Umeshawahi kupotea Kariakoo? Juzi ilibaki nukta nipige mayowe

Hii nyingine zamani Hiyo nilikwenda hapo ubungo business park nakwenda kwenye ATM za EXim ,huko nilikotoka nimetoka na nauli tu sh 500 sina nauli ya kurudia sababu najua naenda kuchukua hela ,hizi huduma za mobile money hazikuwa zimeshika kasi,nafika hapo business park nakuta ATM ina shida haifanyi Kazi ,ATM nyingine ya karibu ipo Mlimani City nikasema sio kesi natembea KWA mguu,

Akili yangu ikapiga hesabu kuwa nikiingilia shekilango nikitembea tembea kisha huko mbele nikakunja kushoto ntatokea Mlimani hahhha
Salaleee!!
Nilikosea hesabu baada ya kuingia Hiyo mitaa ya hapo ubungo ,nilizunguka Sana sanaaaa mwisho wa SIKU nikatokea EMAUS nyuma ya STend ya ubungo baada ya kupoteza muda huko mitaani
Safari ya Mlimani ikaanza upya hapo ubungo Nikiwa hoi .
 
Hahahaha
 
Hahaha yaan hiyo mitaa ya mnazi mmoja to posta za hapo ndani ndani ni kisangaa
 
Kila mtu anakazania kuchukua contacts za muuzaji, ila kumbuka kama mtu sio muungwana ukimpigia akijua umepotea na ndio mara yako ya kwanza kwenda kwake ndio kwisha habari yako hio,

Chukua kwa dharura na wewe jitahidi kwenye mzigo wako andika namba(natarajia kama umeenda kwenye manunuzi hukosi angalau viwili kati ya notebook, kalamu na Marker pen) waambie wakitaka kuondoka wakupigie, wakikupigia basi hao ni watu na kama umepotea anzia hapo sasa...

Kukalili mtaa/kumbukumbu kichwani ni muhimu tuuh, Sio kila ukipotea basi kila mtu ajue umepotea, hasa sehemu za fursa kama zile.
 
asee jamaa yafaa kuwa comedian, nimechekaaa,ila hapo kuuliza watu kama wamekuona ukipita umetisha mkuu,
 
Jumapili nikaingiq njia ya kuelekeq shimoni saiv si wafanya biashara wanafanya biashara nje nikasem ngoja nizunguke nitokee nilipoingilia weeeh najikuta niko mtaa mwingine kabisa faster nikarudi na njia niliyoingilia kariakoo cjwah pazoea
 
Hahahahahahahahahahahaa dah nimecheka sana wallah
 

Eti akariri [emoji23][emoji23]
Wengine hawajui map app ni ipi wanataka wasaidiwe hata kuitumia pia
 
Pole
Sana
 
Ha ha ha .

Pole sana mkuu
 
Endeleza kidogo mkuu, ulimsaidiaje sasa!
 
Nilikwenda kufanya manunuzi maduka matano. Kila nilipoingia na kufunga mzigo walinifata wahuni wakikusanya mzigo kwa kisingizio kwamba niliwatuma wauchukue, wale wahuni walinigawana, kila ukiingia unakuta umeingia naye..ukiondoka anatoa maelezo kama wewe anaoewa mzigo.

Jioni saa mbili Sina mzigo hata mmj wezi wakijibebea, masikini wa Mungu ilikuwa duka la mwisho walau ningeambulia ule mzigo kwa kuwa ndio nilikuwa nao mkonon yule mwiz wa mwisho alifanikiwa baada ya kwenda kuita usafir...

Nikaiyona kariakoo inastahili ipigwe Bomu tufe wote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…