Umeshawahi kupotea Kariakoo? Juzi ilibaki nukta nipige mayowe

Kuna kijiji kimoja(Kibera/Kibira) kiko Nairobi Kenya katikati ya mji kabisa, na kwa ukubwa ni cha pili Africa baada ya Soweto ya Africa kusini(Ndani ya hicho kijiji kuna sehemu inaitqa Soweto pia) , japo sikuwa mwenyeji lakini sikuwahi kupotea.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Mkuu lakini mnazi mmoja na Kariakoo mbona ni pua na mdomo tu, labda kama ulikuwa umechoka
 
Kupota njia ndio kujua njia
 

Kweli kabisa mkuu
 
Hapo k.koo majuzi tu mwezi wa sita nimepotea nilipopaki kigari changu

Ilikuwa hivi nimetoka uelekeo wa fire pale kituo cha mafuta nikaja mpk kwnye mataa ya msikiti pale magari ya muhimbili-Kiwalani yanapoingilia nikaingia kama naenda jangwani vuup mpk mtaa wa nyuma kidogo ya China plaza nikapark pale.
Nilikuwa na shida ya kutengeneza Pc nikamaliza shida zangu fresh njaa ikauma nikaenda kula sehemu flani karibu na Kanisa la KKT lile nadhani.

Sasa nikasema acha niondoke nirudi nyumbani eee bwana eeh tafuta mtaa niliopark gari naona hola. Kila nikienda mtaa huu naona mbona kama nilipita hapa nafuata mtaa mpk barabara ya mwendokasi kule hola narudi tena mtaa wa pili hola.

Nilipoteza kama masaa mawili kila nikienda nakuta gari si yenyewe mpk nikasema nimeibiwa gari mana nilipark hapa na siioni.

Ubaya ni kwamba wakati naingia kuna jamaa alinipigia simu hivyo akili ilikuwa kwenye simu badala ya kukariri sehemu mpk nashuka nilikuwa bado naongea na simu tu.

Mungu si athumani mida ya saa kumi hivi nikapata hiyo sehemu ndio naenda kuikuta gari na dada wa parking anasubiri chake nimpe.
Hapo nimechoka mpk akili majasho kama yote sitaki kukumbuka.
 
Mimi nilishapotea majira ya muda wakati nachunga ng'ombe milimani huko kijijini, yaani kiuhalisia muda ulikuwa saa tisa adhuhuri lakini lile jua lilionekana kama jua la saa nne asubuhi, kilichotokea ni kwamba nilifika na ng'ombe kijijini saa 3 usiku wakati wananzengo wakiwa tayari wamekuja kunitafuta. Kuna neno la kilugha huitwa unapopotea kwa namna hii na wanadai kuna aina ya majani unakuwa umeyakanyaga.
Sasa kwa swala la kupotea kariakoo nilishapotea sehemu nilipokuwa nimepark gari lakini nilikuja kupapata baada ya nusu saa hivi......
 
Pamoja na uzoefu wangu wote kuishi Dar kiukweli sijawahi kuielewa mitaa ya kariakoo.Sijui tatizo ni kutochukulia serious kukariri majina ya mitaa! Sijui mtaa wa Aggrey unaanzia wapi mpaka wapi sijui... Ila maduka ninayajua vizuri,Tatizo usipokuwa makini unaweza ukadhani njia unayofuata unatokea Msimbazi Mwendokasi ukajikuta unatokea Mnazi Mmoja [emoji23][emoji23][emoji23] au ukajikuta unauzunguka mtaa mmoja huohuo unaenda unarudi!
 
watu bwana mnapoteaje kkoo yaani ww unakodi bajaji toka mnazi mmoja mpka gerezani kwa 4000 wa mikoani mnachekesha
Mkuu mm siyo wa mkoani na kariakoo hakuna mtaa nisioujua hata mmoja..nadhani Ile siku akili ilistuck na kosa nililofanya ni kulala ndani ya gari alafu nikashuka Tu bila kumuulizq mshikaji umeniacha mtaa gani nikajikuta mtoto wa town

Jamaa wa bajaji alikuwa anaenda ferry so mm nikamrudisha anipeleke gerezani so alikuwa na Haji ya kutaka hiyo hela maana Tyr nilishafika viunga vya mnazimmoja
 
Bithaa ya farasi malaya na BUNDUKI haramu na watoto wadogo nipe MACHIMBO DM[emoji24][emoji28][emoji24][emoji24][emoji1787][emoji23][emoji28][emoji17][emoji482][emoji482]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…