una balaa wewe, nimecheka kwa nguvu zote, hawa viumbe wana tabu sana, mie ndio ananiambiaga nilikuwa chaguo lake kuwa mke sema shetani tu alimpitia nimpe muda tuongee kidogo aweze kunielezea kilihotokea, yaani namuonaga kama kituko hivi na anshukurugi sana sana alinitenda coz sasa hivi ningekuwa na maisha ya ajabu kama alivyo yeye kwa sasa.
 
Nyie viumbe wawili msinichekeshe ah........yaani maty kuwa Yesu atarudi akukute hai!!! hahahahah

hawa viumbe hadithi jamani acheni................ mie kuna mmoja hapa juzi kati anantafuta eti anaomba 'tuibie' ili apate furaha aliyoipoteza miaka hiyo. Eti mwenza wake wa sasa anam'nyanyasa' yaani najichekea tu hapa kwa masikitiko............anasahau muda wa kulidanganya hili liMwanajamiiOne ushapita looong!
 
Kweli kabisa mpenzi wakipata vimeo huko ndio kutukumbukaga, kipindi kile nilikuwaje halafu sasa nimebadilika lol. Mi ndio huwa namkomeshaga kweli akishaanza habari zake oooh unajua we bado mke wangu tu, tuna mtoto na nini unafikiri nakasirika (maana mwingine angeanza ukome, si uliniacha sa hizi ndio unaniona mzuri?)

Hapana mi nnajifanya najichekesha kumbe langu rohoni halafu kesho yake naanza eeee unajua ba fulani mtoto hana skintaiti na halafu zimepanda kweli moja 50,000/= anahitaji tatu ili abadilishe badilishe yaani naongeza mahitaji kibao kuliko maelezo na yeye anatoa tu.

kwani huko aliko ashaumizwa na anaendelea kuumizwa, akinikumbuka tu namgea kibomu na hapindui na mimi nishamsoma udhaifu wake ukiona anakutafuta ujue yamemzidi na mimi hapo hapo kurudishia machungu aliyonipaga. yeye kwa upande wake anadhani akifanya hivyo ipo siku nitamkubalia hata awe mpenzi wa siri pole yake hajui ujanja ndio yeye mwenyewe kanifundisha baada ya kunikomaza kabla ya umri.

Hope haingiagi Jf lol, hakyanani
 
mie langu lilioa mara mbili na kuacha, sasa hivi yupo yupo tu madai yake ananisubiria nije kuwa mke wake ndio aliyeandikiwa, hahahah atasubiri sana, juzi juzi tena kaniboa kweli kanitumia na pics kibao za enzi zile tulivyokuwa wapenzi, yaani nilikereka kweli...
 
Umeona eee mamy? umeona hawa viumbe walivyo wapuuzi (mtanisamehe sio wote lol) eti uanze tu kuiba kilichowahi kuwa chako phewwww lol. Na kwa ujinga wake anadhani wewe ni yule yule aliewahi kukudanganya enzi hizo, hehehehehe huyu wangu pole yake kabisa asee, tunavyodanganyishiana hadi raha.

Mwanajamii walahi yesu atanikuta, maana hakuna ambalo linanistua sasa hata itokee nini najua tu litapita kama mengine yalivyopita. Halafu Mbu hii thread ilipofikia nitashindwa kumalizia kazi zangu ifunge kwa muda bana lol
 
Mbu nimekusoma sawia kaka...zipo sacrifice ninakubali na ni wazi nitakuwa sawa kufanya hivyo kwa kuwa ni maamuzi yangu katika kuboresha ninachoamini ni kwa faida yangu/yetu.....kama ni mapenzi nitafanya ninachogomba mie ni ile hali ya nimefanya kwa hiyari afu m,ambo yakienda mrama nimnyooshee kidole eti amenioharibia maisha yangu kwa kuwa nilitoka nje ya malengo yanu ya maisha?!! Nilitoka kwa utashi wangu uliopatikana through makubaliano na maelewano yetu. nim Nilitoa maelezo hayo kwa kuangalia ile mtu eti anakuachisha kazi, kwa sababu iso na msingi kisa kaamua tu kwa kuwa yye ni 'Kichwa' cha nyumba basi anatakiwa asikilizwe, niache kazi kwa kumfurahisha yeye bna nafsi yake.pasipo makubaliano!! Akijanitema kusema kweli sitawezajisamehe kwa upuuzi huo!! yaani toil yooote ya wazazi kunisomesha, mie kusoma halafu bila makubaliano niache!! mwe hapo mtanisamehe kwa kweli!

mnh, hiyo kaka hiyo wataka n'nyima nini?
nikishaizoea na shikamoo nitakudai! LOL...."Usijeniharibia maisha!"

Mwj1, maisha ni vile wewe unataka yawe, matokeo ya maisha ni vile ulivyochagua hapo awali!
Hilo la mume kung'ang'ana eti uache kazi kwakuwa yeye hataki, mimi nalipinga kwa nguvu zote!
Hainiingii akilini eti uache kazi, ili iweje?

Hata kama ni yeye kakuunganishia, hata kama ni yeye aliyekushawishi, hata kama amekukuta tayari
waifanya hiyo kazi,...hakuna justification yeyote bana itayoniingia akilini mtu aache kazi yake kumfurahisha mwenziwe.
"Ukipenda boga,....!".... ila kuna zile exceptions...mfano mke anafanya kazi za ajabu ajabu kama stripper/dancer wa hizi bendi za muziki/nk hapo sitamlaumu mtu anayekusudia kuokoa ndoa yake na majaribu ya shetani..

Lakini nimekukuta Mwj1 na jembe lako mkononi, halafu nikulazimishje uache kilimo kwanza? Huh...utakuwa wazimu huo. Mie ndio kwanza nitakununulia mbegu bora na mbolea ili tufanikishe mavuno zaidi.
Haya mambo ya acha kazi ukae nyumbani mwishowe huzua "unalala lala tu hapa, unasubiri uletewe kama Golikipa!"
This Scenario cuts both ways!....namwogopa sana mwanamke ambaye baada ya kuolewa eti naye anaamua kuacha kazi,
na kuamua kuwa full time house wife....kisa? eti apate kumhudumia vizuri mumewe!

Lakini nawe mpaka ukakubali ushawishi huo, mnh! Ama kweli kuishi kwingi ni kuona mengi...
Uwe na amani.
 
Mbu my dear haya mambo yanategemea na umri bana lol, hebu na mimi nifunguke kidogo nisijifanye mgumu siwezi umizwa kumbe msururu wa matukio umri nao vinachangia,

Yaani kama asemavyo nyamayao mi naona hata yeye anaafadhali yaani mimi nasema kabisa kama sikufa kipindi kile basi walahi Yesu atanikuta hai hata kama ni kikongwe cha aina gani, ingawa sikumtishia mtu kujiua lakini nilikua natamani nife kabisa niiache hii dunia.

Ila sasa nikikumbuka huwa najicheka kabisa mwenyewe na kujiuliza sa nini kilikuwa kinanisumbua? mbona maisha sasa ni mazuri kuliko kipindi kile? ila ndio hivyo tena kuna umri kujitambua ni ngumu sana asee. Sasa hivi huwa namshangaa eti we ma fulani nionjeshe basi nimekukumbuka mi mzazi mwenzio, yaani namshangaaga sana asee, ni kipi nilichobadilika sasa? Sana sana kwa hasira lakini za moyoni namwambia embu acha hizo naomba hela ya pampas za mtoto alizonazo zinambana na kutaja kiasi kilichoshiba ili nikapunguzie hasira hata kwa kunywea bia tu. Na yeye kwa ujinga wake anatoa wakati litoto lina miaka kumi huku akidhani ananivuta akiwa na matumaini ipo siku huyu mama atanionjesha lol.

So kuna umri mtu mapenzi yakikuumiza unatamani kufa kabisa na hili wengi wetu tumepitia ila kwa sababu sasa hivi umri umeenda tunajifanya hatujawahi umizwa mwe!

khaaaa? hhhaaa hha hhaaa! ama wajinga ndio waliwao...Maty acha 'kumharibia' mwenzio maisha bana, mtoto amekua huyo!
Au ndio anaziba nyufa?....
 
Hahaha mbu hana haya huyu mwanaume mwenzio alishaniharibia kwanza (yale yaleeeeeeee lol) usicheke.

Sa sasa hivi ananitafuta ni mwana wa mwenzie lol, ingekua ndio enzi zile ningesema anataka kuniharibia kwa mara ya pili lol. Sasa huyu si ananifanya mi mjinga jameni, hivi ananichukuliaje? Ndio hivyo na mi namgeuza mjinga twende kazi
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Wapo humu humu,wanajilizaliza na kukamuliwa hao mpaka mafua lakini wakiingia hapa unafikiri wanasemaga.

Kweli kabisa mpenzi wakipata vimeo huko ndio kutukumbukaga, kipindi kile nilikuwaje halafu sasa nimebadilika lol. Mi ndio huwa namkomeshaga kweli akishaanza habari zake oooh unajua we bado mke wangu tu, tuna mtoto na nini unafikiri nakasirika (maana mwingine angeanza ukome, si uliniacha sa hizi ndio unaniona mzuri?)

Hapana mi nnajifanya najichekesha kumbe langu rohoni halafu kesho yake naanza eeee unajua ba fulani mtoto hana skintaiti na halafu zimepanda kweli moja 50,000/= anahitaji tatu ili abadilishe badilishe yaani naongeza mahitaji kibao kuliko maelezo na yeye anatoa tu.

kwani huko aliko ashaumizwa na anaendelea kuumizwa, akinikumbuka tu namgea kibomu na hapindui na mimi nishamsoma udhaifu wake ukiona anakutafuta ujue yamemzidi na mimi hapo hapo kurudishia machungu aliyonipaga. yeye kwa upande wake anadhani akifanya hivyo ipo siku nitamkubalia hata awe mpenzi wa siri pole yake hajui ujanja ndio yeye mwenyewe kanifundisha baada ya kunikomaza kabla ya umri.

Hope haingiagi Jf lol, hakyanani
 
mie langu lilioa mara mbili na kuacha, sasa hivi yupo yupo tu madai yake ananisubiria nije kuwa mke wake ndio aliyeandikiwa, hahahah atasubiri sana, juzi juzi tena kaniboa kweli kanitumia na pics kibao za enzi zile tulivyokuwa wapenzi, yaani nilikereka kweli...

Umeona eee mamy? umeona hawa viumbe walivyo wapuuzi (mtanisamehe sio wote lol) eti uanze tu kuiba kilichowahi kuwa chako phewwww lol. Na kwa ujinga wake anadhani wewe ni yule yule aliewahi kukudanganya enzi hizo, hehehehehe huyu wangu pole yake kabisa asee, tunavyodanganyishiana hadi raha.

Mwanajamii walahi yesu atanikuta, maana hakuna ambalo linanistua sasa hata itokee nini najua tu litapita kama mengine yalivyopita. Halafu Mbu hii thread ilipofikia nitashindwa kumalizia kazi zangu ifunge kwa muda bana lol

.........hahahaah nyiew abeijing hebu punguzeni ukali kidogo ah........ni vema kuwashukuru kwa kutupitisha huko tulikopita maana wametusaidia kuwa wakomavu, waelewa na 'wakubwa' kusema ukweli mie ninamshukuru sana na nilimwambia kabisa kuwa yaani ninamshukuru sana kwa alivyoni'kuza' na nina uhakika hata huyu niliyenaye kwa sasa anatamani kumshukuru kwa kum'lelea' na kum'fundia' maana nimepikika haswa!

So sidhani kama tunapaswa kuwachukia kiasi hiki loh............nyamayao kama nakuona unavyoachia msonyo wakati unaangalia hizo picha.... ah ulivuta hisia??
 
hahahaah Maty, una balaa wewe, nimecheka kwa nguvu zote, hawa viumbe wana tabu sana, mie ndio ananiambiaga nilikuwa chaguo lake kuwa mke sema shetani tu alimpitia nimpe muda tuongee kidogo aweze kunielezea kilihotokea, yaani namuonaga kama kituko hivi na anshukurugi sana sana alinitenda coz sasa hivi ningekuwa na maisha ya ajabu kama alivyo yeye kwa sasa.
Nyie viumbe wawili msinichekeshe ah........yaani maty kuwa Yesu atarudi akukute hai!!! hahahahah

hawa viumbe hadithi jamani acheni................ mie kuna mmoja hapa juzi kati anantafuta eti anaomba 'tuibie' ili apate furaha aliyoipoteza miaka hiyo. Eti mwenza wake wa sasa anam'nyanyasa' yaani najichekea tu hapa kwa masikitiko............anasahau muda wa kulidanganya hili liMwanajamiiOne ushapita looong!
mie langu lilioa mara mbili na kuacha, sasa hivi yupo yupo tu madai yake ananisubiria nije kuwa mke wake ndio aliyeandikiwa, hahahah atasubiri sana, juzi juzi tena kaniboa kweli kanitumia na pics kibao za enzi zile tulivyokuwa wapenzi, yaani nilikereka kweli...
Hahaha mbu hana haya huyu mwanaume mwenzio alishaniharibia kwanza (yale yaleeeeeeee lol) usicheke.

Sa sasa hivi ananitafuta ni mwana wa mwenzie lol, ingekua ndio enzi zile ningesema anataka kuniharibia kwa mara ya pili lol. Sasa huyu si ananifanya mi mjinga jameni, hivi ananichukuliaje? Ndio hivyo na mi namgeuza mjinga twende kazi

...HHAHHHAAA! ...Nyie watatu mshakutana hapa hapatoshi tena, acha nisogeze kiti pembeni,
namuachia chaki na ubao Mwj1 aendeleze hili darasa....acha nicheke tu hayo mnayoyasema maana mnh!

Kwakweli maisha haya, aheri yangu niliyejifunza "...aheri kivuli kinifuate badala ya kukifuata kivuli!"
 
mnh, hiyo kaka hiyo wataka n'nyima nini?
nikishaizoea na shikamoo nitakudai! LOL...."Usijeniharibia maisha!"

hahahahaha we Mbu bwana mie sijazoea bado lol....sijui ndo nidai kitchen party lol
Mwj1, maisha ni vile wewe unataka yawe, matokeo ya maisha ni vile ulivyochagua hapo awali!
Hilo la mume kung'ang'ana eti uache kazi kwakuwa yeye hataki, mimi nalipinga kwa nguvu zote!
Hainiingii akilini eti uache kazi, ili iweje?

Hata kama ni yeye kakuunganishia, hata kama ni yeye aliyekushawishi, hata kama amekukuta tayari
waifanya hiyo kazi,...hakuna justification yeyote bana itayoniingia akilini mtu aache kazi yake kumfurahisha mwenziwe.
"Ukipenda boga,....!".... ila kuna zile exceptions...mfano mke anafanya kazi za ajabu ajabu kama stripper/dancer wa hizi bendi za muziki/nk hapo sitamlaumu mtu anayekusudia kuokoa ndoa yake na majaribu ya shetani..

Lakini nimekukuta Mwj1 na jembe lako mkononi, halafu nikulazimishje uache kilimo kwanza? Huh...utakuwa wazimu huo. Mie ndio kwanza nitakununulia mbegu bora na mbolea ili tufanikishe mavuno zaidi.
Haya mambo ya acha kazi ukae nyumbani mwishowe huzua "unalala lala tu hapa, unasubiri uletewe kama Golikipa!"
This Scenario cuts both ways!....namwogopa sana mwanamke ambaye baada ya kuolewa eti naye anaamua kuacha kazi,
na kuamua kuwa full time house wife....kisa? eti apate kumhudumia vizuri mumewe!

Lakini nawe mpaka ukakubali ushawishi huo, mnh! Ama kweli kuishi kwingi ni kuona mengi...
Uwe na amani.

Yes Mbu kuna situation na situation aisee nakubali.

Itabidi nitafute automatiki Icon ambayo itadetect kama ninapost kwa kukuadress basi yenyewe iwe inarekebisha mambo......nikiandika kaka yenyewe inaweka Honeypie!!
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
...HHAHHHAAA! ...Nyie watatu mshakutana hapa hapatoshi tena, acha nisogeze kiti pembeni,
namuachia chaki na ubao Mwj1 aendeleze hili darasa....acha nicheke tu hayo mnayoyasema maana mnh!

Kwakweli maisha haya, aheri yangu niliyejifunza "...kivuli kinifuate badala ya kukifuata kivuli!"
Eh umeyachokoa haya maskeletoni yetu afu wakaa pembeni ukiangalia yanavyojikinga baridi?? una visa weye .............
hahah kusema kweli maisha matamu sana nikikumbuka nlivyotaka kujiua kwa kunywa bia tatu kali loh.......(ilikuwa mara yangu ya kwanza) sijui nani alinidanganya bia yaua ah!!
 
.........hahahaah nyiew abeijing hebu punguzeni ukali kidogo ah........ni vema kuwashukuru kwa kutupitisha huko tulikopita maana wametusaidia kuwa wakomavu, waelewa na 'wakubwa' kusema ukweli mie ninamshukuru sana na nilimwambia kabisa kuwa yaani ninamshukuru sana kwa alivyoni'kuza' na nina uhakika hata huyu niliyenaye kwa sasa anatamani kumshukuru kwa kum'lelea' na kum'fundia' maana nimepikika haswa!

So sidhani kama tunapaswa kuwachukia kiasi hiki loh............nyamayao kama nakuona unavyoachia msonyo wakati unaangalia hizo picha.... ah ulivuta hisia??

ila ni kweli mamito, to be frank huwa namshukuru sana sana tena sana kwani amenipika nikapikika, kwa kweli bila kunifanyia yale sidhani ningekuwa mwanamke mwenye msimamo kama ambao nilio nao sasa, mimi kwa sasa mtu akinidanganya ujue nimependa mwenyewe, kwa kweli kwa hilo namshukuru.

Ila anachoniudhigi ni hichi cha kutaka kunifanya mimi kiburudisho chake cha pembeni, kukuona umependeza basi kosa tamaa inamwakaje? hapo bwana huwa ananikera kuliko maelezo na mimi kukereka kwangu huwa sikuonyeshi kwa maneno bali kwa vitendo.
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Back
Top Bottom