Kikubwa ni jinsi ya kuepuka kudondokea kwenye mikono ya wanyang'anyi ili kuepuka kuona kwamba 'umeharibiwa' maisha:
a) Jitahidi kumjua mtu kwa undani zaidi kabla mapenzi hayajafika mbali - ni kweli hisia za mvuto zinaweza kuwa kubwa (kwa kisingizio cha love at first sight) na hii ndo imetengeneza waathirika wengi (kwa mtazamo wangu)
b) Kujaribu kuyajua mahitaji - wengi hapa wanakuwa na shida za kimwili ( tamaa, umaskini) au elimu n.k : Point ni kwamba; kutoruhusu mahitaji yatuzidi akili na uwezo wa kuamua kama jambo ni sahihi au sio sahihi kwa wakati huo
c)
d)
e)
....baadaye
Kwa kifupi hayo ndo maoni yangu
Kaka mpendwa nakubaliana na weye kabisa,
lakini hebu turudi nyuma tukiwa tunadadavua haya kwa,
kuangalia na context nzima ya maisha tuliyonayo kwa sasa,
Nowadays maisha yamebadilika sana, sijui ndo umagharibi wenyewe huu au vipi,
lakini maisha yanatupeleka kweli sisi viumbe,
ukiangalia unakuta sisi viumbe tuna haraka kweli katika kila jambo tunalolifanya,
either tukifikiri tumechelewa, au tunaogopa kuona jicho la jamii linatuonaje,
ndio maana utakuta binti mdogo tu lakini tayari ukifuatilia wakuta ashapita na mijibaba kumi si kidogo,
au kijana wa kiume, lakini tayari ameshatengezeza chain ndefu!
Na issue hii ya uharaka wetu sio katika mapenzi tu,
hata katika mazingira na majukumu mengine yanayotuhusu sisi viumbe......
Inafikia hatua unakuta inakuwa kama sifa kijana kutembea na mabinti wa aina tofauti...
au hata binti kutembea na waume za watu au wanaume tofauti na jamii ikaona ni sawa bila kuonyesha mshangao....
nadhani huku ndipo tulipofikia!!
Sasa issue ya kusema kupata muda wa kusomana tabia kabla hujajiingiza kwenye mahusiano,
kiukweli kuna wakati mimi inanichanganya sana, ukijaribu kuangalia jinsi mchakamchaka wa maisha ulivyo sasa,
na hayo mambo ya kimagharibi yalivyotutawala wallahi unabaki umechanganyikiwa tu.......