Somo kubwa nililopata ni kuwa ili upate mafanikio uwe tofauti na wetu wengine hasa kiuchumi ni lazima upitie mateso kweli kweli hadi hatua ya kupoteza matumaini vinginevyo wazazi wako waliteseka sana kuandaa future zao na watoto wao na wakati wako wa kuteseka teseka we mwenyewe usitake kuwashirikisha watu wengine mateso yako kwani hata wao mpaka unaona wanamafanikio na wanakula bata waliteseka tena sana.Nashukuru maisha mapya baada ya kula msoto wa kutosha mambo yameanza kufunguka najiona kweli nipo tofauti na nilipotoka na ninaimani watoto wangu hawatakula msoto kivile sababu baba yao kikombe nilikibeba na njia nimewatengenezea.