Umeshawahi kupata kazi kupitia Linkedin?

Umeshawahi kupata kazi kupitia Linkedin?

Nilitafutwa na client kazi ya transcription (Google Loft tool) lugha Chichewa na Kilingala.Ilikua ni kazi ya pesa ndefu ila Wamalawi Waka iangusha online gig kwao wanaona ni utapeli.Nikasubcontract kazi Kwa Mkenya at least nikaingiza vidola kadhaa.Client bado nipo naye na kuna kazi za translation nazipata.Kikubwa tengeneza profile nzuri tu.Adios
Na hivi kwa sasa kuna ChatGpt AI ni mseleleko
 
Nshapata kazi nyingi kupitia linkedin na nawafahamu watu wengi waliopata kazi kupitia linkedin tena kwa kufuatwa.
Huwa unapost vitu huko??
Ama una andika qualifications zako as detailed as possible, ur strengths, experience,.. katika kila section ambayo unaweza fill, then fursa zinakuja,..
Em tupe madini
1. Kitu gani kilisababisha ukawa approached at first,,? ni kupitia posts ama just the profile bila posts, ama ni demand ya field uliyopo
2. Nini kilileta hizo kazi nyingi nyingine, ulikuwa unapost kazi nyingine ulizopata before!?
 
Ni app nzuri sana hakikusha profile Yako Iko vyema.

Mimi Huwa nafanya majaribio hata kama kazi siitaku pia jitahidi kuwa na connection kubwa uwezavyo.
Tofauti na kutuma maombi huwa nafuatwa inbox na recruiters kibao. Kwa February pekee nilifuatwa na kampuni 4 inbox na zote nilifanya interview.

Mwezi huu pia nilituma application 2 na zote zikakubalika wakaniita interview nikawaambia niko nje ya nchi labda tufanye phone interview; Moja nilifanya na kazi nikawa nimepewa na walikuwa tayari nifanyie huku nilipo mpaka nitakapo Rudi ; nyingine wanahangaika kufanya appointment na GM wao ili tufanye hiyo interview Huku niliko.

Kwa ufupi ubora wa profile Yako pamoja na connection uliyonayo utakurahisishia kazi.

Jitahidini kujenga mazoea yakufanya interview hata huhitaji kazi hii itakijengea experience moja kubwa sans.

Niliwahi kwenda kwenye interview ya kuitwa bila kuomba kazi nikakutana na mhindi empty kichwani alafu ana nyodo na maswali yake ya google mbona alikoma😂😂😂😂 nilimchana na nikakataa hiyo kazi kitaalamu

Naweka na viushahidi msije kusema ni mbwembwe za JF
Screenshot_20230324-090305.png
Screenshot_20230324-085804.png
Screenshot_20230324-091732.png
Screenshot_20230324-092130.png
 
Huwa unapost vitu huko??
Ama una andika qualifications zako as detailed as possible, ur strengths, experience,.. katika kila section ambayo unaweza fill, then fursa zinakuja,..
Em tupe madini
1. Kitu gani kilisababisha ukawa approached at first,,? ni kupitia posts ama just the profile bila posts, ama ni demand ya field uliyopo
2. Nini kilileta hizo kazi nyingi nyingine, ulikuwa unapost kazi nyingine ulizopata before!?
Hapana sipost chochote ila ni vizuri sana ukapost kitu inakupa mileage.
Mimi huwa nina approach ma hr na ma vendors nawadd then najiintroduce sometimes nawatumia ujumbe kuwaambia services zangu ila mara nyingi kuna ambao huwa wao ndio wananioffer kazi.
Kwa mara ya kwanza kwakweli sina hata jibu, maana nilikuwa new na profile yangu haikuwa nzuri kihivyo ila kuna jamaa alinitumia invitation nilipo iaccept akaniambia kampuni anayofanya nayo kazi inatafuta mtu anayetoa service kama zangu so, akaniomba email akawapa hapo hapo waka niemail.
Kazi nyingi zinakuja zaidi baada ya kuwa umefanya na client wengi zaidi na ukaupdate profile yako kwenye experience. Pia kulink na watu ambao wako kwenye circle ya kitu unachofanya ni rahisi kukurecommend.
 
Back
Top Bottom