Nani mnufaika wa machapisho yako?
Unapoweka chapisho mtandaoni Kuna vigezo unaviangalia?, Nani mlengwa mkuu wa machapisho yako? Je, Chapisho lako linalenga umri wa mnufaika/Msomaji au linajikita zaidi katika jinsi mfano (ke/me).Yote yanaweza kuwa majibu, Machapisho unayoweka mtandaoni mnufaika anweza kuwa mtoto wako,Baba yako au mtu baki,na watu wengi kwa ujumla. Mfano Mimi binafsi nilivutiwa na mijadala mbalimbali ndani ya Jamiiforum Kupitia Majukwaa yake hasa la Siasa,MMU na kadhalika. Vijana wa chichat,Siasani na kwingineko nawapa heko kwa kuchochote mijadala mbalimbali inayo hamasisha watu kujiunga na Jamiiforum.
Je, Unanufaikaje na mitandao ya kijamii?
Mitandao ya kijamii inaweza kuwa na manufaa yafuatayo endapo itatumika ipasavyo;- Kukutana na Marafiki mfano Facebook, Jamiiforum n.k
- Kuuza ujuzi wako mfano LinkedIn
- Kushiriki mijadala mbalimbali yenye lengo la kuchochea maendeleo ya kisiasa,kijamii na kiuchumi mfano Jamiiforum imetoa jukwaa ambayo imeongeza uwajibikaji katika serikali na sekta binafsi.
- Kutangaza bidhaa Mbalimbali, mitandao ya kijamii imetoa mwanya watu kutangaza bidhaa zao mfano jukwaa la matangazo Jamiiforum , Facebook n.k
- Kutafuta taarifa mbalimbali mfano taarifa zinazohusu Teknolojia,Siasa,Elimu,Muziki,Michezo,Utalii n.k.
- Kutafuta Mwenza au Mchumba. Dunia ya Sasa umekuwa ndani ya kiganja inakuwezesha kukutana na mtu yeyote kutoka Kona yoyote ndani ya Dunia. Mfano jukwaa la Love connect lililopo Jamiiforum.
Je, Ni zipi athari zinazoweza kujitoketa endapo utatumia mitandao ya kijamii?
Mitandao ya kijamii inaweza kuwa na athari mbalimbali kwa mtumiaji mmoja mmoja na jamii kwa ujumla;- Uraibu uliopitiliza wa matumizi ya mitandao ya kijamii hupelekea Msongo wa mawazo. Jamii inapaswa ielewe matatizo ya akili yameongezeka na kichocheo kimojawapo kinaweza kuwa mitandao ya kijamii. Mfano uvujaji wa picha au video za faragha(siku hizi huitwa connection) hupelekea baadhi ya watu kuona wametengwa na Dunia pale wanaposhambuliwa kwenye mitandao ya kijamii.
- Wizi wa mitandaoni(Scams) umeongezeka. Jamii inapaswa ichukukue tahadhari pale mtu/watu wanapotembelea link asiyo na taarifa nayo au kuombwa taarifa zao katika mitandao ya kijamii. Kwani wezi wa mitandaoni nao ni wabunifu,kutokuwa makini utajikuta unapoteza Pesa na taarifa zako kuvuja mitandaoni.
- Bullying (Kudhalilishwa). Je umejiandaaje kisaikolojia kukabilia na vitendo vya Kudhalilishwa mtandaoni?,Unaweza kuhimili? .Muda wote unapaswa kuwa umejiandaa kisaikolojia maana mashambulio ya mitandaoni wakati mwingine hupelekea kujitoa uhai.
- Kupunguza morali ya kazi. Mitandao ya kijamii isipotumiwa kwa kiasi hupunguza Hali ya utendaji wa kazi, kwani ufanisi unaposhuka hupunguza uzalishaji na kipato cha muhusikia.
- Udukuzi, Je,taarifa zako ziko salama wakati wote?.Ili kuepukana na udukuzi usitoe taarifa zako Kama email ,password ili account yako isidukuliwe.
- Mitandao ya kijamii imeifanya Karne ya Sasa watu watafute ukamilifu(Perfection) kwa kujiongezea au kupunguza sehemu za miili ya yao kwa kuonekana Bora au kuvutia zaidi.
Mtu Kama Kim Kardashian(mwanamitindo na mjasiliamali) amefanya wanawake wa kileo wapigane kupata mionekano mizuri wenyewe wanaita "body goals" bila kujali athari zake
Je, hatua gani za kuchukua kukabiliana na Athari zitokanozo na mitandao ya kijamii?
Ili kuepuka/kupunguza athari zitokano na mitandao ya kijamii huna budi kufanya yafuatayo;- Kutobonyeza link ambayo huna uwakika nayo Hadi pale utapojihakikishia usalama wake. Kwani kwa kufanya hivyo unakuwa umeepukana na Athari ambazo zingekupata Kama udukuzi wa taarifa zako au kutapeliwa.
- Kutoa taarifa kwa mtandao husika pale unapohisi taarifa zako haziko salama, au unapofanyiwa bullying.
- Ku Log out pale unapochangia kifaa Cha kuingilia mtandaoni mfano simu au kompyuta. Hiii itakupunguzia taarifa zako kutovuja.
- Kuomba ushauri wa wataalmu pale unapoona huna ujuzi napo hasa masuala ya Teknolojia.
- Elimu, jielimishe kabla haujajiunga na mtando wa kijamii.
Je, Sheria ya mtandaoni imeongeza au imepunguza Nini kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii?
Ilichoongeza
Sheria imetukumbusha tusiitumie mitandao ya kijamii vibaya, kwani kw kuchapisha maudhui ya "kichochezi" unaweza kukutana la rungu la sheria ambayo faini inaweza kuwa milioni tatu au zaidi au kifungo gerezani.Ilichopunguza
- Imeshusha morali ya wachangiaji kwa kuhofia kutiwa nguvuni na vyombo vya dola.
- Imekimbiza mijadala yenye tija amabo ilikuwa na lengo kuiwajibisha serikali na kuchochea maendeleo ya nchi .
- Imejenga woga miongoni mwa watumiaji wa mitandao ya kijamii. Watu wako tayari kuchangia habari za udaku,Michezo na sio Siasa kwa kuhofia mkono wa dola.
Hii ni Baadhi ya mitandao ya kijamii kwa uchache;
- JamiiForums
- Snapchat
- Quora
- YouTube
- Tik Tok
- Viber
- Telegram
- Badoo
- Myspace
- Xanga
- Clubhouse
- Sportfy live
- Line
- Tribe
- Vero
Kuna ulazima wa kujiunga na mtandao zaidi ya mmoja?
Jibu ni ndio/hapana kutegemea na matumizi ya muhusika, unaweza kutumia mitandao tofauti kuwafikia walengwa tofauti tofauti kwa kuwa na account zaidi ya moja.Teknolojia imewezesha simu zetu kuweza kuweka application mbali mbali mfano Instagram, Facebook,jamii, Snapchat, telegram n.k hii imerahisisha matumizi zaidi.
Pia, Mitandao ya kijamii kwa kiasi kikubwa inamatumizi yanayo fanana, sio lazima uwe na Account nyingi za Mitandao tofauti ndio uwe wa kileo. Unapaswa uwe na na ile ambayo una matumizi nayo au ile inayohusisha Shughuri zako za kila siku, mfano WhatsApp, YouTube , jamiiforum n.k
Maswali mengine ninayojiuliza kuhusu mitandao ya kijamii?
- Je, nini kesho (future) ya mitandao ya kijamii, kutakuwa na teknojia kubwa zaidi ya hii kuhusu mitandao ya kijamii. Evolution yake iko vipi? Kuna mitandao itakufa au ataibuka mbabe wa mmoja na kumeza wote?, Maswali Ni meng hapa.
- Je, mitandao ya kijamii imetusaulisha au Ni hamasa kwa mazingira yetu,mfano suala zima la tabia ya nchi. Ipi nafasi ya mitandao ya kijamii hapa?, je, Ni mbwa anaebweka bila vitendo?.
Karibuni kwa mjadala.
Upvote
26