AmKATRINA
JF-Expert Member
- Jul 27, 2012
- 1,020
- 2,422
Je, ulishawahi kujiuliza msichana wenu wa kazi wa kipindi hiko yuko wapi na anafanya nini?
Habari zenu wapendwa wana Jf na guests mnaosoma kimya kimya.
Ulishawahi kujiuliza hili swali?
Yuko wapi,
Yu hai au alifariki?
Je, kama ana watoto....huwa anakuja kuwatembelea siku moja moja?
Najua wengi wetu huwa tunawapuuza dada zetu hawa kwani wanakuwa wameshaondoka katika familia zetu na kuanza maisha yao sehemu ingine.
Dada aliyekulea tangu ukiwa una mwaka 1 mpaka unafikisha miaka 10 au 20 n.k unajua alipo?
Alikulea kwa upendo.
Alikupikia, alikufulia nguo zako za shule na za nyumbani, mlicheza pamoja.
Alikuwa anajua ratiba yako ya wiki nzima na anahakikisha anaifuata.
Kuna wadada wengine wa kazi walikuwa ni zaidi ya wazazi kuanzia kwenye upendo mpaka kwenye malezi.
Hata mzazi wako usipomuona siku 3 (kutokana na majukumu ya kazi), dada wa kazi alikuwa mstari wa mbele katika kukulinda na kukutunza.
Kuna zile familia ambazo baba na mama wanaondoka kwenda kazini alfariji sana watoto wakiwa wamelala na wanarudi usiku mkubwa watoto wakiwa wamelala pia, je, hapo umuhimu wa dada wa kazi bado hujauona?
Siku unaamka asubuhi, unakuta dada yako aliyezoea kukuamsha asubuhi, kukuogesha, kukunyooshea nguo na kukupeleka shule hayupo,....lazima ujiulize.
Najua haina umuhimu sana, ila leo nimekaa na kuwaza hili jambo.
Nawakumbuka:
1. Dada Mwajuma....alinilea tangu mama yangu kanizaa mpaka natimiza miaka 8 (huyu alishatangulia mbele ya haki, aendelee kupumzika kwa amani)
2. Dada Gerite miaka 8 mpaka 13 (ana familia yake)
3. Na dada Asha miaka 14 mpaka 18 (nachati nae sana Fb, yuko na familia yake na mumewe na watoto)
Mungu awatunze na muendelee kuwa wamama bora kwa waume zenu na watoto wenu kwa maana mlitulea vyema.