Umeshawahi kujutia kumsaidia mtu?

Kuna rafiki yangu mmoja kwa kabila ni muhaya ..tulisoma nae Tambaza sekondari...akaenda pale TIA kurasini kwenda kusomea degree ya procurement..

Mimi nikiwa Arusha akanitafuta alipokua mwaka wa tatu na ndo ame graduate..akasema kaka,nimeitwa kwenye interview na staki kukosa kazi .

Akasema naomba uniazime laptop niende Nayo kwenye usahili...maana hiyo ndo requirement ya kuingia kwenye chumba cha usahili...

Basi ilikua mwaka 2015, nikamjibu nikamwambia Mimi sina laptop ,siwezi kukusaidia..akasema niazimie hata kwa rafiki zako wengine.

Basi nikajipinda,nikamuazimia kwa msela then nikampa laptop aende nayo kwenye usahili...

Zikapita siku, wiki,mwezi ,miezi...na simu akanizimia na akawa hapatikani..kwao walikua wanaishi na mjomba ake ambae ni kigogo pale TRA makao makuu nao wakawa hawajui alipo.

Mjomba ake nilivyoenda kumlalamikia akasema hawezi kulipa maana "ameshalipa" laptops nyingi sana ambazo mdogo wake aliwaibia watu ..

Basi ikabidi nitafute million moja nimnunulie PC mpya huyu msela alieniazima..


Miaka ikapita,toka tukio litokeee mwaka 2015...mwaka 2019 MUNGU sio athumani..akamleta mdaiwa wangu mikononi mwangu. ..

Nikamuona pale Temeke ,kituoni akiwa anasubiri bus ...nikamfanyia ambush..nikachukua vyeti vyake vyote toka cha kuzaliwa,sekondari mpaka degree na vyeti vyote vya trainings na nikavitia moto.....


Kenge sana huyu....!
 
Dah!! Mkuu ulifika mbali sana!!!
 
mmh!...sisemi ila mpaka mda huu naandika..
kuna jitu limelia shida nikalisaidia japo kuwa na mie ni mnyonge...
Lakini..alichonifanya... sina hamu..nimechomoa pesa pabaya kwa kujua atanipa nirejeshe baada ya siku mbili.
Leo hii karibia mwezi...
 
Dah, pole sana mkuu. Fadhili mfadhili mbuzi utamnywa supu siku moja na ngozi utawambia ngoma watu wacheze mdumange huko mboga zako zikinawiri kwa mbolea ya samadi bustanini.
Msamehe bure, kuna sababu Mungu anataka ujifunze jambo.
Tunza sana maneno yangu. Kuna siku atatembea kwa magoti 2km kukuomba msamaha au msaada, hayo ni mapito tu usikate tamaa.
 
Nimemsaidia jamaa kulimpia ada university, semester moja, lakini haitoshi msenge huyu akanidhulumu tena 85,000tshs.
 
Yaan hawa watu wanaweza wakakufundisha roho mbaya yaan acha mpaka leo nilkuwa najiuliza et hv m n mpaka lini ntapunguza hz huruma za kijinga yaan m sijui nikoje sijui n huruma yan mtu akishaniambia nna tatzo bas niko laz nimkopee hata kwa mtu ila sasa nnayoyaona yanachosha watu sijui wakoje
 
I feel you bro
 
Same as me nmekuwa lijinga sana la ku saidia watu ambao wengi wao hawana impacts yoyote kwangu zaidi kuniretea shida. Nna mifano zaidi ya 100 watu ambao nmewasaidia wakaja kuni betrayal.
 
Unajifungia baraka zako kwa hilo, tenda wema nenda zako. Sio lazima usaidiwe na ulomsaidia. Hata huyo mama alokusaidia ni kwasababu nawe ulimsaidia jamaa.
Samehe na achilia.
 
Hapa nitajaza gazeti ila kikubwa nilichojifunza.

Msaidie mtu akiwa na shida aende zake akafanye yake ili arudi tena akiwa Na shida nyingine.Hii Ina maana epuka sana kuwasaidia watu ile first time maana pale ndo umewapa kibali na jinsi unavyomsaidia mtu ndo jinsi anavyokuja kwako na shida.

Wengine walivyo was*nge anakopa laki leo anaenda tatua shida yake akimaliza anajisahaulisha deni,Kama unavyojua watoaji wote duniani hatujui kudai dai. Anakaa huko weee kama miezi 6 anarudi tena kukopa hazumgumzii deni la nyuma,najiulizaga kwahiyo anahisi nimesahau deni langu au ndo ananiona mi far*
Watoaji ni wale wale siku zote na walia shida Ni wale wale siku zote.

Watoaji tujifunze kuwapuuza watu tuliowasaidia maana baraka zetu Mungu atatupa kwa wale ambao hatujawahi wasaidia, tuachane na manung'uniko Yana punguza baraka.

Ukimsaidia mtu Ni tusi yaani wengi wao pale Ni Kama umemtukana, wewe una shida na mimi nipo juu yako ndo Mana nakusaidia .Kwakuwa walimwengu Ni wabaya basi anatamani hata akuseme vby tu ili usionekane mwema sana au mgombane ili asilipe huo Msaada.

Namalizia kwakusema watu wakulia shida Ni wabinafsi sana wanakuawaga wamesaidiwa sehemu nyingi na wanaogopa wakitoboa watalipa fadhila sehemu..

Givers should be careful because takers do not have any.
 
Kwanza pole Kwa madhila yanayokukuta. Lakini kwa upande mwingine naomba nitofautiane nawe Kwa namna hii, wewe hukutenda Wema na kwenda zako, bali ulingoja na bado unangoja shukrani. Kwa maana hiyo, kinachokuumiza si kule kutokusaidiwa na jamaa, BALI MSAADA ULIOTOA unalinganisha na kinachotokea sasa.. wangapi huwajui na hujawahi kuwasaidia WAMEKUPITA ULIPOSIMAMA BILA YA KUKUSAIDIA NA HUWALAUMU?

Ukimsaidia mtu usitegemee malipo, ingawa kibinadamu ni ngumu.
 
Wengine walivyo was*nge anakopa laki leo anaenda tatua shida yake akimaliza anajisahaulisha deni,Kama unavyojua watoaji wote duniani hatujui kudai dai. Anakaa huko weee kama miezi 6 anarudi tena kukopa hazumgumzii deni la nyuma,najiulizaga kwahiyo anahisi nimesahau deni langu au ndo ananiona mi far*
Watoaji ni wale wale siku zote na walia shida Ni wale wale siku zote.




[emoji115] Hapo kama nimekuelewa vile.
Kwakweli huwa wanakera. Mtu anajisahaulisha Sijui ili iweje!?!?!
Ukifatilia chako anakuona msumbufu. Khaaa!
 
Ndo ungundue kuwa tunatofautiana na hapo umeshajua hakuwa rafiki sahihi,Wakati mwingine Mungu hurusu majaribu ili ujue rafiki wa kweli
 
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16] hahaaaa
 
No haupo sahihi mkuu kumbuka ni rafiki amgu mkuu tangu utotoni

Na unapopatwa na shida huwez omba msaada popote utawaomba unaowafahamu

Akiwa kama rafiki mkuu ilikua lazima nimwombe si kwa kuwa nadai fadhila hapana n kwa kuwa ndio mmja ya watu waliostahili kwangu kuomba msaada ule
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…