[emoji1787][emoji1787][emoji1787] ndio maana k.koo unaweza useme mwenzako yupo bussy kutafuta pesa kumbe kapoteanaaa yupo kwenye harakati za pimbi..
Maajabu ya Kariakoo kuzunguka na kushangaa umerudi duka ulilotoka ni kitu cha kawaida, dhamilia kutafuta duka ulilotoka sasa kama utalipata.
Kuna jamaa yangu naye alipoteana, inafika jioni anasema au niende polisi?????
Nikamuuliza unaenda polisi umetapeliwa? Haya lets say umedanganya ukadai umetapeliwa, haya wakikuambia tupeleke utaenda wapi?...
Kariakoo achana tuu na duka, ukiingia kule kati, kuitafuta tuu barabara kuu ya msimbazi pale polisi ni mtihani, badala ya kuifuata unaitoroka kuelekea mnazi mmoja, unakutana na mtu posta unamuuliza aggrey ipo wapi hapa?????
Au unamuuliza mtu, "huku naenda wapi?"
Mimi kipindi ndio naanza machimbo ilikua nikifika sehemu nikifanya manunuzi nikaacha mzigo, naigingia google map na search location then na save au ku screenshot, baadae nafuatilia tuu, kwa njia hio sijawahi potea, kwa sasa sihitaji uongozi wowote popote natoka...
Niliwahi kupotea Tanga usiku kwenye zile barabara zao za namba, ikabidi nirudi baharini nianze kuhesabu barabara.