Kuna kijiji kimoja(Kibera/Kibira) kiko Nairobi Kenya katikati ya mji kabisa, na kwa ukubwa ni cha pili Africa baada ya Soweto ya Africa kusini(Ndani ya hicho kijiji kuna sehemu inaitqa Soweto pia) , japo sikuwa mwenyeji lakini sikuwahi kupotea.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Siku moja natoka tegeta na lift ya gari la mshikaji mida ya saa moja usiku,tulipofika k/koo jamaa kanishusha akaelekea zake ferry anaenda kigamboni mm ikabidi nichukue usafiri wa home kule gerezani..nikikumbuka Ile siku kilichotokea nachekaga tu maana jamaa tulipofika k koo aliniamsha Tu oya mwanangu kariakoo hii km vp tomorrow basi..nikashuka!!
usingizi jumlisha usiku sikujua kbs nimeshuka mtaa gani. Akili iliganda km nusu saa najiuliza jamaa kanishusha wapi hapa? Ikanibidi nitembee Tu mm mtoto wa mjini bn siwezi potea k/koo lkn bado akili haisomi kbs ninakoenda ni wapi
Nikasema isije nikatokezea kusikojulikana maana nimetembea kishenzi sifiki gerezani ngoja niulize.Nikamcheki muuza mayai kumuuliza asee naelekea iliko stend ya mwendo Kasi akanijibu sasa huku unakoenda mbona unakaribia kufika mnazi mmoja[emoji1787] ..nikamwambia niitie bodaboda akanijibu labda bajaji.Nikakodi bajaji Kwa buku 4 Hadi gerezani..nikikumbuka najiuliza hivi ilikuwaje nikapotea k/koo siku ile.Sipati jibu
Hahahaahakila nikisikia wanashusha yale ma milango yao ya bati, napanick natoka nduki....
Kupota njia ndio kujua njiaHii mada inawalenga sana wale wenye mishe misheza manunuzi kariakoo.
Aisee kama huna uzoefu na ile mitaa, hasa ile ya nguo, nakushauri ukinunua mzigo wako ukiona huwezi tembea nayo bora utafute hoteli ulipie uwe unakusanyia mizigo yako hapo...
Mimi sio mgeni wa k.koo hata kidogo, ila juzi ni kama ndio nimefika kwa mara ya kwanza,
Ipo hivi
Nimefanya manunuzi yangu ya nguo za jumla, Ikawa kila ninapochukua mzigo sababu ni mkubwa na bado naendelea basi naufunga namwachia mwenye duka mpaka nitakapo maliza nazungukia kote nabeba,
Pasipo kuelewa jinsi ninavyoiacha ndio nazidi kuchanganya mambo, imefika saa 9 hivi nikawa nishamaliza, ni kuanza ku kusanya sasa,...
Nilikua na location 9..., Nikaanza moja baada ya nyingine, Zikabaki 3, hizi sasa ndio kimbenbeee,
Siku za nyuma ilikua kila nikiacha mzigo basi na kalili ule mtaa na duka ili iwe rahisi baadae, Sasa juzi kwa haraka niliyokua nayo na huku nikiamini sijawahi potea na nishakua mzoefu nika ignore hilo swala,
Aloo, Nilizunguka ile mitaaa huku machozi yakinilenga kadiri mda unavyopita,
Duka la kwanza kati ya yale matatu nililipata baada ya 2hrs, kumbuma hizo 2hrs zote nilikua natafuta bila kupumzika,
Na sio kama nililiona mwenywe ila nilikua napita lesi ndio jamaa akaniita akaniuliza "bro vipi bado sana maana ndio tunakaribia kufunga...."?
Nikajifanya "Ahaaa basi poa ngoja tuu nitembee nao" nikachukua mzigo huku moyo ukiruka ruka kwa kushukuru, Yaani pale ndio kabisaa nilikua sipawazi kama nilifanya manunuzi....
Sikutaka hata kuchelewa nikaupeleka guest, inshu ni hayo maduka mawili, Kazi ikaanza tena, hapo mda umeenda, watu washaanza kufunga, kila nikisikia wanashusha yale ma milango yao ya bati, napanick natoka nduki....
Nikatafutaweeeeee, inafika saa 12, nimechoka, nimepanick, nimekata tamaa, Jasho na kiu haviniishii Nishanunua maji kama katoni nzima na henganjifu za kutosha ila vyote kila ninapo simama nikiondoka nimesahau.
Ikafika saa moja, Hapo sasa wengi washafunga, nikawa natembea kinyonge, machozi yananilenga nikiona magrili yanashushwa tuu, nikakaa sehemu ilibakia nukta nipige mayoweee....
Sikua na la kufanya zaidi ya kusubiri kesho yake ambayo ni jana, Akili ilikua ishachoka, nikampigia Rafiki yangu aje tuu anitoe pale nilipokuwepo, maana niliona kabisa mwendokasi ikinivaa, ..
Asubuhi, nikaingia tena, Inafika saa 6, bila bila, hapa nikaanza kupiga hesabu namna ya ku compensate hasara ya kama 900k na usheee(almost 1M kasoro).
Nikakaa tena sehemu, hapa ndipo nikagundua kweli akili ya binadamu kuna mzingira inafanya kazi baadae ukikaa ukijiuliza ni wewe huamini....
Nilianza kuvuta kumbukumbu za kuanzia Mwanzo naingia k.koo ile jana asubuhi, nini nilianza nacho, wapi nilianzia, basi kuanzi hapo mtiririko wa mazingira ya nje ya kuanzia duka la kwanza mpaka la 9 ukanijia,
Hayo ni mazingira ya pale dukani, inshu ni mtaa na njia gani??? Kwa kumbukumbu hivyo hivyo nikaja nikajua ni duka la ngapi na la ngapi katika ule mtiririko ndio nimeyapoteza,
Njia kila nikivuta kumbukumbu haziji, nikaona best option ni kwenda kuanzia duka la kwanza kutembea huku nikivuta kumbukumbu, ile ndio ilikua pona yangu, Mzigo wa kwanza nikaupata duka namba 4 mtaa wa Congo na agrrey, mzigo wa pili duka namba 7 Mchikichi na Nyamwezi...
Bahati nzuri ni waaminifu, nikakuta mizigo yangu salama, nikabeba, huyoooo....
Mpaka nikakumbukaga kale ka meme, watu wanakatumaga kiutani ila kumbe inaonesha wao yalishakuta..
"Ulishawahi kupotea kariakoo mpaka ukapita sehemu ukawaliza watu, mliniona nikipita hapa?"
Mtu unaweza ukapotezwa na akili yako japo ile sehemu unaifahamu,unaweza kupotea coz akili yako inakua ipo mbali sana,ndio maana mtu akitulia,akili nayo hutoa ushirikiano na utakumbuka unapokwenda,
Kupotea ni jambo la kawaida hasa kama mtu ana mawazo,kupotea sometimes hakuhusiani na uenyeji au ugeni.
Mm nikiwa sehemu nimepotea vile ninavyotembea kwa kudunda na kujidai ili watu wasinishtukie unaweza kusema huyu jamaa ni mwenyeji wa eneo hili,kumbe kichwani nna stress tele.
Zero mlizozipata darasani zinawafata mpaka kwenye maisha ya kawaida
🤣🤣[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Mkuu lakini mnazi mmoja na Kariakoo mbona ni pua na mdomo tu, labda kama ulikuwa umechoka
Mkuu mm siyo wa mkoani na kariakoo hakuna mtaa nisioujua hata mmoja..nadhani Ile siku akili ilistuck na kosa nililofanya ni kulala ndani ya gari alafu nikashuka Tu bila kumuulizq mshikaji umeniacha mtaa gani nikajikuta mtoto wa townwatu bwana mnapoteaje kkoo yaani ww unakodi bajaji toka mnazi mmoja mpka gerezani kwa 4000 wa mikoani mnachekesha
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]Zero mlizozipata darasani zinawafata mpaka kwenye maisha ya kawaida
Bithaa ya farasi malaya na BUNDUKI haramu na watoto wadogo nipe MACHIMBO DM[emoji24][emoji28][emoji24][emoji24][emoji1787][emoji23][emoji28][emoji17][emoji482][emoji482]Bhs wewe sio mzoefu na kariakoo, kariakoo unatakiwa uijue mitaa yake ma majina yake mfano machimbo ya nguo ni congo street na nyamwezi street lakin kuna mitaa ambayo inakutana na congo au nyamwezi ukijua hlo bhs kariakoo huwez potea mtu akikwambia nko agrey na congo chap unakimbia. Kariakoo kila bidhaa najua mtaaa inakopatikana[emoji119]