Umeshawahi kukutana na mtu anachekesha sana bila kutumia nguvu?

Umeshawahi kukutana na mtu anachekesha sana bila kutumia nguvu?

Oya kumchekesha mtu zima tena live ni kazi sana..
Waheshimu sana wale wa live comedy na watu wanacheka!
 

Mlicheka sana kwakuwa hamkuwa mmelipa kiingilio kwaajili ya kwenda kuchekeshwa. Ni ngumu kidogo kuchekesha watu waliotoka nyumbani kwenda kuchekeshwa.
Ukimsikiliza bwana kelvin hart akiwa anahojiwa tu,sio ukumbini kwenye kiingilio,utajua kweli kuchekesha ni kipaji.jamaa huwa anachekesha kwa kila story yake,hata za maisha ya kawaida tu akikusimulia.

Mtu mwenye kipaji huwa hatumii nguvu kabisa,kuna jamaa tukiwa wadogo tunacheza mchezo wa kombolela,akiwa yeye ndiye ana zamu ya kutafuta,hachukui dkk 5 kashawashika wote😅😅😅.
Ataanza kujiongelesha upuuzi wewe ukisikia lazima uangue kicheko.
 
E bana jana kwenye bajaji nimekutana na jamaa mmoja anakipaji cha kuchekesha, angepata exposure sipati picha kwenye stage angekalisha sana.

Tulikua abiria watatu na dereva, pikipiki ikapita kwa speed sana ndio akaanza kuelezea mkasa wake wa ajali wakiwa wamepakizwa kwenye fekon huko mkoani.

Aisee kikawaida mtu angeelezea ungemsikiliza halafu ukamjibu ikaisha ila wooote ikiwemo dereva mpaka anamaliza story kila mmoja amekaukia anacheka sana.

Yaani lilikuwa jambo la kusikitisha lakini mimi binafsi mpaka naandika hapa nacheka bado imagine hiyo jana.

Sina muda mrefu sijacheka namna hii mpaka machozi yalitoka. Yule jamaa angepata exposure ni comedian level za juu sana. Imagine uchekeshe bajaji nzima tena kwa jambo la huzuni.

Aisee guys huyu jamaa anakipaji sana.
Alisemaje mkuu?
 
Back
Top Bottom