Umeshawahi kukosa au kukataa hela sababu ya mapenzi

Mshangazi dot com

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2011
Posts
1,345
Reaction score
3,503
Mapenzi Shikamoo!

Usiku huu nimeshuhudia mkaka anarudisha gari na fremu ya biashara kwa mmama aliyekua anadate naye sababu amepata msichana anayempenda na anataka kumuoa. Huyu mkaka amekua na mahusiano na huyu mmama ambaye ni rafiki yetu kwa zaidi ya miaka mitatu. Aliacha ajira serikalini, akafunguliwa biashara, akapewa gari na mwaka huu kalipiwa fremu yake ya pili kodi mwaka mzima apanue biashara zake.

Nyuma ya pazia kumbe alikutana na msichana, akampenda na akamwambia kila kitu kuhusu mmama wake anayefadhili lifestyle yake. Msichana akamwambia achague kati ya yeye au mmama na kama anampenda arudishe vitu vyote alivyopewa na waanze maisha upya wao kama wao.

Leo kijana kaja na karudisha kila kitu including gari lilikokua na jina lake na umiliki wake halali. Rafiki yetu naye anaugulia maumivu na hataki vitu vilivyorudishwa anasema yule kijana avichukue tu, upande wa pili mkaka hawezi kwa sababu demu wake mpya hataki.

Vipi, ushawahi kukataa hela au kuachia kitu chenye gharama kwa sababu ya mapenzi?

 
Mwambie anichukulie mimi yeye kama hataki Mxiuuuuuu πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…
 
A-level Mwakavuta high school 2015, nilikuwa na hali ngumu ya maisha, rafiki yangu kwao palikuwa mambo safi, akawa ananisaidia mambo madogo madogo ya matumizi.

Siku Moja akaniambia nimfire anipe 50,000 nikashtuka sana maana sikutarajia kama jamaa ni mchicha mwiba. Niligoma na ushkaji ukaishia hapo.
 
Mkuu haya mambo kumbe yapo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…