Hata mimi ningekuwa mzembe hali hii ingenitokea,ila nilijiongeza ,kuna kipindi nimemaliza form 6 miaka ya 2010 hapo wazazi wote washafariki chuo nimenyimwa mkopo nikawa nipo nipo tu,ikabidi niende kwa brother angu mtoto wa baba Mkubwa nikakae mitaa ya temeke ili nibadili mazingira kidogo ya mtaani kwetu maana niliona frustrutation za kuulizwa chuo lini sijui unafanya nini sasa hivi zitanichanganya!kwanza niliongea na bro kwa simu akakubali niende ,nikafika pale nikawa very descent boy,bro alikuwa na mke na watoto wawili pia alikiwa anaishi na mdogo wake wa tumbo moja umri sawa tu na mimi hivyo tukaws tunaishi chumba kimoja na mshkaji ila jamaa alikuwa haelewani na shemeji yake kabisa,hivyo mimi nikawa kidogo nabalance mambo,naamka asubuh nasaidia kazi za,nyumbani ,napeleka madogo shule,nawafata jioni ,napitia maftari yao ya shule yaani walinipenda kiukweli sabbu bro na mke wake hawakuwa na elimu kivile walikuwa wafanyabiashara tu,hivyo mimi ndo nilikuwa nawasaidia watoto homework etc,kwa aina ya yale maisha nikatokea kuelewana na shem ila yeye akawa anataka kuvuka mipaka na mazoea,mara siku nyingine akiona bro hayupo aniite chumbani nimsaidie kuweka vzr kitanda huku kavaa khanga moja tu na aidondoshe maksudi ila najifanya sijaona kitu,siku nyingine akiona tumebaki wawili tu anataka kuangalia picha za kikubwa,nikaona hapa utakuwa msala nitaharibu mahusiano na ndugu yangu nikatafuta sehem walau niwe nafhndisha tuition kwa udi na uvumba ili niwe nashinda hukooo,nategea muda wa kurudi watu wote wamerudi home,nikawa siku nyingine nikiona bro amesafiri nalala kwa mshkaji wangu mahali hata siku 2 ili kupoteza yale mazingira ya mazoea kupitiliza,mpaka nikapata kijibarua mahali cha kunipa mia 2 ya uhakika nikapanga chumba fasta nikahama,ila inshort tu niliandaa mazingira ya kupoteza yale mazoea ya kupitiliza naamini kilikuwa kama kiupepo flani kibaya hivi kilitaka kumpitia kwani baada ya pale alirudi normal tu tukawa tunapiga stori kawaida namimi sikutaka kuiongelea mahala popote zile situation ,nilikabiliana nazo mwenyewe kiume!
Sent using
Jamii Forums mobile app