Umeshawahi kupotea Kariakoo? Juzi ilibaki nukta nipige mayowe

Umeshawahi kupotea Kariakoo? Juzi ilibaki nukta nipige mayowe

🤣🤣🤣, kwa miaka yangu yote 10 Dar K/koo bado inanitoa jasho hiyo mitaa wanayouza nguo. Imewahi kunitokea mara 2 kama mwanzisha uzi, nimenunua nguo kwaajili ya biashara ili kuepuka usumbufu wa kuzunguka na mizigo basi nikawa nimeiacha dukani, sikuweza kufikiri kama ninaweza kusahau duka lilipo, nishamaliza kufanya manunuzi nalitafuta duka lilipo kumbukumbu haiji kabisa, nilizunguka almost saa nzima, nikaanza kupoteza matumaini ya kulipata duka na kuanza kukubaliana na hasara, nikahisi kifua kuwa kizito ghafla🤣🤣, nilivaa barakoa ilinibidi ile barakoa niitupilie mbali.

Nikajiapiza nazunguka mzunguko wa mwisho nisipolipata potelea pote. Baada ya kutuliza akili nikarudi starting point yangu jengo la DDC nikaambaa na huo mtaa mara ghafla sijafika mwisho nikaona utambulisho wa mtaa nilioingilia dukani, nikaambaa nao hapo sasa akili ndo ikafunguka,, tangu hiyo siku siachi mzigo bila kuchukua namba ya simu ili hata nikipotea napiga kuomba msaada🤣, nyieeeee acheni.
Mtaa wenyewe ni Raha na Muhonda.
 
[QUOTE="Champagnee, post: 40197317, member: 533Kariakoo kila bidhaa najua mtaaa inakopatikana[emoji119]
[/QUOTE]
Jibu ndo hili....sijawahi kupotea kariakoo na sitopotea...japokuwa Nina miaka miwili sijafika hapo!!!
 
Kwa asiyefika Tandika anaweza kushindwa kukuelewa lakini aliyewahi kufika, wala hashangai kusikia ulipotea!!
Hapo Tandika usiku nilizunguka mpaka nikachoka natafuta kituo cha daladala na mfukoni nilikuwa na buku tu aseee!! Pamekaa vibaya! But now haiwezi kuwa tena
 
Nimewahi poteana hapo Kariakoo mtaa wenyewe sio complicated
Lengo langu niende NMB nyuma ya kituo cha polisi msimbazi ,nimepanda costa natokea manzese ,badala ya Costa kupita fire ikakatisha mitaa ambayo siijui nadhan ni kwenye ofisi za mwendo kasi pale ila sikunote nilikuwa nimelala,
Tukaenda shushwa mitaa siko familiar nayo
Nikaona isiwe tabu nikachukua bodaboda nikampa maelekezo anishushe BIG BON
Nikapelekwa ila akili yangu ikagoma kbsa kuwa pale ni big bon ,
Petrol station naiona,na kituo cha polisi nakiona ,Ili viko upande tofauti na vinapotakiwa kuwa(KWA mujibu wa akili yangu)
Yaani mfano akili inaniambia kituo cha polisi kinatakiwa kiwe upande wa kushoto kwako mimi naona kiko Kulia kwangu ,nikadaka wenge
Najua kbsa Nmb wako nyuma ya kituo cha polisi ,ila akili yangu inageuza mazingira
Nikaamua kujiripua kwenda mtaa unaonipeleka huko nyuma ya kituo cha polisi Ndo kama nikawa nimeRESET akili
Vitu vyote vikarudi kama vinavyitakiwa kuwa.
Hii ilinotokeaga kipindi niko 1st year pale Duce. mwanzoni nilikuwa nimefikia kwa ndugu yangu Kimara, sasa nilikuwa nimezoea kwenda Duce kwa kupanda magari ya Kimara-posta/ Kimara k/koo, nashukia Magomeni, kisha napanda magari ya kwenda mbagala nashukia Duce.

Siku hiyo nikajichenga nikapanda magari ya Mbezi/ Kimara -simu 2000. Nikashushwa mawasiliano kwa mara ya kwanza..nashangaa shangaa tu. Ndo kuulizia wakaniambia ili kufika duce lazima nipande magari ya kwenda mbagala.

Nikapanda. Si nikashushwa kituo cha TAIFA, bwanaweeeeeee. Kwanza palivyo, kituo cha taifa kipo mbele kidogo ya barabara ya kwenda Duce kupitia Uhuru na uwanja wa taifa. Ili kuipata bara bara ya kwenda Duce lazima urudi nyuma kidogo.

Nilidata kinyama. Kila nikipiga picha haiji..load wee picha haiji. Kwa baadaeee ndo naona tujamaa tulitobeba mabegi nikajua hawa ni wanachuo, nikaanza kuwafata kwa nyuma..ghafla picha yotee hiii hapaaa..Nikasema ALAAAA!!!!
 
Acha tu haya mambo haya hayana mjanja. Nilienda Chuo cha DIT kumsalimia jamaa angu nilisomaga nae O level nilikuwa natokea mbagala sasa baada ya kushuka jamaa akanichukua tukaanza kutembea kwa miguu kwenda Chuo nikawa nakariri mitaa sasa tukamaliza kuongea akaniaga nikawa nasepa jamani Kurudi kwa migui kutafuta ile Stand ya Mbagala nilitamani kuliaaa[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28] ubaya na njia ya kurudi chuo nimeipotea hata kumpigia simu mwana naogopa... Nilizurura kule posta mamaee mpaka nikakomaa. Mwisho wa siku nikamuuliza machinha flani akanipa mwanga nilijicheka sana.


Siku nyingine nimetoka Kigamboni kuja kkoo kupitia njia ta darajani sasa nikashushwaa stand flani maeneo ya kule karume jamani sijui walinishushia upande ganii sikuamini kama sipajui waliponishushiaa[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] ila karume lile jengo la soko naliona aisee shukuru Mungu nikaliona jenga la Machinga Complex ndo ikawa pona yangu nikaanza kulifata maana lengo langu ilikuwa kwenda msimbazi.[emoji3] Kkoo na Posta hazina mwenyeji yani.
 
Acha tu haya mambo haya hayana mjanja. Nilienda Chuo cha DIT kumsalimia jamaa angu nilisomaga nae O level nilikuwa natokea mbagala sasa baada ya kushuka jamaa akanichukua tukaanza kutembea kwa miguu kwenda Chuo nikawa nakariri mitaa sasa tukamaliza kuongea akaniaga nikawa nasepa jamani Kurudi kwa migui kutafuta ile Stand ya Mbagala nilitamani kuliaaa[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28] ubaya na njia ya kurudi chuo nimeipotea hata kumpigia simu mwana naogopa... Nilizurura kule posta mamaee mpaka nikakomaa. Mwisho wa siku nikamuuliza machinha flani akanipa mwanga nilijicheka sana.


Siku nyingine nimetoka Kigamboni kuja kkoo kupitia njia ta darajani sasa nikashushwaa stand flani maeneo ya kule karume jamani sijui walinishushia upande ganii sikuamini kama sipajui waliponishushiaa[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] ila karume lile jengo la soko naliona aisee shukuru Mungu nikaliona jenga la Machinga Complex ndo ikawa pona yangu nikaanza kulifata maana lengo langu ilikuwa kwenda msimbazi.[emoji3] Kkoo na Posta hazina mwenyeji yani.
Tuliozaliwa ilala na kariakoo tunasoma comment zenu na kucheeeka
 
[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]
Nacheka kama mazuri lakini Hiyo ndio kariakoo bwana kiboko ya mabishoo. Pole sana.
 
Kwa staili liyofanya, ya kununua nguo halafu anaacha hapo hapo kisha anaenda sehemu nyingine na nyingine ili apitie baadae; my braza, hata kama unaifahamu vizuri mitaa lazima utachanganya madesa tu kwa sababu hapo issue ni zaidi ya kujua mitaa bali kujua nini ulinuua wapi!!!
Inabidi uchague point ambayo ndo kituo chako Cha kukusanyia mzigo. Kila unaponunua unapeleka pale na Kila unapokata mitaa hakikisha haupotezi uelekeo wa hiyo point.

Nakumbuka wakati naanza kuizunguka kariakoo point yangu ilikuwa AZANIA bank,
Kila nikipotea naingia MAp natafuta AZANIA bank, naelekea ilipo.
Nikifika ndo natokea pale kwenda sehemu nyingine.

Japo nshawahi kuitafuta karume ikakosa kwa zaidi ya masaa mawili nikiwa natokea kariakoo.
Mwenyeji wangu alikuwa karume akiniuliza namwambia nipo nakuja.
Kijasho kilivonitoka ikabidi nijisalimishe akanifuata nilipo.
 
Kuna ile mitaa karibia na BIGBORN sheli,
Kuna kichochoro unaingia.
Wanauza spea used za magari.

Aisee vile vichochoro vya vibanda vya mbao nilinyoosha mikono[emoji4][emoji116]
IMG_20210520_020503.jpg
 
Nilikwenda kufanya manunuzi maduka matano. Kila nilipoingia na kufunga mzigo walinifata wahuni wakikusanya mzigo kwa kisingizio kwamba niliwatuma wauchukue, wale wahuni walinigawana, kila ukiingia unakuta umeingia naye..ukiondoka anatoa maelezo kama wewe anaoewa mzigo.

Jioni saa mbili Sina mzigo hata mmj wezi wakijibebea, masikini wa Mungu ilikuwa duka la mwisho walau ningeambulia ule mzigo kwa kuwa ndio nilikuwa nao mkonon yule mwiz wa mwisho alifanikiwa baada ya kwenda kuita usafir...

Nikaiyona kariakoo inastahili ipigwe Bomu tufe wote
Pole Sana aisee
 
Kariakoo buana[emoji846], ukifika huwa mishale ya usiku inakuwaga kama sehemu nyingine kabisa, japo me nadhani ni kutokuwa na mazoea, Nilipofika DSM kwa mara ya kwanza, nilitamani nifahamu sehemu mbalimbali, Mungu si Athumani nikawa nimezifahamu sehemu nyingi,
One day nmefika Kariakoo kutoka mkoani,mida ya saa tatu usiku[emoji38] nilizunguka kutafuta stend ya daladala hadi saa tano usiku[emoji28], Just imagine masaa mawili, na begi lilikuwa zito kinouma nouma, mara nitokelezee mnazi moja, mara kama naenda Posta, mara nitokee hadi ilipo stend ya sahivi magerezani[emoji28][emoji28] Nikawa najiuliza hivi nipo siriaz kweli, [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]ukawa unaona mapicha picha
 
kwa upande wangu dar sijaenda Mara nyingi lakini kuna kipindi nilienda wakati naingia chuo. safari hii nilienda kubadilisha details za chuo pale tcu, maana nilikuwa nahama kutoka chuo kimoja kwenda kingine.

na pindi hiyo nilifikia huku picha ya ndege, so nilikuwa natoka pale picha ya ndege natembea mpaka maili moja kisha napanda gari kuelekea ubungo. nikifika ubungo nashuka naanza kutembea mpaka shekilango nakatisha naanza kuitafuta tcu.

nilipiga root kama siku mbili mfululizo, siku ya tatu wakati natoka kule tcu nikasema ngoja nitembee nione mji. Ukumbuke hii ilikuwa mara yangu ya kwanza kuingia dar yaani 2013 hiyo. Tofauti na hapo mara ya mwisho ilikuwa ni mwaka 2006, na kipindi hiki nilikuwa mdogo sana hivyo sikuwa najitambua.

basi bwana nikatoka pale tcu nikaanza kula mitaa nikibadilisha ule uelekeo wa kurudi shekilango.

muda si muda nikatokea sehemu fulani kuna mto. nikaanza kushangaa dar gani hii ina mito kama nipo mbalizi mbeya [emoji1787][emoji1787]
 
Back
Top Bottom