Umeshawahi kujiuliza wewe ni nani?

Umeshawahi kujiuliza wewe ni nani?

Kama wewe ni mimi na mimi ni wewe mbona linapokuja suala la kufurahi hatufurahi wote au kuumia hatuumii wote?

Au ni nini kinatenganisha matendo haya?
 
Sijaongezea nimeuliza tu maana hata mtu akifa mwili unabaki kuwa wa marehemu. Sasa huyo marehemu unakuta yuko wapi hadi asahau nyumba yake ambayo ndio mwili.
Hahahahahahahahaaaaaaa aiseee jamaaa u made my day!
 
Mhh sasa unaponitenganisha na mwili,mawazo yangu jinsia nk wakati ndio mimi huyo unategemea ubaki na nini
Wewe is a unique combination of everything that u are
 
Hiyo ni Yoga meditation steps.
Naona wameshamchanganya huyu. Nimetembelea mataifa mengi yanayofanya hiyo kitu naona wao wanafanya na Budha akiwa mbele.
Hata hapa hotelini Champ De lamar, Port Luis, Mauritis naona sanamu ya Budha.
Asante mkuu tupo pamoja hii ni moja ya safari kubwa za kiroho ambazo kwa namna ya kipekee ukifunzu shule ya wanga uliotukuka unaipitia hapo utaambia ufanye madoido ya aina yake ya kutoa ''ruuhaw" (hebrew word) roho au pumzi yako ubakie mtupu pengine ili shetani apate kiti ndani yako huku wewe ukipepea huku na huko humo(too and fro)rejea majibu ya shetani kwa swali la Mungu katika biblia kitabu cha Ayubu 1...Aina hii ya ibada ilikuwepo mashariki karibu na malango ya bustani ya edeni yakijibu hoja za uwongo wa shetani kwamba Mungu amemuumba mwanadamu bila kumpatia kusudi(life purpose)ni jukumu lake kulitafuta hilo kusudi ndipo wazo la Uchawi huu wa ''Yoga" linapopata nguvu.
Yoga ni ushetani na ni ibada ya sanamu tu watu wa Mungu hawapaswi kujizingua na ibada hizi.
 
  • Thanks
Reactions: Ok9
Ndefu ila ntaipitia nijue
hahahahaaaa hii maneno yako yalinipeleka mbaaaali we ulitaka iwe fupi kwa kiasi gani ila ukiipitia nijuze pia kama inafurahisha au la maana pia nna yangu ndefu kama hii ya huyu kaka

ila hiyo inahusu siasa
 



Wewe ni nani?



Wewe sio kazi yako unayofanya, wewe sio kundi la watu unalojihusisha nalo.

Wewe sio mawazo yako,

Wewe sio Akili yako,

Wewe sio mwili wako,

Wewe sio mtu mwenye furaha, huzuni, hasira wala shida kama unavyojifahamu,

Wewe sio tafsiri uliyozoea kuifahamu.





Wewe ni nani?

Wewe sio ambaye wazazi wamekuambia,

Wewe sio ambaye marafiki wamekuwa wakikuambia,
Wewe sio ambaye viongozi wa dini wamekuwa wakikuambia,
Wewe sio ambaye serikali imekuwa ikikuambia,

Wewe sio maelezo unayotumia kujielezea kuhusu wewe.




Achia mbali majina unayoitwa, maelezo unayojielezea kwenye mitandao kama Facebook au mitandao mingine ya kijamii.




Achia mbali jina lako, aina ya mtu unayejijua wewe ndiye, sifa ulizonazo, muonekano, asili, tamaduni yako au sifa ulizoandikiwa kwenye kitambulisho chako cha kazi au masomo,




Je unajisikiaje hivyo vyote ukiviachia mbali na kujiuliza wewe ni nani.




Nini kinabakia ukitoa mali zako, mwili, akili, shida, mawazo yako, imani yako, mazoea yako, tamaa zako, jina unalopewa na watu au unalojipa wewe, na sifa unazopewa na watu na sifa unazopewa wewe?




Wewe ni nani?




Kama wewe sio unachofanya,

Kama wewe sio unachofikiria,

Kama wewe sio unachopenda,

Kama wewe sio maelezo unayotumia kujitambulishia,

Je Wewe ni nani?




Tambua kwa kina...




Hauzuiliwi na mipaka ya mwili,

Wala wewe sio mapigo ya moyo wako,

Wewe sio Akili yako, mawazo yako na hisia zako,

Je kama wewe sio hivyo vyote je wewe ni nani?




Vuta pumzi taaratibu, hewa hiyo inaingia kwenye mapafu halafu inaingia kwenye kila seli ya mwili wako.

Funga macho, acha kuwaza, acha kuweka mawazo nje yako, hisi nafasi inayobakia iliyo kimya, na isiyo fikiria, waza, wala isiyokuwa na hisia yoyote kutoka kwenye milango ya ufahamu.




Kumbuka wewe ni nani, kumbuka hauna mipaka, mwili utakufa utauacha, jinsia yako nayo unaiacha, mali utakuwa nazo bali nazo utaziacha, hisia ulizonazo ambazo chanzo chake ni mwili wako nazo utaziacha mwilini, hasira na mawazo nayo yote utayaacha, sifa ulizopewa kama vile ulikuwa mchoraji bora au mwimbaji bora n.k nazo utaziacha kwani nazo zinategemea mwili mfano unaimba kwa kutumia mdomo lakini ukifa unauacha na huo mdomo na sifa zake ulizozizoea.

Je kama maisha yako ya hapa duniani yatakapoisha vyote hivi unaviacha...

Je wewe ni nani???








Wewe ni ufahamu unaofahamu vyote hivyo,

Jiangalie ndani yako kwa kina,

Wewe ni empty,hauna kitu

Wewe ni sehemu ya muumbaji,

Kila ukionacho, unachokiwaza, unachokitenda, na unachokizungumza kinawakilisha ulimwengu wa ndani yako.




Wewe na mimi ni kitu kimoja, wewe upo kama mimi na mimi nipo kama wewe.




Tunachopaswa kufanya katika safari ya maisha ni kujijua na kujitambua. . .



[h=3]Asante.[/h]
Naamini ile module utakuwa umeielewa kwelikweli nfkiri ni ktk philosophy of the mind hapo ndipo Renee de carte aliposema " I THINK THEREFORE IAM"
Umenikumbusha mbali sana asante
 
ni shairi sema modern poet ndio mana hajafata vina na mizani...
 
Back
Top Bottom