1 Nimejifunza kwamba kumsubiri Yesu aje akukute ukiwa hai na akakutwaa ni jambo jema na Imani nzuri, Ila jua unaweza kuzeeka na ukafa hajarudi Ila wewe ndie umemfuata huko. Kwa hiyo jambo la muhimu Ni kujiweka tayari hata ukifa uwe mmoja wa watakaofufuliwa kuingia uzima na milele. Mimi nikiwa kijana nilijua angerudi mapema tu ila Sasa Nina miaka 70 bado hajarudi, labda nitakufa na hajaja.
2. Nimejifunza kwamba aliyedhulumiwa lazima atashinda japo inawezakuwa baada ya muda mwingi kupita, lakini haki yake haitapotea kamwrme
3. Nimejifunza kwamba Ni ngumu sana mtu kukupiga kofi umgeuzie lingine....nadhani Kuna maana ingine isiyo hiyo.
4. Nimejifunza? kwamba maisha yanaweza kumalizika wakati wowote huku tukiwa hatujatimiza ndoto zetu hata robo.....Mtu aliyempokea Yesu lazima atimize kusudi kwa sehemu kubwa.
5. Nimejifunza kwamba maneno matamu na uso wenye bashasha na ukarimu ni afya njema sana kwa mtu Ila uso uliokunjamana na hasira hupunguza sana siku za mtu.
6. Nimejifunza kwamba tajiri mkubwa kuliko matajiri wote duniani ni yule ambaye anamiliki afya na amani.
7. Nimejifunza Chochote kinaweza kutolea muda wowote ule kwahyo nipunguzie mategemeo