Godfrey- denis
Member
- Aug 26, 2022
- 64
- 124
Sekta ya Bank inazidi kukua.
Takwimu za nusu ya kwanza ya mwaka 2025 zinaonesha picha nzuri sana kwa sekta ya benki nchini. Benki za biashara zimepata jumla ya faida ya Sh1.2 trilioni, ongezeko la 9% ukilinganisha na Sh1.09 trilioni kipindi kama hicho mwaka 2024. Ukuaji huu umechochewa na mapato mazuri kutoka kwenye vyanzo vya riba na visivyo vya riba.
Vinara wa soko – CRDB na NMB zimeendelea kuonesha ubora wao:
■ NMB Bank: Faida ya Sh358.57 bilioni (+14%)
■ CRDB Bank: Faida ya Sh346.45 bilioni (+26%)
Lakini si hao pekee — hata benki nyingine zilizo kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) kama Mkombozi Commercial Bank na Maendeleo Bank zimeanza kuonesha ukuaji wa kuvutia.
📈 Matarajio ya ukuaji zaidi:
Sekta inatarajiwa kuendelea kupaa kwa kuboresha mikopo na kupunguza mikopo chechefu (Non-Performing Loans) chini ya 5%, sambamba na kuongeza ufanisi wa uendeshaji ili kuhakikisha uwiano wa gharama za uendeshaji na mapato (Cost to Income Ratio, CIR) unabaki chini ya 55% kama ilivyoelekezwa na Benki Kuu.
Kwa hali hii, hakika yajayo yanafurahisha kwa sekta ya fedha na uwekezaji nchini. Huu ni muda mzuri kwa wawekezaji na wananchi kufuatilia kwa karibu mwenendo wa sekta hii yenye mchango mkubwa katika uchumi wa taifa.
Je wewe umenunua hisa benki yoyote kwenye soko la hisa la Dar es Salaam?
Tujuze kwenye comment